M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Ajitambulisha Kwa Wanafunzi Saba
21 Baada ya haya Yesu alijitambulisha tena kwa wanafunzi wake kando ya bahari ya Tiberia. Ilitokea hivi: 2 Simoni Petro, Tomaso aitwaye Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. 3 Simoni Petro aka waambia wenzake, “Mimi nakwenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua. Lakini usiku ule hawakupata cho chote. 4 Kulipopambazuka, Yesu alisimama ufukoni, lakini wale wana funzi hawakumtambua. 5 Yesu akawaambia, “Wanangu, mmepata samaki wo wote?” Wakamjibu, “La.” 6 Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kulia wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Walivyofa nya hivyo walipata samaki wengi mno hata wakashindwa kuingiza ule wavu uliojaa samaki katika mashua! 7 Kisha yule mwanafunzi ali yependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Petro aliposikia haya akajifunga nguo yake, kwa kuwa alikuwa amevua wakati wakifa nya kazi, akajitosa baharini, akaogelea kuelekea ufukoni. 8 Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakivuta ule wavu uliojaa samaki. Hapo walipokuwa wakivua hapakuwa mbali na nchi kavu; ilikuwa kama hatua mia moja hivi.
9 Walipowasili nchi kavu, wakaona moto wa mkaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate. 10 Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua.” 11 Simoni Petro akaenda akauvuta ule wavu ambao ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na tatu, akauleta ufukoni. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 12 Yesu akawaambia, “Njooni mle.” Hakuna hata mmoja wao aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua hakika ya kuwa ni Bwana. 13 Yesu akaenda akachu kua ile mikate na baadaye samaki, akawagawia. 14 Hii ilikuwa ni mara ya tatu Yesu kujitambulisha kwa wanafunzi wake tangu afufuke kutoka kwa wafu.
Yesu Amwuliza Petro Kama Anampenda
15 Walipokwisha kula, Yesu akamwuliza Simoni Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?” Yeye akamjibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wana kondoo wangu.” 16 Kwa mara nyingine Yesu akamwul iza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akajibu, “Ndio Bwana, wewe unajua ya kuwa nakupenda.” Akamwam bia, “Chunga kondoo wangu.” 17 Kwa mara ya tatu Yesu akamwul iza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?” Petro akahuzu nika sana kwa kuwa Yesu alimwuliza mara ya tatu, ‘Unanipenda?’ Akamjibu, “Bwana, wewe unajua kila kitu. Unajua ya kuwa naku penda.” Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu. 18 Nakuambia wazi, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka; lakini ukiwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika nguo na kukupeleka usipotaka kwenda.” 19 Alisema haya ili kumfahamisha Petro jinsi atakavyokufa, na kwa kifo hicho Mungu atukuzwe. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate.” 20 Petro akageuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. Huyu mwanafunzi ndiye yule aliyekaa karibu kabisa na Yesu alipokula naye chakula cha mwisho akauliza, ‘Bwana, ni nani atakayekusaliti?’ 21 Petro alipomwona huyo mwanafunzi akamwuliza Yesu, “Bwana, na huyu je?” 22 Yesu akamjibu, “ Ikiwa nataka aishi mpaka nitakapo rudi, inakuhusu nini? Wewe nifuate!” 23 Kwa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea kati ya ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini?”
24 Huyu ndiye yule mwanafunzi ambaye anashuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushu huda wake ni wa kweli.
1 Kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu na Timotheo ndugu yetu. 2 Kwa ndugu katika Kristo, watakatifu na waaminifu waishio Kolosai. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
Shukrani Na Maombi
3 Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea. 4 Kwa maana tumepata habari juu ya imani yenu katika Kristo Yesu na upendo wenu kwa watu wote wa Mungu. 5 Imani hii na upendo umetokana na tumaini mlilowekewa mbinguni na ambalo mmelisikia katika neno la kweli, yaani Habari Njema. 6 Duniani kote, hii Habari Njema iliyowajia inaenea na kuzaa mat unda kama ilivyokuwa kwenu mlipoisikia na kuelewa neema ya Mungu kwa kina.
7 Mlijifunza juu ya Habari Njema kutoka kwa mtumishi mwenzenu mpendwa, Epafra. Yeye ni mhudumu mwaminifu wa Kristo ambaye ana fanya kazi kwa niaba yetu, 8 naye ametufahamisha juu ya upendo wenu mliopewa na Roho.
9 Kwa sababu hii, tangu tuliposikia habari zenu, hatujaacha kuwaombea. Tunamsihi Mungu awape kwa wingi, maarifa ya kujua mapenzi yake, kwa njia ya hekima ya kiroho na ufahamu. 10 Ili mpate kuishi maisha yanayomtukuza Bwana na kumpendeza kabisa: mkizaa matunda kwa kila kazi njema na kukua katika kumjua Mungu. 11 Tunawaombea pia muimarishwe na nguvu zote kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake; mpate kuwa na subira na uvumilivu, huku 12 mkimshukuru kwa furaha Baba aliyewafanya mustahili kuwa na fungu katika urithi wa watakatifu, katika ufalme wa nuru. 13 Kwa maana ametuokoa kutoka katika nguvu za giza, akatuweka katika ufalme wa Mwanae mpendwa, 14 ambaye ametukomboa kwa damu yake, tukapata msamaha wa dhambi.
Ukuu Wa Kristo
15 Kristo anafanana kabisa na Mungu asiyeonekana. Yeye ali kuwepo kabla Mungu hajaumba kitu cho chote. 16 Yeye ndiye ali yeumba vitu vyote mbinguni na duniani; vitu vinavyoonekana na visivyoonekana; kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala au milki na mamlaka: vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake. 17 Yeye alikuwapo kabla ya vitu vingine vyote na kwa uwezo wake vitu vyote vinahusiana kwa mpango. 18 Yeye ni kichwa cha mwili, yaani kanisa lake; naye ni wa kwanza na mzaliwa wa kwanza wa wale wote wanaofufuka kutoka kwa wafu, ili yeye peke yake awe mkuu katika vitu vyote. 19 Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba ukamil ifu wake wote wa kimungu uwe ndani ya Mwanae; 20 na kwamba kwa njia ya mwanae vitu vyote vilivyoko duniani na vilivyoko mbinguni vipatanishwe na Mungu, kwa ajili ya damu yake iliyomwagwa msala bani kuleta amani.
21 Hapo kwanza ninyi mlikuwa mmefarakana na Mungu na mlikuwa maadui zake kwa sababu ya mawazo na matendo yenu maovu. 22 Lakini sasa Mungu amewapatanisha naye kwa njia ya mwili wa Kristo katika kifo, ili awaweke mbele yake mkiwa watakatifu, bila doa wala lawama. 23 Lakini hamna budi kuendelea kuwa imara na thabiti katika imani yenu, pasipo kuyumba katika tumaini lililomo katika Injili. Hii ndio ile Injili mliyoisikia na ambayo imetan gazwa kwa kila kiumbe duniani na ambayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi wake.
Huduma Ya Paulo Kwa Makanisa
24 Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu na kwa mateso yangu ninakamilisha kile ambacho kimepungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa lake. 25 Mimi nime kuwa mtumishi wa kanisa kufuatana na wajibu niliopewa na Mungu, kuwasilisha kwenu neno la Mungu kwa ukamilifu. 26 Hii ni siri ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyingi na vizazi vingi viliv yopita, lakini sasa imefunuliwa kwa watu wa Mungu. 27 Kwao, Mungu amependa kudhihirisha kati ya mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, yaani, Kristo ndani yenu ndiye tumaini pekee la utu kufu.
28 Kwa sababu hii tunamtangaza Kristo, tukiwaonya na kuwa fundisha watu wote kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya Mungu akiwa amekamilika katika Kristo. 29 Kwa shabaha hii nina fanya kazi, nikijitahidi kwa nguvu kuu ya Kristo inay ofanya kazi kwa uwezo mkuu ndani yangu.
Copyright © 1989 by Biblica