M’Cheyne Bible Reading Plan
Malaika Amtoa Petro Gerezani
12 Wakati huu mfalme Herode aliwatesa vikali baadhi ya waamini katika kanisa. 2 Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. 3 Alipoona kuwa kitendo hicho kimewapendeza Wayahudi, akaamuru Petro akamatwe. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate isiyotiwa chachu. 4 Baada ya kumkamata Petro walimweka jela chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, kila kikundi kikiwa na askari wanne. Herode alikuwa amepanga kumtoa Petro mbele ya Wayahudi baada ya Pasaka. 5 Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani; lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii. 6 Usiku ule ambao Herode alikuwa ameamua kumtoa kwa watu, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa kwa minyororo miwili, na askari wengine walikuwa wakilinda nje ya lango la gereza. 7 Mara malaika wa Bwana akatokea, na mwanga ukamulika ndani ya chumba. Yule malaika akampiga Petro ubavuni akamwamsha, akisema, “Haraka! Amka!” Na mara ile minyororo ikaanguka toka mikononi mwa Petro. 8 Yule malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, “Vaa koti lako unifuate.” 9 Petro alitoka mle gere zani akifuatana na malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitokea yalikuwa kweli. Alidhani alikuwa katika ndoto. 10 Wal ipita kituo cha askari wa kwanza, na kituo cha askari wa pili, ndipo wakafika katika lango la chuma la kutokea kuelekea mjini. Lango likafunguka lenyewe, wakatoka nje wakaelekea katika bara bara mojawapo . Mara yule malaika akamwacha Petro. 11 Ndipo Petro alipopata fahamu sawa sawa, akasema, “Sasa nina hakika ya kuwa Bwana amemtuma malaika wake aniokoe kutoka kwa Herode na maovu yote ambayo Wayahudi walikuwa wamekusudia kunitendea.”
12 Baada ya kutambua alipokuwa, Petro alikwenda nyumbani kwa Maria, mama yake Yohana Marko, ambako waamini wengi walikuwa wamekutana kwa maombi. 13 Petro alipobisha hodi mlangoni, mfany akazi msichana aitwaye Roda, akaja kumfungulia.
4 Lakini ali potambua sauti ya Petro, alirudi mbio kwa furaha kuwaambia wen gine kuwa Petro yuko nje, hata akasahau kumfungulia . 15 Wakam wambia yule msichana, “Una kichaa!” Lakini yeye alisisitiza kwamba ilikuwa ni kweli amesikia sauti ya Petro. Wakasema, “Ni malaika wake.” 16 Wakati huo Petro aliendelea kugonga mlangoni; nao walipofungua mlango wakamwona Petro, walistaajabu sana. 17 Lakini yeye aliwaashiria wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa jela. Akawaambia, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Akaondoka akaenda sehemu nyingine. 18 Kulipopam bazuka kukawa na hekaheka huko gerezani. Askari wakawa wanauli zana kuhusu yaliyompata Petro. 19 Herode akaamuru msako ufanyike lakini waliposhindwa kumpata Petro, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri hao askari wauawe. Basi Herode akatoka Yudea akaenda Kaisaria, akakaa huko.
Kifo Cha Herode
20 Herode alikuwa amekasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Watu wa miji hiyo miwili wakaungana pamoja wakapeleka wajumbe wakaonane na Herode. Wajumbe hao wakapata kibali cha Blasto, mtumishi mwaminifu wa Mfalme Herode, ili waonane na mfalme kutaka amani kwa kuwa miji hiyo ilipata chakula chake kutoka katika milki ya mfalme. 21 Siku ya hao wajumbe kumwona mfalme ilipofika, Herode alivaa mavazi rasmi ya kifalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi akaanza kutoa hotuba. 22 Alipokuwa akihutubu watu walimshangilia, wakapiga kelele wakisema, “Hii ni sauti ya Mungu! Sio sauti ya mwanadamu!” 23 Mara malaika wa Bwana akampiga Herode; akaliwa na funza akafa kwa sababu hakumpa Mungu utukufu. 24 Lakini neno la Mungu liliendelea kuenea na waamini wakaongezeka sana. 25 Barnaba na Sauli walipomaliza kazi yao walirudi Yerusalemu wakiwa pamoja na Yohana Marko.
Mafundisho Ya Kale
7 Mafarisayo na baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu walikusanyika mbele ya Yesu. 2 Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula bila kunawa kama ilivyotakiwa na sheria ya dini ya Wayahudi. 3 Wayahudi, na hasa Mafarisayo, hawali chakula pasipo kunawa kwa kufuata mila za wazee wao. 4 Na kwa sheria wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi nyingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu, na vyombo vya shaba.
5 Kwa hiyo wale Mafarisayo na walimu wa sheria walimwuliza Yesu, “Mbona wanafunzi wako hawafuati desturi za wazee wetu, na badala yake wa nakula kwa mikono najisi?”
6 Yesu akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa: ‘Watu hawa wanani heshimu kwa midomo yao, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. 7 Kuniabudu kwao ni bure. Wanafundisha watu amri zao badala ya sheria yangu.’ 8 Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushikilia desturi za watu.” 9 Akawaambia, “Mnaepuka kwa ujanja amri za Mungu ili mpate kutimiza desturi zenu! 10 Kwa mfano, Musa alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako’ na ‘Ye yote amtuka naye baba au mama auawe.’ 11 Lakini ninyi mnasema mtu akimwambia baba yake au mama yake kuwa, “Msaada ambao ningekupa ni Kor bani,” yaani umetengwa kama sadaka kwa Mungu, 12 basi hawaji biki tena kumsaidia baba yake au mama yake. 13 Kwa njia hiyo mnadhalilisha neno la Mungu kwa taratibu zenu mlizojiwekea. Na mnafanya mambo mengi ya jinsi hii.”
14 Yesu akaita tena ule umati wa watu akawaambia, “Nisiki lizeni nyote kwa makini na muelewe. 15 Hakuna kitu kinachomwin gia mtu kutoka nje ambacho kinaweza kumfanya mchafu. Kitu kina chotoka ndani yake ndicho kinachomfanya mchafu. 16 Mwenye nia ya kusikia na asikie.”
17 Alipoachana na wale watu aliingia ndani. Wanafunzi wake wakamwuliza maana ya mfano ule. 18 Akawajibu, “Hata nanyi hamwelewi? Hamtambui kwamba kitu kimwingiacho mtu kutoka nje hakiwezi kumfanya mchafu? 19 Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni, na baadaye hutolewa nje. Kwa kusema hivi, Yesu alifundisha kuwa aina zote za vyakula ni halali kuliwa.
20 Akaendelea kusema, “Kile kitokacho ndani ya mtu ndicho kinachomfanya awe mchafu. 21 Kwa maana ndani ya mtu, yaani moy oni mwake, hutoka: mawazo mabaya, uasherati, 22 wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matusi, kiburi na upumbavu. 23 Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, na ndio yanayomfanya mchafu.”
Yesu Amponya Binti Ya Mama Mtaifa
24 Ndipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia nyumba moja, ambapo hakupenda mtu afahamu yupo. Lakini hakuweza kujificha. 25 Mama mmoja ambaye binti yake mdogo ali kuwa na pepo mchafu aliposikia habari za Yesu, alikuja mara moja akajiangusha miguuni pake. 26 Huyo mama hakuwa Myahudi, alikuwa Mgiriki aliyezaliwa Siria-Foinike. Akamsihi Yesu amtoe binti yake huyo pepo mchafu.
27 Yesu akamwambia, “Tuwaache watoto wale washibe kwanza, kwa maana si halali kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”
28 Yule mama akajibu, “Ni kweli Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.” 29 Yesu akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, unaweza kwenda nyumbani. Yule pepo ameshamtoka binti yako.”
30 Akaenda nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo amemtoka.
Yesu Amponya Mtu Aliyekuwa Bubu Na Kiziwi
31 Yesu akaondoka katika eneo la Tiro, akapita katikati ya Sidoni akaenda hadi Ziwa la Galilaya kwa kupitia katika eneo la Dekapoli. 32 Hapo, watu walimletea kiziwi mmoja ambaye pia alikuwa hawezi kusema sawa sawa, wakamwomba amwekee mikono ili apone. 33 Yesu akampeleka yule kiziwi kando mbali na watu, akain giza vidole masikioni mwake kisha akatema mate na akaugusa ulimi wake. 34 Ndipo Yesu akatazama mbinguni, akahema kwa uchungu, akamwambia, “Efatha!” yaani “Funguka!” 35 Wakati huo huo masikio ya yule mtu yakafunguka na ulimi wake ukawa huru akaanza kusema vizuri.
36 Yesu akawaamuru wasimwambie mtu ye yote habari hizi. Lakini kadiri alivyowazuia ndivyo walivyozidi kutangaza habari zake. 37 Watu wakastaajabu mno. Wakasema, “Amefanya mambo yote vizuri mno! Amewawezesha viziwi wasikie na bubu waseme!”
Copyright © 1989 by Biblica