M’Cheyne Bible Reading Plan
Petro Aeleza Alivyotumwa Kwa Mataifa
11 Baadaye mitume na waamini wa sehemu zote za Yudea wakapata habari kwamba watu wasiokuwa Wayahudi nao wamepokea neno la Mungu. 2 Kwa hiyo Petro alipokwenda Yerusalemu, wale waliokuwa wakishikilia sheria ya tohara walimshutumu wakasema, 3 “Kwa nini ulikwenda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao?” 4 Ndipo Petro akaanza kuwaeleza mambo yote yalivyotokea akasema, 5 “Nil ikuwa nikiomba katika mji wa Jopa, nikaona katika ndoto kitu kama shuka kubwa ikishushwa chini kwa ncha zake nne, kutoka mbinguni, nayo ikanifikia. 6 Nilipotazama kwa makini nikaona wanyama wa kila aina, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani. 7 Nikasikia sauti ikiniambia, ‘Amka Petro, chinja, ule!’ 8 Nami nikasema, ‘La, Bwana! Sijawahi kula kitu cho chote kili chokatazwa na sheria zetu.’ 9 Lakini ile sauti kutoka mbinguni ikasema kwa mara ya pili, ‘Usiite kitu cho chote alichokitakasa Mungu kuwa ni uchafu.’ 10 Jambo hili lilitokea mara tatu ndipo vyote vikachukuliwa tena mpaka mbinguni. 11 Wakati huo huo watu watatu waliokuwa wametumwa kutoka Kaisaria wakawasili katika nyumba niliyokuwa nikikaa. 12 Roho akaniambia niende nao bila kusita. Nikaenda nao nikisindikizwa na hawa ndugu sita, tukaingia katika nyumba ya Kornelio. 13 Kornelio akatuambia jinsi malaika alivyomtokea akamwambia, ‘Tuma watu Jopa wakamwite Simoni aitwaye Petro. 14 Yeye anao ujumbe utakaokuokoa wewe na wote walio nyum bani mwako.’ 15 Nami nilipokuwa nikisema nao, Roho Mtakatifu akashuka juu yao kama alivyotushukia sisi mwanzoni. 16 Nami nikakumbuka jinsi Bwana alivyosema, ‘Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.’ 17 Basi kwa kuwa Mungu ndiye aliyewapa hawa watu karama ile ile aliyotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu, mimi ni nani hata nimpinge Mungu?” 18 Nao waliposikia maneno haya hawakuwa na la kusema. Wakamsifu Mungu, wakasema, “Mungu amewapa watu wa mataifa nafasi ya kutubu na kupokea uzima wa milele.’ ’
Kanisa Laenea Antiokia
19 Wale waamini waliotawanyika kutoka Yerusalemu wakati wa mateso yaliyotokana na kifo cha Stefano, walisafiri hadi Foinike na Kipro na Antiokia. Wakawa wakihubiri Habari Njema kwa Wayahudi peke yake. 20 Lakini baadhi yao walikwenda Antiokia wakitokea Kipro na Kirene. Wakawaambia Wagiriki Habari Njema za Bwana Yesu. 21 Roho wa Bwana alikuwa pamoja nao kwa hiyo watu wengi wakaamini na kumgeukia Bwana. 22 Habari hizi zilipowafikia vion gozi wa kanisa huko Yerusalemu, walimtuma Barnaba aende Antiokia. 23 Alipofika akaona jinsi Mungu alivyokuwa akiwabariki watu kwa neema yake, alifurahi sana akawatia moyo waendelee kwa juhudi kuwa waaminifu kwa Bwana. 24 Barnaba alikuwa mtu mwema aliyejawa Roho Mtakatifu, mwenye imani kuu; na watu wengi waliongoka wakam wamini Bwana. 25 Kisha Barnaba akasafiri kwenda Tarso kumtafuta Sauli. 26 Alipompata akaja naye mpaka Antiokia. Na wote wawili wakakaa huko kwa mwaka mzima, wakiwafundisha wengi walioamini katika kanisa la Antiokia. Hapo Antiokia ndipo waamini waliitwa ‘Wakristo’ kwa mara ya kwanza.
27 Wakati huu manabii walitoka Yerusalemu wakaenda Antiokia. 28 Na mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama katika mkutano aka tabiri kwa uweza wa Roho kwamba pangetokea njaa kubwa dunia nzima. Njaa hiyo ilitokea wakati Klaudio alipokuwa mtawala. 29 Waamini wakaamua kwamba kila mtu, kulingana na uwezo alio nao, atoe msaada upelekwe kwa ndugu waliokuwa wanaishi Yudea. 30 Wakafanya hivyo, na misaada ikapelekwa na Barnaba na Sauli kwa wazee wa kanisa.
Watu Wa Nazareti Wamkataa Yesu
6 Yesu akaondoka mahali hapo, akaenda mji wa kwao, akifu atana na wanafunzi wake. 2 Ilipofika siku ya sabato, alianza ku fundisha katika sinagogi na wengi waliomsikia walishangaa. Wakasema, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya? Amepataje kuwa na hekima ya namna hii? Amepata wapi uwezo wa kutenda miujiza ya namna hii? 3 Huyu si yule seremala mtoto wa Mariamu? Na ndugu zake si Yakobo, Yose, Yuda na Simoni? Dada zake si tuko nao hapa?” Basi hawakumwamini.
4 Yesu akawaambia, ‘ ‘Nabii huheshimiwa kila mahali isipokuwa katika mji wake na kati ya jamaa na ndugu zake.” 5 Hakufanya miujiza yo yote huko isipokuwa kuwagusa wagonjwa wachache na kuwaponya. 6 Alishangazwa sana na jinsi walivyokuwa hawana imani.
Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili
7 Akawaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili na akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu.
8 Akawaagiza wasichukue cho chote safarini isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mfuko, wala fedha. 9 Ila wavae viatu lakini wasichukue nguo ya kubadili. 10 Pia akawaambia, “Mkiin gia nyumba yo yote, kaeni hapo hapo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 11 Na mahali po pote ambapo hamtakaribishwa wala kusikili zwa, mtakapoondoka hapo, kung’uteni mavumbi yaliyoko miguuni mwenu, kama onyo lenu kwao.”
12 Kwa hiyo wakatoka, wakaenda wakihubiri kwamba watu wat ubu, waache dhambi. 13 Wakawatoa watu wengi pepo, wakawapaka mafuta wagonjwa wengi, wakawaponya.
Kifo Cha Yohana Mbatizaji
14 Mfalme Herode akapata habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limefahamika kila mahali. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka kwa wafu ndiyo maana uwezo wa kutenda miujiza unafanya kazi ndani yake!” 15 Wengine walisema, “Huyo ni Eliya!” Na wengine wakasema, “Ni nabii kama wale manabii wa zamani.” 16 Lakini Herode ali posikia habari hizi alisema, “Huyo ni Yohana Mbatizaji niliyem kata kichwa; amefufuka!” 17 Kwa maana Herode alikuwa ameagiza kwamba Yohana Mbatizaji akamatwe, awekwe gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa kaka yake, Filipo, ambaye alikuwa amemwoa. 18 Yohana alikuwa amemwambia Herode, “Si halali wewe kumwoa mke wa kaka yako.” 19 Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwe kea kinyongo Yohana akataka kumwua. Lakini hakupata nafasi, 20 kwa sababu Herode alimwogopa Yohana ambaye alifahamu kuwa ni mtu mwenye haki na mtakatifu, akawa anamlinda. Ingawa Herode alifadhaika sana kila alipomsikiliza Yohana, bado alipenda kumsi kiliza.
21 Baadaye Herodia alipata nafasi aliyokuwa akiitafuta. Wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwa mfalme Herode, mfalme alifanya sherehe kubwa, akawaalika viongozi wakuu wa ikulu, makamanda wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. 22 Binti yake Herodia akaja akacheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake. Mfalme Her ode akamwambia yule binti, “Niombe kitu cho chote utakacho, nami nitakupa.” 23 Akala kiapo akamwambia, “Cho chote utakachoomba, hata ikiwa ni nusu ya ufalme wangu, nitakupa.”
24 Yule binti akaenda akamwuliza mama yake, “Niombe nini?” Mama yake akajibu, “Mwombe kichwa cha Yohana Mbati zaji.” 25 Yule binti akarudi haraka kwa mfalme akamwambia, “Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia .” 26 Mfalme akajuta sana, lakini hakuweza kumkatalia kwa kuwa alikuwa ameapa mbele ya wageni wake, na hakupenda kuvunja ahadi yake. 27 Kwa hiyo Herode akamtuma mmojawapo wa walinzi wake mara moja akamwagiza alete kichwa cha Yohana. 28 Yule mlinzi akaenda gerezani akamkata Yohana kichwa kisha akakileta kwenye sinia akampa yule binti; naye akampatia mama yake.
29 Wanafunzi wa Yohana walipopata habari hizi, walikuja wakauchukua mwili wake, wakauzika kaburini.
Yesu Awalisha Watu Elfu Tano
30 Wale wanafunzi kumi na wawili waliporudi, walimweleza Yesu mambo yote waliyofanya na kufundisha. 31 Kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakakosa nafasi ya kula, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.” 32 Basi wakaondoka kwa mashua peke yao wakaenda mahali pasipo na watu.
33 Lakini watu waliowaona wakiondoka, wakawatambua. Wakawa tangulia mbio kwa miguu kutoka miji yote wakielekea kule waliko kuwa wakienda. Wakawahi kufika.
34 Yesu alipofika nchi kavu na kuuona huo umati wa watu, aliwaonea huruma kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.
35 Hata saa za mchana zilipoanza kupita, wanafunzi wake wakamwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa zimek wenda. 36 Waruhusu watu waondoke wakajinunulie chakula kwenye mashamba na vijiji vya jirani.”
37 Lakini Yesu akawajibu, “Wapeni ninyi chakula.” Wakam wambia, “Tunahitaji fedha nyingi sana, kununulia mikate ya kutosha kulisha watu wote hawa.”
38 Akawauliza, “Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Waliporudi wakamwambia, “Ipo mikate mitano na samaki wawili.”
39 Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye nyasi, 40 nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na hamsini hamsini. 41 Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili akatazama mbinguni, akashukuru, kisha akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. 42 Watu wote wakala, wakashiba. 43 Wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu kumi na viwili. 44 Idadi ya wanaume waliokula walikuwa elfu tano.
Yesu Atembea Juu Ya Maji
45 Wakati huo huo Yesu akawaamuru wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye anawaaga watu. 46 Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kusali. 47 Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imeshafika katikati ya ziwa na Yesu alikuwa peke yake nchi kavu. 48 Aliwaona wanafunzi wake wakihangaika na kuvuta makasia kwa nguvu kwa sababu upepo ulikuwa ukielekea walikotoka. Karibu na mapambazuko, Yesu aka waendea wanafunzi wake akitembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 49 lakini walipomwona akitembea juu ya maji, walid hani ni mzimu, wakapiga yowe, 50 kwa maana wote walimwona wakaogopa. Lakini mara Yesu akasema nao, “Tulieni! Ni mimi, msi ogope!” 51 Akapanda kwenye mashua yao na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa. 52 Walikuwa bado hawajaelewa hata maana ya u le muujiza wa mikate. Walikuwa bado hawajafunuliwa akilini mwao.
53 Walipokwisha kuvuka, walifika katika wilaya ya Gene zareti, wakatia nanga. 54 Waliposhuka kutoka katika mashua yao, watu walimtambua Yesu mara moja, 55 wakapita vijiji vyote haraka haraka, wakawabeba wagonjwa kwenye machela wakamfuata mahali po pote waliposikia kuwa yupo. 56 Na kila mahali Yesu alipokwenda, ikiwa ni vijijini, mijini na mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa angalao waguse pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa, waliponywa.
Copyright © 1989 by Biblica