M’Cheyne Bible Reading Plan
Petro Amponya Mlemavu Kwa Jina La Yesu
3 Siku moja Petro na Yohana walikwenda Hekaluni saa tisa kwa sala ya adhuhuri. 2 Karibu na mlango uitwao Mzuri, palikuwa na mtu aliyekuwa amelemaa tangu kuzaliwa. Kila siku huyo mlemavu aliwekwa karibu na lango la Hekalu akawa akiomba fedha kwa watu waliokuwa wakiingia ndani ya Hekalu. 3 Alipowaona Petro na Yohana wakielekea Hekaluni, aliwaomba wampe cho chote. 4 Wakamkazia macho, kisha Petro akamwambia, “Tuangalie!” 5 Akawakodolea macho akitazamia kupata kitu kutoka kwao.
6 Lakini Petro akamwambia, “Sina fedha wala dhahabu za kukupa, lakini nitakupa kile nilicho nacho. Kwa jina la Yesu wa Nazareti nakuamuru, tembea!” 7 Petro akamshika yule mtu mkono, akamwinua, akasimama kwa miguu yake mwenyewe. Mara miguu na viungo vyake vikapata nguvu. 8 Akaruka juu, akasimama, akaingia Hekaluni pamoja na Petro na Yohana, huku akirukaruka na kumsifu Mungu. 9 Watu wote walimwona akitembea na kumsifu Mungu 10 wakam tambua kuwa ni yule mlemavu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango akiomba omba. Wakashangaa mno kuhusu maajabu yaliyomtokea.
Petro Anashuhudia Kuwa Yesu Aponya
11 Yule mtu aliyeponywa alipokuwa bado anawang’ang’ania Petro na Yohana, watu wakawakimbilia mpaka kwenye ukumbi wa Sule mani wakiwa wamejawa na mshangao.
12 Petro alipoona watu wamekusanyika aliwaambia, “Watu wa Israeli, kwa nini mnastaajabu kuhusu jambo hili? Mbona mnatukazia macho kwa mshangao? Mnadhani ni kwa uwezo wetu au utakatifu wetu tumemwezesha mtu huyu kutembea? 13 Sivyo! Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo na wa baba zetu amemtukuza mtumishi wake Yesu kwa muujiza huu. Ninyi mlimtoa ahukumiwe kifo na mkamkana mbele ya Pilato ijapokuwa Pilato alitaka kufuta mashtaka na kumwachilia. 14 Ninyi mlimkataa aliyekuwa Mtakatifu na Mwenye Haki mkaomba mpewe yule muuaji. 15 Hivyo mkamwua aliye chanzo cha Uzima, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Sisi ni mashahidi wa mambo haya. 16 Imani katika jina la Yesu imempa nguvu huyu mtu ambaye mnamwona na kumfahamu. Ni kwa jina la Yesu na imani inay opatikana kwake ambayo imemponya huyu mtu kabisa, kama ninyi wenyewe mnavyoona.
17 “Na sasa ndugu zangu, najua ya kuwa mambo mliyomtendea Yesu, ninyi na viongozi wenu, mliyafanya kwa kutokujua. 18 Lakini Mungu alikuwa ametabiri kwa njia ya manabii wake wote kwamba Kristo angeteswa, na hivi ndivyo alivyotimiza utabiri huo. 19 Kwa hiyo tubuni mumgeukie Mungu, ili azifute dhambi zenu, 20 na mpate nguvu za kiroho kutoka kwa Bwana. Naye atampeleka Kristo, yaani Yesu, ambaye alichaguliwa tangu awali kwa ajili yenu. 21 Yeye hana budi kukaa mbinguni mpaka wakati Mungu ataka pofanya kila kitu kuwa kipya tena, kama alivyotamka tangu zamani, kwa kupitia kwa manabii wake watakatifu. 22 Kama Musa alivy osema, ‘Bwana Mungu atawateulia nabii kati ya ndugu zenu kama alivyoniteua mimi. Mtamtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia. 23 Mtu ye yote ambaye hatamsikiliza huyo nabii, atatengwa daima na watu wake na kuangamizwa.’
24 “Manabii wote tangu wakati wa Samweli na kuendelea pia walitabiri kuhusu siku hizi. 25 Ninyi ni wana wa manabii na wa ile ahadi ambayo Mungu aliwapa baba zenu, alipomwambia Abrahamu, ‘Kutokana na uzao wako familia zote ulimwenguni zitabarikiwa.’ 26 Mungu alipomfufua mtumishi wake alimtuma kwenu kwanza ili awaletee baraka kwa kuwawezesha kuacha uovu wenu.”
Mpango Wa Kumwua Yesu
26 Yesu alipomaliza kusema hayo yote, aliwaambia wanafunzi wake, 2 “Mnafahamu kwamba sikukuu ya Pasaka inaanza baada ya siku mbili na mimi Mwana wa Adamu nitasalitiwa na kusulubiwa.”
3 Wakati huo makuhani wakuu na wazee walifanya mkutano katika ukumbi wa kuhani mkuu, jina lake, Kayafa. 4 Wakashauriana jinsi ya kumkamata Yesu na kumwua kwa siri. 5 Wakasema, “Lakini tusi fanye haya wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.”
Yesu Anapakwa Mafuta Bethania
6 Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, 7 mwa namke mmoja alimjia akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya thamani kubwa; akammiminia Yesu manukato hayo kichwani akiwa ame kaa mezani. 8 Lakini wanafunzi wake walipoona hayo waliudhika, wakasema, “Kwa nini kupoteza manukato bure? 9 Haya yangaliuzwa kwa bei kubwa na fedha hizo wakapewa maskini.”
10 Yesu alifahamu mawazo yao kwa hiyo akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mama? Amenifanyia jambo zuri sana. 11 Maskini mnao siku zote lakini hamtakuwa nami siku zote. 12 Aliponimimi nia haya manukato alikuwa akiandaa mwili wangu kwa mazishi. 13 Ninawaambia kweli, mahali po pote Habari Njema itakapohubi riwa ulimwenguni, jambo hili alilofanya litatajwa, kwa ukumbusho wake.”
Yuda Akubali Kumsaliti Yesu
14 Kisha mmojawapo wa wale wanafunzi kumi na wawili aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa kuhani mkuu akamwambia, “Mtanilipa kiasi gani nikimtoa kwenu?” 15 Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. 16 Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti Yesu.
Matayarisho Ya Pasaka
17 Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate isiotiwa chachu wale wanafunzi walikuja kwa Yesu wakamwuliza, “Ungependa tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?”
18 Akajibu, “Nendeni kwa mtu fulani huko mjini mkamwambie, ‘Bwana anasema hivi: saa yangu imekaribia, napenda kula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu nyumbani kwako.’ ” 19 Wanafunzi waka fanya kama Yesu alivyowaambia, wakaandaa Pasaka.
20 Ilipofika jioni, Yesu aliketi mezani pamoja na wanafunzi wake. 21 Walipokuwa wakila akawaambia, “Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti.” 22 Wakasikitika sana, wakaanza kumwul iza mmoja mmoja, “Ni mimi, Bwana?” 23 Yesu akawaambia, “Yule aliyechovya mkono wake katika bakuli pamoja nami, ndiye ata kayenisaliti. 24 Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama ilivy oandikwa katika Maandiko, lakini ole wake mtu yule atakayenisal iti. Ingalikuwa nafuu kwake kama hakuzaliwa!”
25 Kisha Yuda, yule ambaye alimsaliti akasema, “Ni mimi, Bwana?” Yesu akamjibu, “Umetamka mwenyewe.”
Bwana?” Yesu akamjibu, “Umetamka mwenyewe.”
26 Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, “Chukueni mle; huu ni mwili wangu.” 27 Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa akisema, “Kunyweni nyote katika kikombe hiki. 28 Hii ni damu yangu ya agano ambayo inamwagika kwa ajili ya wengi ili wasame hewe dhambi. 29 Ninawahakikishia kuwa sitakunywa tena maji ya mzabibu mpaka siku nitakapoyanywa pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu.”
Baba yangu.”
30 Walipokwisha kuimba wimbo walikwenda kwenye mlima wa Mizeituni.
Yesu Amwambia Petro Atamkana
31 Kisha Yesu akawaambia, “Usiku wa leo kila mmoja wenu atanikimbia kwa maana Maandiko yanasema, ‘Nitampiga mchungaji, na kondoo wote wa kundi lake watatawanyika.’ 32 Lakini baada ya kufufuka, nitawatangulia kwenda Galilaya.”
33 Petro akasema, “Hata kama wote watakuacha, mimi sitaku acha.”
34 Yesu akamjibu, “Ninakuambia kweli, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” 35 Lakini Petro akasema, “Hata kama itabidi nife pamoja na wewe, sitakukana.” Na wana funzi wote wakasema hivyo hivyo.
Gethsemane
36 Kisha Yesu akaenda nao mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane. Akawaambia, “Kaeni hapa, mimi ninakwenda mbele zaidi kuomba.” 37 Akamchukua Petro, pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kufadhaika na kuhuzunika. 38 Kisha Yesu akawaambia, “Moyo wangu umejaa majonzi karibu ya kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami.”
39 Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi akaomba, “Baba yangu, kama inawezekana, niondolee kikombe hiki cha mateso, lakini si kama nipendavyo bali kama upendavyo wewe.”
40 Akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamwul iza Petro, “Hamkuweza kukesha nami hata kwa saa moja? 41 Kesheni muombe, msije mkaingia katika majaribu. Kwa maana roho i radhi lakini mwili ni dhaifu.” 42 Akaenda tena mara ya pili, akaomba, “Baba yangu, kama haiwezekani kikombe hiki kion dolewe pasipo mimi kukinywea, mapenzi yako yafanyike.” 43 Ali porudi tena aliwakuta wamelala kwa maana macho yao yalikuwa mazito. 44 Kwa hiyo akawaacha akaenda tena mara ya tatu, akaomba vile vile.
45 Kisha akarudi kwa wale wanafunzi akawaambia, “Bado mme lala na kupumzika? Angalieni, saa imefika ambapo mimi Mwana wa Adamu sina budi kukabidhiwa mikononi mwa wenye dhambi. 46 Amkeni, twendeni! Yule anayenisaliti atafika sasa hivi!”
Yesu Akamatwa
47 Alipokuwa anazungumza, Yuda, mmojawapo wa wale kumi na wawili, akafika,akifuatana na umati wa watu wenye mapanga na mar ungu. Walikuwa wametumwa na makuhani wakuu na wazee wa watu.
48 Yuda alikuwa amepatana na hao watu kuwa, ‘Nitakayembusu ndiye, mkamateni.’ 49 Basi alipofika, alimwendea Yesu moja kwa moja, akamsalimia, “Salaam, Rabi!” Akambusu. 50 Yesu akamjibu, “Rafiki, umekuja kufanya nini hapa?” Basi wale watu wakasogea, wakamkamata Yesu. 51 Ndipo mmojawapo wa wafuasi wa Yesu ali poona hivyo, akachukua panga lake, akampiga nalo mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 52 Yesu akamwambia, “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote watumiao upanga watakufa kwa upanga. 53 Unadhani siwezi kumwomba Baba yangu aniletee mara moja majeshi kumi na mbili ya malaika? 54 Lakini nikifanya hivyo yatatimiaje Maandiko yale yasemayo kwamba mambo haya lazima yato kee?”
55 Wakati huo Yesu akawaambia ule umati, “Mmekuja kunika mata kama mnyang’anyi kwa mapanga na marungu? Mbona siku zote nilikaa Hekaluni na kufundisha lakini hamkunikamata? 56 Lakini haya yametokea ili Maandiko ya manabii yatiimie.” Ndipo wana funzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.
Yesu Ashtakiwa Mbele Ya Baraza
57 Wale waliomkamata Yesu wakampeleka nyumbani kwa Kayafa, kuhani mkuu, ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekutanika.
58 Lakini Petro alimfuata kwa mbali mpaka uani kwa kuhani mkuu akaingia ndani pamoja na walinzi aone litakalotokea. 59 Basi makuhani wakuu na baraza zima wakatafuta ushahidi wa uongo ili wamwue Yesu, 60 lakini hawakupata, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza. Hatimaye wakajitokeza watu wawili, 61 wakasema: “Huyu mtu alisema, ‘Nina uwezo wa kuvunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena katika muda wa siku tatu .’ ”
62 Kisha kuhani mkuu akasimama, akamwambia Yesu, “Huna jibu? Husikii huo ushahidi waliotoa watu hao?” 63 Lakini Yesu hakusema neno. Basi kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha kwa jina la Mungu aliye hai, tuambie kama wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu.”
Mungu.”
64 Yesu akajibu, “Umetamka mwenyewe. Lakini nina waambieni nyote kwamba baada ya hapa, mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wa Mungu mwenye uweza na akija juu ya mawingu ya mbin guni.”
65 Aliposikia maneno hayo, kuhani mkuu alirarua mavazi yake akasema, “Amekufuru! Tunahitaji ushahidi gani zaidi? Si mmemsi kia akikufuru? 66 Mnaamuaje?” Wakajibu, “Anastahili kufa!”
67 Kisha wakamtemea mate usoni; wengine wakampiga ngumi na makofi, 68 wakasema, “Hebu toa unabii wewe Kristo! Ni nani ame kupiga?”
69 Wakati huo Petro alikuwa amekaa uani. Mtumishi mmoja wa kike akamjia akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.” 70 Lakini Petro akakana mbele yao wote akisema, “Sijui usemalo.”
71 Kisha alipotoka nje, mlangoni mtumishi mwingine wa kike alimwona, akawaambia watu waliokuwapo, “Huyu mtu alikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 72 Akakana tena kwa kiapo akisema, “Simfa hamu mtu huyo!” 73 Baada ya muda mfupi wale waliokuwa wamesi mama pale walimwendea Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao kwa maana namna yako ya kusema ni kama yao.” 74 Ndipo Petro akalaani na kuapa, akawaambia, “Simfahamu mtu huyo!” Wakati huo huo jogoo akawika. 75 Na Petro akakumbuka Yesu alivyomwambia, “Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu.” Akaenda nje, akalia kwa uchungu.
Copyright © 1989 by Biblica