M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Anawaombea Wanafunzi Wake
17 Yesu alipomaliza kusema maneno haya, alitazama mbinguni akasema, “Baba, wakati umefika. Dhihirisha utukufu wangu ili nami nikutukuze wewe, 2 kwa kuwa umenipa mamlaka juu ya watu wote, niwape uzima wa milele wale ambao umewakabidhi kwangu. 3 Na huu ndio uzima wa milele: wakufahamu wewe ambaye pekee ni Mungu wa kweli, nakumfah amu Yesu Kristo ambaye umemtuma. 4 Baba nime kutukuza hapa duniani kwa kutimiza kazi uliyonipa niifanye. 5 Na sasa Baba nipe mbele yako ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe hata kabla dunia haijaumbwa. 6 Nimewafahamisha jina lako wale ambao umenipa kutoka katika ulimwengu. Wao wametii neno lako. 7 Sasa wamefahamu ya kuwa vyote ulivyonipa vinatoka kwako ; 8 kwa kuwa nimewapa ujumbe ulionipa, nao wameupokea. Wamefahamu hakika ya kuwa nimetoka kwako na wameamini kwamba ulinituma. 9 Siwaombei watu wote wa ulimwengu bali nawaombea hawa ulionipa kwa sababu wao ni wako. 10 Wote ulionipa ni wako, na walio wako ni wangu; nao wanadhihirisha utukufu wangu. 11 Mimi naondoka ulimwenguni ninakuja kwako. Lakini wao wako ulimwenguni. Baba Mtakatifu, walinde kwa jina lako ambalo umenipa ili wawe na umoja kama sisi tulivyo mmoja. 12 Nilipokuwa pamoja nao niliwalinda wakawa salama kwa uwezo wa jina ulilonipa. Nimewalinda na hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyeamua kupotea, ili Maandiko yapate kutimia. 13 Lakini sasa nakuja kwako na ninasema haya wakati nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kikamil ifu. 14 Nimewapa neno lako na ulimwengu umewachukia kwa kuwa wao, kama mimi, si wa ulimwengu huu. 15 Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde na yule mwovu shetani. 16 Kama mimi nisivyo mwenyeji wa ulimwengu huu, wao pia sio wa ulimwengu. 17 Watakase kwa neno lako; kwa maana neno lako ndilo kweli. 18 Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma wao ulim wenguni. 19 Kwa ajili yao nimejitoa wakfu kwako ili na wao wapate kuwa watakatifu kwa kufahamu kweli yako.
Yesu Anawaombea Watakaoamini Baadaye
20 “Siwaombei hawa peke yao; bali nawaombea pia wale wote watakaoniamini kwa sababu ya ushuhuda wa hawa. 21 Ninawaombea wote wawe kitu kimoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi ni ndani yako; ili na wao wawe ndani yetu na ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ulinituma. 22 Nimewapa utukufu ule ule ulionipa ili wawe kitu kimoja kama sisi tulivyo - 23 mimi nikiwa ndani yao na wewe ndani yangu; ili wakamilike katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma na kwamba unawapenda kama unavyonipenda mimi. 24 Baba, shauku yangu ni kwamba, hawa watu ulionipa wawepo mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu; utukufu ambao umenipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ulimwengu haujaumbwa. 25 Baba Mtakatifu, ijapokuwa ulimwengu haukufahamu wewe, mimi ninakufahamu, na hawa wanajua ya kuwa umenituma. 26 Nimekutambulisha wewe kwao, na nitaendelea kulitambulisha jina lako kwao ili upendo ulio nao kwangu uwe upendo wao pia; nami niwe ndani yao.”
1 Kutoka kwa Paulo na Timotheo, watumwa wa Yesu Kristo. Kwa watakatifu walioko Filipi pamoja na maaskofu na wasaidizi wote wa kanisa. 2 Tunawatakieni neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Shukrani Na Maombi.
3 Ninamshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbuka 4 katika sala zangu zote, nikiomba kwa furaha 5 na shukrani kwa ajili ya ushi rikiano uliopo kati yetu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. 6 Nina hakika kwamba, yeye aliyeianza kazi yake njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha siku ile ataka porudi Yesu Kristo.
7 Ninajisikia hivi kwa sababu nawathamini sana moyoni mwangu. Kwa maana tumeshiriki pamoja neema ya Mungu wakati nikiwa kifun goni na wakati nikiitetea na kuithibitisha Injili. 8 Mungu ni shahidi wangu kwamba natamani mno kuwa pamoja nanyi na kwamba upendo nilio nao kwenu ni upendo wa Kristo Yesu. 9 Na sala yangu kwa ajili yenu ni kwamba upendo wenu uzidi kuongezeka siku hadi siku pamoja na maarifa na busara 10 ili mpate kutambua mambo yaliyo mema. Na pia mpate kuwa watu safi, wasio na hatia hadi siku ya Kristo. 11 Maisha yenu yawe na matunda ya haki yatokayo kwa Yesu Kristo, ili Mungu apewe utukufu na sifa. 12 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba haya mambo yaliyonipata yamesaidia sana kueneza Injili ya Kristo. 13 Watu wote hapa pamoja na maaskari wa ikulu wanajua wazi kuwa mimi niko kifungoni kwa sababu ya kumtumikia Kristo. 14 Kwa sababu ya kifungo changu, ndugu wengi katika Bwana wametiwa moyo kuhubiri neno la Mungu pasipo hofu. 15 Ni kweli kwamba wapo ndugu wengine wanaom hubiri Kristo kutokana na wivu na kwa kutaka kushindana; lakini wengine wanamhubiri Kristo kwa nia njema. 16 Hawa wanahubiri kwa moyo wa upendo, wakifahamu kwamba Mungu ameniweka hapa kifungoni ili niitetee Injili. 17 Hao wengine wanamtangaza Kristo kwa tamaa ya kupata sifa wala si kwa moyo wa upendo, wakifikiri kwamba kwa kufanya hivyo wataniongezea mateso yangu kifungoni. 18 Lakini kwangu mimi hiyo si kitu. Lililo la muhimu ni kwamba kwa kila njia Kristo anahubiriwa, ikiwa kwa nia mbaya au kwa nia njema. Kwa sababu hiyo, mimi nashangilia. Pia nitaendelea kushan gilia, 19 kwa sababu najua kwamba kwa ajili ya sala zenu na kwa msaada wa Roho wa Yesu Kristo, jambo lililonipata litageuka kuwa njia ya kufunguliwa kwangu. 20 Shauku yangu na tumaini langu ni kwamba sitaaibika kwa njia yo yote, bali nitakuwa na ujasiri, ili kama ilivyo sasa, Kristo aendelee kutukuzwa kutokana na maisha yangu, kama ni kuishi au hata kama ni kufa. 21 Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida. 22 Kama nitaendelea kuishi katika mwili, hii itaniwezesha kufanya kazi yenye matunda. Lakini sijui nichague lipi! 23 Yote mawili yananivutia: nata mani niyaache maisha haya ili nikakae pamoja na Kristo, jambo ambalo naona ni bora zaidi. 24 Lakini kwa sababu yenu naona kuwa ni muhimu zaidi nikiendelea kuishi. 25 Nina hakika kwamba, kwa sababu hii nitabaki na kuendelea kuishi pamoja nanyi nyote, ili mpate kukua na kuwa na furaha katika imani. 26 Na hivyo, kwa ajili yangu, muwe na sababu ya kuona fahari ndani ya Kristo Yesu kwa kuja kwangu kwenu.
Mapambano Kwa Ajili Ya Imani
27 Lakini hata ikitokea nini, hakikisheni kuwa mwenendo wenu unalingana na Injili ya Kristo. Ili kama nikija kuwaona au hata nisipojaliwa kufika, nipate habari kuwa mnasimama imara katika roho ya umoja, mkiwa na nia moja huku mkipambana kwa pamoja kwa ajili ya imani ya Injili, 28 bila kuwaogopa wale wanaowapinga. Hii ni ishara dhahiri ya kuangamia kwao, lakini kwenu ninyi, hii ni ishara ya wokovu wenu kutoka kwa Mungu. 29 Kwa maana mmepewa heshima kwa ajili ya Kristo, sio tu kumwamini, bali pia kuteswa kwa ajili yake. 30 Sasa mnashiriki mapambano yale yale mliyoona nikiwa nayo na ambayo mnasikia kwamba bado naendelea nayo.
Copyright © 1989 by Biblica