M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Ahukumiwa Kifo
19 Ndipo Pilato akamtoa Yesu akaamuru apigwe viboko. 2 Askari wakasuka taji ya miiba wakamwekea Yesu kichwani, wakamvika na kanzu ya zambarau.
3 Lakini walipomkaribia Yesu wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu.
Mfalme wa Wayahudi!’
5 Kwa hiyo Yesu akatoka nje akiwa amevaa ile taji ya miiba na kanzu ya zambarau. Pilato akawaambia, “Huyu hapa mtu wenu.” 6 Wale makuhani wakuu na viongozi wa Wayahudi walipomwona wakapiga kelele, “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawajibu, “Mchukueni mumsulubishe ninyi, kwa sababu mimi sioni kosa alilo tenda.” 7 Wao wakamjibu, “Sisi tunayo sheria ambayo inamhukumu kifo kwa sababu yeye anajiita Mwana wa Mungu.” 8 Pilato aliposi kia haya aliingiwa na hofu. 9 Akaingia ukumbini tena akamwuliza Yesu, “Wewe unatoka wapi?” Lakini Yesu hakumjibu. 10 Pilato akamwambia, “Kwa nini hunijibu? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukuachilia huru au kukusulubisha?” 11 Ndipo Yesu akamwambia, “Wewe hungekuwa na mamlaka ye yote juu yangu kama Mungu hakukupa mamlaka hayo; kwa hiyo mtu aliyenishtaki kwako ana dhambi kubwa zaidi.” 12 Tangu wakati huo Pilato akaanza kutafuta njia ya kumfungua Yesu, lakini Wayahudi wakazidi kupiga kelele wakasema, “Ukimwachilia huyu mtu, wewe si rafiki wa Kaisari. Mtu ye yote anayejifanya kuwa mfalme anampinga Kaisari.” 13 Pilato aliposi kia maneno haya alimtoa Yesu nje tena akaketi katika kiti chake cha kuhukumia, mahali palipoitwa Sakafu ya Jiwe - kwa Kiebrania paliitwa Gabatha.
14 Siku hiyo ilikuwa ni siku moja kabla ya Pasaka, siku iliyoitwa siku ya Matayarisho, yapata kama saa sita hivi. Pilato Akawaambia Wayahudi, “Huyu hapa Mfalme wenu!” 15 Wao wakapiga kelele, “Mwondoe! Mwondoe! Msulubishe!” Pilato akawauliza, “Je, nimsulubishe Mfalme wenu?” Wale makuhani wakuu wakamjibu, “Hatuna mfalme mwingine ila Kaisari.” 16 Ndipo Pilato akawaka bidhi Yesu wamsulubishe.
Yesu Asulubishwa
17 Kwa hiyo wakamchukua Yesu, naye akatoka akiwa amebeba msalaba wake kuelekea mahali palipoitwa, ‘Fuvu la kichwa,’ au kwa Kiebrania, Golgotha. 18 Hapo ndipo walipomsulubisha. Pamoja naye walisulubishwa watu wengine wawili, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia wa Yesu. 19 Pilato aliandika maneno yafuatayo kwenye kibao, kikawekwa juu kwenye msalaba wa Yesu: “YESU WA NAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI” 20 Kwa kuwa mahali hapo palikuwa karibu na mjini, Wayahudi wengi walisoma maneno haya ambayo yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiebrania, Kilatini na Kigiriki. 21 Makuhani wakuu wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi,’ bali ‘Mtu huyu alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi.”’ 22 Pilato akawajibu, “ Nilichokwisha andika, nimeandika.”
Mavazi Ya Yesu Yagawanywa
23 Maaskari walipokwisha msulubisha Yesu, walichukua mavazi yake wakayagawa mafungu manne; kila askari akapata moja. Ila wal ikubaliana wasipasue ile kanzu yake kwa maana ilikuwa imefumwa tangu juu hadi chini na haikukatwa mahali po pote. 24 Wakaam biana, “Tusiipasue ila tupige kura tuone ni nani aichukue.” Hii ilitimiza yale Maandiko yaliyosema, “Waligawana mavazi yangu, na kanzu yangu wakaipigia kura.” 25 Kwa hiyo wakapiga kura. Karibu na msalaba wa Yesu walikuwa wamesimama: Mariamu mama yake, shan gazi yake, Mariamu mke wa Klopa na Mariamu Magdalena. 26 Yesu alipomwona mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda wamesimama karibu, alimwambia mama yake, “Mama, huyo ni mwanao!” 27 Kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Na huyo ni mama yako.” Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Yesu nyumbani kwake.
Kifo Cha Yesu
28 Baada ya haya Yesu alifahamu ya kuwa mambo yote yameka milika, kwa hiyo, ili kutimiza Maandiko, akasema, “Naona kiu.” 29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachukua sponji iliyolowanishwa kwenye hiyo siki wakaichomeka kwenye ufito wa hisopo wakampandishia mdomoni. 30 Baada ya kuipokea hiyo siki, Yesu akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa, akakata roho.
31 Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi ya Pasaka Wayahudi hawakutaka miili yao ibaki msalabani siku ya sabato. Hii ingekuwa sabato ya pekee kwa kuwa iliangukia wakati wa Pasaka. Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe ili wafe upesi waondolewe msalabani. 32 Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa na Yesu na wa pili pia. 34 Ila askari mmoja akamchoma mkuki ubavuni, na mara pakatoka damu na maji. 35 Mambo haya yamehakikishwa na mtu aliyeyaona, na ushahidi wake ni wa kuaminika. Yeye anajua ya kuwa aliyosema ni kweli, naye ametoa ushuhuda huu ili nanyi mpate kuamini. 36 Kwa maana mambo haya yalitokea ili kutimiza Maandiko yaliyosema, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.” 37 Na pia Maandiko mengine yanasema, “Watamtazama yeye waliyemchoma kwa mkuki.” 38 Baada ya haya, Yusufu wa Arimathea aliyekuwa mfuasi wa siri wa Yesu, maana aliwaogopa Wayahudi, akamwomba Pilato auchukue mwili wa Yesu; naye akamruhusu. Kwa hiyo akaja, akauchukua mwili wa Yesu. 39 Naye Nikodemo, yule ambaye alimwen dea Yesu kwa siri usiku, alikuja na mchanganyiko wa manukato zaidi ya kilo thelathini. 40 Wakauchukua mwili wa Yesu, wakau vika sanda iliyokuwa na manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Way ahudi. 41 Karibu na pale walipomsulubisha palikuwa na bustani yenye kaburi ambalo lilikuwa halijatumika. 42 Kwa hiyo ili kuka milisha mazishi kabla ya sabato, wakamzika Yesu kwenye hilo kab uri lililokuwa karibu.
Njia Ya Kweli Ya Wokovu
3 Hatimaye ndugu zangu, furahini katika Bwana. Mimi sichoki kuwaandikieni mambo yale yale niliyokwisha waandikia kwa maana najua kwamba yatakuwa ni kinga kwenu. 2 Jihadharini na watenda maovu, hao mbwa, na wale wanaokaza mafundisho ya kutahiriwa. 3 Sisi tumepokea tohara ya kweli, kwa maana tunamwabudu Mungu katika Roho. Sisi tunaona fahari kwa ajili ya maisha yetu ndani ya Kristo Yesu. Hatuweki matumaini yetu katika mambo ya mwili, 4 ijapokuwa mimi mwenyewe ninazo sababu za kuweka matumaini katika mambo hayo. Kama mtu mwingine ye yote anadhani kuwa anazo sababu za kuweka matumaini yake katika mambo ya mwili, basi mimi ninazo sababu zaidi. 5 Nilitahiriwa siku ya nane, mimi ni Mwis raeli wa kabila la Benjamini; Mwebrania halisi. Kuhusu mambo ya kushika sheria, mimi nilikuwa Mfarisayo; 6 na kwa upande wa juhudi, mimi nilikuwa na bidii katika kutesa kanisa; na kuhusu haki ipatikanayo kwa kutii sheria, mimi nilikuwa sina hatia.
7 Lakini mambo hayo niliyoyaona mwanzo kuwa ni faida kwangu, sasa nayaona kuwa ni hasara kwa ajili ya Kristo. 8 Zaidi ya hayo, nahesabu mambo yote kuwa hasara tupu yakilinganishwa na faida kubwa ninayopata kwa kumjua Kristo Yesu aliye Bwana wangu. Kwa ajili yake nilikubali kupoteza kila kitu na kuona mambo hayo yote kuwa ni takataka ili nipate faida ya kuwa na Kristo; 9 na nikiwa kwake nisionekane kama mtu mwenye haki yake mwenyewe, inayotokana na kushika sheria, bali niwe na ile haki inayotokana na kumwamini Kristo, ambaye yeye ni haki itokayo kwa Mungu inayopatikana kwa imani. 10 Nataka nimjue Kristo na nguvu ya ufufuo wake na nishi riki mateso yake, niwe kama yeye katika kifo chake; 11 na hivyo, kama ikiwezekana, niufikie ufufuo kutoka kwa wafu.
12 Sisemi kwamba nimekwisha kupokea haya yote, au kwamba nimekwisha kuwa mkamilifu, la hasha; bali nazidi kukaza mwendo ili nipate kile ambacho, kwa ajili yake, Kristo amenifanya niwe wake. 13 Ndugu zangu, bado sijihesabu kuwa nimekwisha pata ile zawadi. Lakini jambo moja ninalofanya ni kusahau mambo yote yali yopita, na kukaza mwendo kufikia yaliyo mbele yangu. 14 Nakaza na nifikie ushindi, ili nipate zawadi ambayo Mungu ameniitia mbinguni, nikiwa ndani ya Kristo Yesu.
15 Sisi tuliokomaa kiroho tuwe na msimamo kama huu. Lakini kama kuna mawazo tofauti kuhusu jambo lo lote, Mungu atawafunu lia. 16 Ila tushike sana yale tuliyokwisha kupokea.
17 Ndugu zangu, nawasihi mfuate mfano wangu, na muwatazame wale wanaofuata mfano tuliowapa. 18 Kwa maana, kama nilivyok wisha waambia kabla, na sasa nasema tena kwa machozi, wako watu wengi miongoni mwenu ambao maisha yao yanaonyesha kuwa wao ni adui wa msalaba wa Kristo. 19 Mwisho wa watu hao ni kuangamia, na Mungu wao ni tumbo; kwa sababu wao huyaonea fahari mambo ya aibu na mawazo yao yametawaliwa na mambo ya dunia. 20 Lakini uraia wetu uko mbinguni. Nasi tunangoja kwa hamu Mwokozi kutoka huko, yaani Bwana wetu Yesu Kristo, 21 ambaye, kwa uwezo unaomwezesha kutawala kila kitu, atabadilisha miili yetu midhaifu ili iwe na utukufu kama alionao yeye.
Copyright © 1989 by Biblica