M’Cheyne Bible Reading Plan
8 Na Sauli aliunga mkono kuuawa kwa Stefano Tangu siku hiyo waamini katika kanisa la Yerusalemu walianza kuteswa sana. Waamini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia katika majimbo ya Yudea na Samaria. 2 Watu waliomcha Mungu walimzika Stefano na kumwombolezea sana. 3 Lakini Sauli alitaka kulianga miza kanisa kabisa. Akawa akienda kila nyumba akawaburura waamini, wanaume kwa wanawake, akawatia jela.
Injili Yahubiriwa Samaria
4 Wale waamini waliotawanyika walihubiri neno la Mungu kila mahali walipokuwa. 5 Filipo naye alikwenda katika mji mmoja wa Samaria akahubiri habari za Kristo. 6 Watu wengi walipomsikiliza Filipo na kuona ishara za ajabu alizofanya, walizingatia kwa makini ujumbe wake. 7 Pepo wachafu walikuwa wakiwatoka watu wengi, huku wakipiga makelele; na wengi waliopooza na viwete, waliponywa. 8 Pakawa na furaha kuu katika mji huo.
9 Lakini katika mji huo alikuwepo mtu mmoja aitwaye Simoni, ambaye alikuwa mchawi. Kwa muda mrefu alikuwa amewapumbaza na kuwashangaza watu kwa mazingaombwe, akawa anajigamba kuwa yeye ni mtu maarufu. 10 Watu wa tabaka zote, wakubwa kwa wadogo, walivu tiwa sana naye, wakawa wanasema, “Bila shaka mtu huyu ndiye ile nguvu ya Mungu iitwayo ‘Uwezo Mkuu.’ ” 11 Wakamsikiliza kwa makini kwa sababu aliwastaajabisha kwa mazingaombwe yake. 12 Lakini watu walipoamini mahubiri ya Filipo kuhusu Habari Njema ya Ufalme wa Mungu, na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, waume kwa wake. 13 Hata Simoni naye aliamini na alipokwisha batizwa aliambatana na Filipo. Alipoona ishara na miujiza aliy ofanya Filipo alistaajabu sana .
14 Basi mitume waliokuwa Yerusalemu waliposikia kuwa watu wa Samaria wameamini neno la Bwana, waliwatuma Petro na Yohana waende huko. 15 Nao walipofika waliwaombea ili wapokee Roho Mta katifu; 16 kwa maana walikuwa wamebatizwa tu katika jina la Bwana Yesu na Roho Mtakatifu alikuwa bado hajawashukia. 17 Petro na Yohana wakaweka mikono yao juu ya wale waliobatizwa, nao waka pokea Roho Mtakatifu. 18 Simoni alipoona kuwa watu walipokea Roho Mtakatifu mitume walipoweka mikono juu yao, aliwapa fedha 19 akasema, “Nipeni na mimi uwezo huu ili kila mtu nitakayeweka mikono yangu juu yake apokee Roho Mtakatifu.” 20 Petro akam jibu, “Uangamie wewe na fedha zako, kwa maana unadhani unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!” 21 Wewe huwezi kuwa na sehemu wala fungu katika jambo hili kwa kuwa moyo wako hauko sawa mbele za Mungu. 22 Kwa hiyo tubu, uache huu uovu wako; na umwombe Mungu ili kama inawezekana akusamehe makusudio maovu uliyo nayo moyoni. 23 Kwa maana ninaona wazi kwamba wewe umejawa na wivu na ni mfungwa wa dhambi. 24 Simoni akajibu, “Niombeeni kwa Bwana, ili hayo mliyosema yasije yakanipata.” 25 Nao wali pokwisha kutoa ushuhuda na kufundisha neno la Bwana, walirudi Yerusalemu; na walipokuwa wakisafiri walihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.
Filipo Ambatiza Afisa Wa Ethiopia
26 Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara itokayo Yerusalemu kuelekea Gaza.” Hii ilikuwa barabara iendayo jangwani. 27 Filipo akaondoka akaenda. Wakati huo Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa waziri wa fedha wa Kandake, Malkia wa Ethiopia, alikuwa anarudi nyumbani baada ya kumwabudu Mungu huko Yerusalemu. 28 Alikuwa amekaa kwenye gari la kuvutwa na farasi akielekea makwao, akisoma kitabu cha nabii Isaya. 29 Roho wa Mungu akamwambia Filipo, “Nenda kasimame karibu na lile gari.” 30 Kwa hiyo Filipo aka harakisha kulikaribia, na alipofika karibu akamsikia yule afisa akisoma katika kitabu cha nabii Isaya, akamwuliza, “Je, unaelewa unachosoma?” 31 Yule afisa akamjibu, “Nitaelewaje mtu asipo nielekeza? Akamkaribisha Filipo katika gari, akaketi pamoja naye. 32 Maneno aliyokuwa akisoma ni haya, ‘Alipelekwa kama kon doo anayetolewa kuchinjwa na kama mwana-kondoo anavyotulia anapo katwa manyoya, naye hakusema neno lo lote. 33 Aliaibishwa, aka nyimwa haki yake. Ni nani awezaye kuelezea juu ya kizazi chake? Kwa maana uhai wake umeondolewa duniani.’ 34 Yule towashi akam wuliza Filipo, “Tafadhali niambie, Isaya alikuwa akisema haya juu yake mwenyewe au juu ya mtu mwingine?” 35 Ndipo Filipo akaanza kusema naye, akitumia Maandiko haya akamweleza Habari Njema za Yesu. 36 Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, na yule towashi akamwambia Filipo, “ Tazama, hapa kuna maji! Kuna kitu gani cha kunizuia mimi nisiba tizwe? [ 37 Filipo akamwambia, “Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”] 38 Akaamuru gari lisimamishwe. Wakateremka, yule towashi na Filipo, wakaenda pale kwenye maji. Filipo akamba tiza. 39 Walipotoka katika yale maji, Roho wa Bwana akamchukua Filipo na yule towashi hakumwona tena. Kwa hiyo akaendelea na safari yake akiwa amejawa na furaha. 40 Filipo akajikuta yuko Azoto; akasafiri akihubiri Injili katika miji yote mpaka alipo fika Kaisaria.
Yesu Amponya Mtu Aliyelemaa Mkono
3 Yesu aliingia tena katika sinagogi na mtu mmoja aliyelemaa mkono alikuwapo pia. 2 Baadhi ya watu waliokuwa wakimtega, ili wapate sababu ya kumshtaki, walimtazama kwa makini waone kama atamponya huyo kilema siku ya sabato. 3 Yesu akamwambia yule mwe nye mkono uliolemaa, “Njoo hapa mbele.”
4 Yesu akawauliza, “Ni lipi lililo halali siku ya sabato? Kufanya jema, au baya? Kusalimisha maisha au kuua?” Wakakaa kimya.
5 Yesu akawatazama kwa hasira, akahuzunishwa na ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akauny oosha, nao ukapona kabisa! 6 Kisha Mafarisayo wakatoka nje, wakaenda kushauriana na kundi la wafuasi wa Herode mbinu za kum wua Yesu.
Umati Wa Watu Wamfuata Yesu
7 Yesu pamoja na wanafunzi wake waliondoka mahali hapo wakaenda ziwani wakifuatwa na umati mkubwa wa watu kutoka Gali laya na Yudea. 8 Na watu kutoka Yerusalemu, Idumaya, na eneo lote la ng’ambo ya Yordani, sehemu za Tiro na Sidoni, waliposi kia mambo aliyokuwa akitenda, wakamwendea. 9 Akawaomba wanafunzi wake wamwandalie mashua ili asisongwe na kubanwa sana na watu. 10 Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wote wenye mar adhi walikuwa wakisukumana wapate kumgusa. 11 Na kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia kwa sauti kuu, “Wewe ni Mwana wa Mungu.” 12 Lakini aliwaamuru wasimtambulishe kwa watu.
Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili
13 Yesu alipanda mlimani akawaita wale aliowataka, nao wakaja. 14 Akawachagua kumi na wawili wafuatane naye na awatume kuhubiri na 15 wawe na mamlaka ya kufukuza pepo. 16 Hawa ndio aliowachagua: Simoni, ambaye alimwita Petro, 17 Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo ambao aliwaita Boanerge, yaani wana wa ngurumo; 18 Andrea; Filipo; Bartholomayo; Mathayo; Tomaso; Yakobo, mwana wa Alfayo; Thadayo; Simoni, Mkanaani; na 19 Yuda
Yesu Na Beelzebuli
20 Yesu akarudi nyumbani. Umati wa watu ukamfuata tena, hata yeye na wanafunzi wake wakashindwa kula chakula. 21 Ndugu zake walipopata habari walikuja kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”
22 Walimu wa sheria waliotoka Yerusalemu walikuwa wakisema, “Amepagawa na Beelzebuli, mkuu wa mashetani; na ni kwa uwezo wa Beelzebuli anawafukuza mashetani.”
Beelzebuli anawafukuza mashetani.”
23 Basi Yesu akawaita akazungumza nao kwa mifano: “Shetani awezaje kufukuza shetani? 24 Ikiwa utawala wa nchi umegawanyika wenyewe, hauwezi kudumu. 25 Hali kadhalika kama jamaa moja ime gawanyika yenyewe kwa yenyewe, jamaa hiyo haiwezi kudumu. 26 Na kama shetani akijipiga vita yeye mwenyewe hatatimiza cho chote ila mwisho wake umekaribia. 27 Pia hakuna mtu awezaye kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumwibia vitu vyake vyote pasipo kwanza kumfunga huyo mwenye nyumba mwenye nguvu. Akisha mfunga, ndipo anaweza kumwibia kila kitu.
28 “Nawaambieni kweli, dhambi zote watendazo wanadamu na maneno yote ya kufuru wasemayo, watasamehewa. 29 Lakini ye yote anayemtukana Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.” 30 Yesu alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema ana pepo mchafu.
Mama Na Ndugu Wa Yesu
31 Mama yake Yesu na ndugu zake wakafika wakasimama nje wakamtuma mtu amwite. 32 Umati wa watu waliokuwa wameketi kum zunguka wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wana kutafuta.”
33 Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni akina nani?”
34 Akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka, akasema, “Hawa ndio mama zangu na ndugu zangu. 35 Mtu ye yote anayetenda mapenzi ya Mungu ndiye ndugu yangu na dada yangu na mama yangu.”
Copyright © 1989 by Biblica