Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Exod for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 15

Mzabibu Wa Kweli

15 ‘Mimi ni mzabibu wa kweli na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda, Baba yangu hulikata; na kila tawi lizaalo, yeye hulisafisha ili lipate kuzaa matunda zaidi. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya mafundisho nili yowapa. Kaeni ndani yangu nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda pasipo kuwa sehemu ya mzabibu, vivyo hivyo, ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kufanya lo lote. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; anayekaa ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa matunda mengi sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi na kunyauka. Matawi hayo hukusanywa na kutupwa motoni, yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lo lote mtakalo nanyi mtatendewa. Mnapozaa matunda kwa wingi Baba yangu anatukuzwa, na hivyo mnadhihirisha kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.

“Kama Baba alivyonipenda mimi, hivyo ndivyo mimi nilivy owapenda ninyi; dumuni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu mtakaa ndani ya pendo langu kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.

11 “Nimewaambia haya kusudi furaha yangu iwe ndani yenu, nanyi mpate kuwa na furaha iliyokamilika.

12 “Amri yangu ni hii: pendaneni kama nilivyowapenda. 13 Hakuna mtu mwenye upendo unaozidi ule wa mtu anayejitoa afe kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafa nya ninayowaagiza. 15 Siwaiti ninyi watumishi tena kwa sababu mtumishi haelewi shughuli za bwana wake; bali nimewaita rafiki, kwa maana mambo yote niliyoyasikia kutoka kwa Baba yangu nimewa fahamisha. 16 Hamkunichagua, bali mimi nimewachagua ninyi na nimewatuma mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu, ili lo lote mtakalomwomba Baba katika jina langu, awatimizie. 17 Hii ndio amri yangu: pendaneni.

18 “Kama ulimwengu ukiwachukia, fahamuni kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa watu wa ulim wengu huu, ulimwengu ungeliwapenda. Ulimwengu unawachukia kwa sababu ninyi si wa ulimwengu huu na mimi nimewachagua kutoka katika ulimwengu.

20 “Kumbukeni lile neno nililowaambia, ‘Hakuna mtumishi aliye mkuu kuliko bwana wake.’ Kama wamenitesa mimi na ninyi pia watawatesa; kama wamelishika neno langu na neno lenu watalishika pia. 21 Lakini yote haya watawatendea kwa ajili yangu kwa sababu hawamfahamu Baba yangu ambaye amenituma. 22 Kama sikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia. Lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi zao. 23 Mtu ye yote anayenichukia mimi anamchukia na Baba yangu. 24 Kama nilikuwa sikuwafanyia miujiza ambayo haijapata kufanywa na mtu mwingine ye yote, wasingalikuwa na hatia ya dhambi. Lakini wameona miujiza hii na bado wakatuchukia mimi na Baba yangu. 25 “Hali hii imetokea kama ilivyoandikwa katika Sheria kwamba, ‘Walinichukia pasipo sababu.’ 26 Lakini atakapokuja yule Msaidizi nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, yaani yule Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. 27 Na ninyi pia ni mashahidi wangu kwa maana tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.”

Error: Book name not found: Prov for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Waefeso 5

Kwa hiyo mfuateni Mungu kama watoto wapendwa. Muishi maisha ya upendo kama Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu. Lakini uasherati, uchafu wa aina zote na tamaa, wala yasitajwe miongoni mwenu, kwa maana mambo haya hayawastahili watakatifu wa Mungu. Kusiwepo na mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuuzi au mzaha; mazungumzo ya namna hii hayafai. Badala yake mshukuruni Mungu. Mjue hakika kwamba hakuna mwasherati wala mtu mwenye mawazo machafu, wala mwenye tamaa, yaani mwabudu sanamu, ambaye ataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu. Msikubali kudan ganywa na mtu ye yote kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya watu wote wasiomtii. Kwa hiyo, msishirikiane nao. Zamani ninyi pia mlikuwa gizani, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana; basi muishi kama watoto wa nuru. Kwa maana tunda la nuru hupatikana katika kila lililo jema, lililo la haki na la kweli. 10 Jifunzeni mambo yanayom pendeza Bwana. 11 Msishiriki matendo ya giza yasiyofa a, bali yafichueni. 12 Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo wanayofanya kwa siri. 13 Lakini ikiwa jambo lo lote linawekwa katika nuru, huonekana, kwa maana ni nuru inayofanya vitu vionekane. 14 Ndio sababu husemwa, “Amka wewe uliyelala, ufufuke kutoka kwa wafu, na Kristo atakuangazia.” 15 Kwa hiyo muwe waangalifu jinsi mnavyoishi; msiishi kama watu wasio na hekima, bali kama watu wenye hekima, 16 mkitumia vizuri muda mlio nao, kwa maana hizi ni nyakati za uovu. 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali muelewe yaliyo mapenzi ya Mungu. 18 Pia msilewe divai, kwa sababu huo ni upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Zungumzeni ninyi kwa ninyi kwa zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia Mungu mioyoni mwenu kwa sauti tamu. 20 Wakati wote na kwa kila kitu mshukuruni Mungu Baba katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 21 Kila mmoja wenu ajinyenyekeze kwa mwenzake kwa sababu ya upendo mlio nao kwa Kristo. 22 Wake, watiini waume zenu kama mnavyomtii Bwana. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo ni mwili wake, naye mwe nyewe ni Mwokozi wa kanisa. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyom tii Kristo, vivyo hivyo na wake pia wanapaswa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili 26 alitakase. Alifanya hivyo kwa kuliosha kwa maji na kwa neno lake 27 ili ajipatie kanisa linalong’aa, lisilo na doa wala kunjamano wala kitu kingine cho chote kama hicho; liwe takatifu na bila kasoro. 28 Vivyo hivyo waume wawapende wake zao kama miili yao. Anayempenda mkewe anajipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza kanisa lake. 30 Sisi tu viungo vya mwili wake. 31 “Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataungana na mkewe, na hawa wawili wata kuwa mwili mmoja.” 32 Hili ni fumbo gumu kueleweka, nami nasema kuwa ni kielelezo kuhusu Kristo na kanisa. 33 Hata hivyo kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake; na mke naye ahakikishe anamheshimu mumewe. Watoto Na Wazazi

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica