M’Cheyne Bible Reading Plan
16 “Nimewaambia mambo haya yote ili msije mkapoteza imani yenu. 2 Watawatenga na kuwatoa katika ushirika wa masinagogi. Na si hivyo tu, bali utafika wakati ambapo mtu ye yote atakayewaua atadhani kuwa anamtumikia Mungu. 3 Watu watawatendea haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala hawanifahamu mimi. 4 Lakini nimew aambia mambo haya kusudi muda huo utakapofika mkumbuke kuwa nili kuwa nimewaambia. Sikuwaambia mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.
Kazi Ya Roho Mtakatifu
5 “Lakini sasa ninakwenda kwake yeye aliyenituma, wala hakuna mmoja wenu anayeniuliza, ‘Unakwenda wapi?’ 6 Kwa kuwa nimewaambia mambo haya, mioyo yenu imejawa na huzuni. 7 Lakini nawaambia kweli kwamba kuondoka kwangu ni kwa faida yenu kwa maana nisipoondoka, yule Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda nitamtuma aje kwenu. 8 Naye akija atauthibitishia ulim wengu kuhusu dhambi, haki na hukumu. 9 Kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini; 10 kuhusu haki kwa sababu ninakwenda kwa Baba na hamtaniona tena; 11 na kuhusu hukumu kwa sababu mtawala wa ulim wengu huu amekwisha kuhukumiwa.
12 “Nina mambo mengi zaidi ya kuwaambia lakini hamwezi kuy apokea sasa. 13 Akija yule Roho wa kweli atawaongoza muijue kweli yote. Yeye hatanena kwa uwezo wake mwenyewe bali atanena yote atakayosikia. Atawafundisha kuhusu mambo yote yajayo. 14 Atanitukuza mimi, kwa maana atayachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi. 15 Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu, ndio maana nimesema kuwa atachukua yaliyo yangu na kuwaambia ninyi.
Huzuni Na Furaha
16 “Baada ya muda mfupi hamtaniona tena; na kisha muda mfupi baadaye mtaniona.” 17 Baadhi ya wanafunzi wakaulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘Baada ya muda mfupi hamtaniona tena na muda mfupi baadaye mtaniona’? Na ana maana gani asemapo, ‘Kwa sababu ninakwenda kwa baba’?” 18 Wakaendelea kuulizana, “Ana maana gani asemapo, ‘muda mfupi?’ Hatuelewi ana maana gani!”
19 Yesu alitambua walilotaka kumwuliza kwa hiyo akawaambia, “Mnaulizana nina maana gani nisemapo, ‘Baada ya muda mfupi ham taniona tena na baada ya muda mfupi mtaniona?’ 20 Ninawaambia yaliyo hakika kwamba mtalia na kuomboleza lakini ulimwengu utafu rahi. Mtahuzunika lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Mwanamke akaribiapo kuzaa huwa na huzuni kwa sababu saa yake ya uchungu imefika. Lakini mtoto azaliwapo mama anasahau mateso hayo kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtoto duniani. 22 Na ninyi sasa mna huzuni lakini nitawaona tena na mtafurahi, wala hakuna atakayewaondolea furaha yenu. 23 Wakati huo hamtaniomba kitu cho chote. Ninawaambia kweli kwamba Baba yangu atawapa lo lote mta kaloomba kwa jina langu. 24 Mpaka sasa hamjaomba lo lote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapewa ili furaha yenu ipate kukamil ika.
Ushindi
25 “Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Lakini wakati unakuja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nita waeleza wazi wazi kuhusu Baba yangu. 26 Wakati huo mtaomba kwa jina langu. Wala sisemi kwamba nitamwomba Baba kwa niaba yenu; 27 kwa maana Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na mmeamini kwamba nimetoka kwa Baba. 28 Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni, tena sasa naondoka ulimwenguni na ninak wenda kwa Baba.” 29 Wanafunzi wake wakasema, “Sasa unazungumza wazi wazi wala si kwa mafumbo. 30 Sasa tumejua kwamba wewe una jua mambo yote wala hakuna haja ya mtu kukuuliza maswali. Kwa hiyo tunaamini kwamba ulitoka kwa Mungu.” 31 Yesu akawajibu, “Sasa mnaamini? 32 Saa inakuja, tena imeshawadia, ambapo mtata wanyika, kila mtu aende nyumbani kwake na kuniacha peke yangu; lakini mimi siko peke yangu kwa sababu Baba yuko pamoja nami. 33 Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”
6 Watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana kufanya hivyo ni vizuri. 2 “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 3 “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.” 4 Akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana. Watumwa Na Mabwana
5 Watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani, kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnamtii Kristo. 6 Watiini, sio tu wakati wakiwaona ili mpate sifa, bali mtumike kama watumishi wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. 7 Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na sio watu. 8 Mkumbuke kuwa Bwana atampa kila mmoja tuzo kutegemeana na wema aliotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru. 9 Nanyi mabwana watendeeni watumwa wenu kwa jinsi hiyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.
10 Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu. 11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama na kupin gana na hila zote za shetani. 12 Kwa maana hatupambani na bina damu, bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama imara siku ya uovu itakapokuja; na mkishafanya yote, mtakuwa bado mme simama. 14 Kwa hiyo simameni imara mkisha jifunga na kweli kama mkanda kiunoni na haki kama kinga ya kifuani; 15 na kuvaa Injili ya amani kama viatu miguuni, ili muweze kusimama barabara. 16 Zaidi ya haya yote, jivikeni imani kama ngao ambayo itawawe zesha kuzuia mishale yenye miale ya moto kutoka kwa yule mwovu. 17 Vaeni wokovu kama kofia ya vita vichwani na chukueni upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu. 18 Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea watu wote wa Mungu. 19 Niombeeni mimi pia, ili kila ninapozungumza, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili pasipo woga. 20 Mimi ni balozi kifun goni kwa ajili ya Injili hii. Kwa hiyo niombeeni niihubiri Injili kwa ujasiri kama inipasavyo. 21 Ndugu mpendwa Tikiko, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawaelezeni kila kitu ili mjue habari zangu na mfahamu ninachofanya. 22 Ninamtuma kwenu kwa kusudi hili, mpate habari zetu naye awafariji. 23 Nawatakia ndugu wote amani na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo.
Copyright © 1989 by Biblica