M’Cheyne Bible Reading Plan
Mwanamke Aliyefumaniwa Akizini
8 Lakini Yesu akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni. 2 Alfajiri Yesu akaja tena Hekaluni, watu wengi wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha. 3 Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya watu wote. 4 Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. 5 Katika sheria, Musa ametuamuru kuwapiga mawe wanawake waliokamatwa wakizini, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?” 6 Walim wuliza hivi kwa kumtega, kusudi wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini akaanza kuandika kwa kidole chake mavumbini. 7 Walipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, “Asiyekuwa na dhambi kati yenu awe wa kwanza kumtupia jiwe.” 8 Akainama tena akaendelea kuandika chini. 9 Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, akianza mkubwa wao. Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama pale walipomwacha. 10 Yesu akasimama akamwuliza, “Mama, wale waliokuwa wanakush taki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?” 11 Yule mwa namke akajibu, “Hakuna Bwana.” Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Unaweza kwenda, lakini usitende dhambi tena.”]
Yesu Ni Nuru Ya Ulimwengu
12 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru yenye kuleta uzima.” 13 Mafarisayo wakam wambia, “Ushuhuda wako haukubaliki kwa sababu unajishuhudia mwe nyewe.” 14 Yesu akawajibu, “Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni wa kweli kwa sababu najua nilikotoka na nina kokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakokwenda. 15 Ninyi mnatoa hukumu kwa kufuata vipimo vya kibinadamu. Mimi simhukumu mtu ye yote. 16 Lakini hata kama nikitoa hukumu, ita kuwa sahihi kabisa kwa sababu sitoi hukumu peke yangu; Baba ali yenituma yupo pamoja nami. 17 Imeandikwa katika Sheria zenu kwamba ushahidi wa watu wawili unatosha kuthibitisha ukweli. 18 Mimi najishuhudia mwenyewe; shahidi wangu mwingine ni Baba ambaye amenituma.” 19 Wakamwuliza, “Huyo baba yako yuko wapi?” Yesu akawajibu, “Ninyi hamfahamu mimi ni nani, wala ham fahamu Baba yangu ni nani. Kama mngefaham u mimi ni nani, mngem fahamu na Baba yangu.” 20 Yesu alisema haya alipokuwa akifund isha Hekaluni katika chumba ambamo vyombo vya sadaka viliwekwa. Wala hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa wakati wake ulikuwa hauja timia.
Yesu Asema, ‘Niendako Hamwezi Kufika’
21 Tena Yesu akawaambia, “Nitaondoka, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Mahali ninapokwenda ninyi hamwezi kufika.” 22 Wale Wayahudi wakaulizana, “Mbona anasema, ‘Mahali ninapokwenda hamwezi kufika’? Je, anataka kujiua?” 23 Akawaambia, ‘Tofauti kati yenu na Mimi ni kwamba ninyi ni wa hapa duniani, mimi natoka mbinguni. Ninyi ni wa ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu. 24 Kwa hiyo nimewaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu. Kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye 25 Wakamwuliza, “Kwani wewe ni nani?” Yesu akawajibu, “Nimekuwa nikiwaambia mimi ni nani tangu mwanzo. 26 Kuna mambo mengi ambayo ningeweza kusema juu yenu na kuna mambo mengi ambayo ningeweza kuwahukumu. Lakini yeye ali yenituma ni wa kweli, na yale niliyosikia kutoka kwake nawaambia wa ulimwengu.” 27 Hawakuelewa kuwa alikuwa anasema juu ya Baba yake wa Mbinguni. 28 Kwa hiyo Yesu akawaambia, “Mtakaponiinua juu, mimi Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa, ‘Mimi Ndiye
29 Baba yangu ambaye amenituma yupo pamoja nami, hajaniacha; kwa kuwa siku zote nafanya mapenzi yake.” 30 Wengi waliomsikia Yesu akisema maneno haya walimwamini.
Watu Huru Na Watumwa
31 Kwa hiyo Yesu akawaambia wale waliomwamini, “Kama mkiendelea kutii maneno yangu mtakuwa wanafunzi wangu halisi. 32 Mtaelewa yaliyo kweli kumhusu Mungu na ukweli huu utawafanya muwe watu huru. 33 Wao wakamjibu, “Una maana gani kusema tuta kuwa huru? Sisi ni wa uzao wa Ibrahimu. Hatujawahi kuwa watumwa wa mtu ye yote.” 34 Yesu akawaambia, “Ukweli ni kwamba, mtu ye yote anayetenda dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35 Mtumwa hana haki ya kuishi siku zote katika nyumba anapotumika, lakini mwana ana haki zote katika nyumba ya baba yake. 36 Kwa hiyo, kama Mwana akiwafanya muwe huru, mtakuwa huru kweli. 37 Ninajua ya kuwa ninyi ni wa uzao wa Ibrahimu; lakini mnatafuta njia ya kuniua kwa sababu hamkubaliani na mafundisho yangu. 38 Ninasema yale niliy oyaona kwa Baba yangu na ninyi mnafanya yale mliyosikia kutoka kwa baba yenu.” 39 Wakasema, “Baba yetu ni Ibrahimu.” Yesu akawajibu, “Kama mngekuwa wa uzao wa Ibrahimu mngekuwa na tabia kama yake. 40 Lakini mnataka kuniua kwa sababu nimewaambia maneno ya kweli niliyosikia kutoka kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya jambo la namna hii! 41 Ninyi mnafanya kama baba yenu afanyavyo. Wakamjibu, “Sisi si watoto wa haramu; tunaye Baba mmoja ambaye ni Mungu.” 42 Ndipo Yesu akawaambia, “Kama Mungu angekuwa ni Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa nipo hapa. Sikuja kwa mapenzi yangu mwenyewe ila kwa kuwa Mungu alini tuma. 43 Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu mnaka taa kusikiliza ujumbe wangu. 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu shetani; kwa hiyo mnapenda kufanya maovu kama yeye. Tangu mwanzo yeye alikuwa muuaji na hana uhusiano wo wote na mambo ya kweli; kwa maana hana asili ya kusema lililo kweli. Shetani anapodanga nya anadhihirisha asili yake kwa kuwa yeye ni mwongo na ni baba wa uongo. 45 Lakini mimi nawaambia yaliyo kweli ndio sababu ham uamini maneno yangu! 46 Ni nani kati yenu anayeweza kuonyesha kuwa mimi nina dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona basi hamnisadiki? 47 Mtu wa Mungu hupokea maneno ya Mungu. Ninyi ham pokei maneno ya Mungu kwa sababu ninyi si wa Mungu.”
Yesu Amekuwepo Kabla Ya Ibrahimu
48 Wakamjibu, “Tulitamka sawa tuliposema kuwa wewe ni Msa maria na tena umepagawa na pepo.” 49 Yesu akawajibu, “Sina pepo. Mimi namheshimu Baba yangu bali ninyi mnanivunjia heshima yangu. 50 Hata hivyo mimi sitafuti utukufu wangu binafsi; yuko anayetaka niheshimiwe na ndiye atakayekuwa mwamuzi. 51 Ninawaam bia wazi kwamba, mtu ye yote anayetii mafundisho yangu hatakufa kamwe.” 52 Wakasema, “Sasa umetuhakikishia kabisa kwamba una wazimu! Ikiwa Ibrahimu alikufa na Manabii nao walikufa, utase maje, ‘mtu akitii mafundisho yangu hatakufa?’ 53 Je, wewe ni mkuu zaidi ya baba yetu Ibrahimu ambaye alikufa? Na Manabii ambao nao walikufa? Hivi unajifanya wewe kuwa nani?” 54 Yesu akawa jibu, “Kama nikijisifu mwenyewe sifa hiyo itakuwa haina maana. Anayenipa heshima ni Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnamwita Mungu wenu. 55 Lakini ninyi hamumfahamu. Mimi namfahamu. Nikisema sim fahamu nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namfahamu na ninatii maneno yake. 56 Baba yenu Ibrahimu alishangilia alipojua kuwa atashuhudia siku ya kuja kwangu. Aliiona siku hiyo na akafurahi sana.” 57 Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, itawezekanaje uwe umemwona Ibrahimu?” 58 Yesu akawa jibu, “Nawaambia wazi, kabla Ibrahimu hajazaliwa, ‘Mimi nipo.’ ” 59 Ndipo wakainua mawe wamwue; lakini Yesu akajificha wasim wone; akatoka Hekaluni.
Wana Wa Mungu
4 Nataka muelewe kwamba mrithi akiwa bado ni mtoto mdogo hana tofauti na mtumwa, ingawa mali yote ni yake. 2 Kwa sababu anakuwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. 3 Hali kadhalika na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa tunatawaliwa na kanuni za mazingira. 4 Lakini wakati ulipotimia, Mungu alimtuma Mwana we, ambaye alizaliwa na mwanamke chini ya sheria, 5 ili kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, tupate kibali cha kuwa wana wa Mungu. 6 Na kwa kuwa ninyi sasa ni wana wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanae akae ndani ya mioyo yenu, akiita, “Abba! Baba.” 7 Kwa hiyo, wewe sio mtumwa tena, bali ni mwana wa Mungu, na ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, basi wewe pia ni mrithi.
Paulo Alivyowajali Wagalatia
8 Zamani, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa mkitumikia ‘miu ngu’ ambayo kwa asili si miungu. 9 Lakini sasa kwa kuwa mmemfa hamu Mungu, au tuseme, sasa Mungu anawafahamu ninyi, mnawezaje kurudia tena upungufu na umaskini wa nguvu za pepo muwe watumwa wake? 10 Bado mnaadhimisha siku maalumu, miezi, nyakati na miaka! 11 Nina hofu juu yenu; inaelekea kazi niliyofanya kwa ajili yenu imepotea bure.
12 Ndugu zangu, nawasihi muwe kama mimi, kwa sababu na mimi nimekuwa kama ninyi. Hamkunitendea ubaya wo wote. 13 Ninyi mnafahamu kwamba ugonjwa wangu ndio ulionipatia nafasi ya kuwa hubiria Habari Njema kwa mara ya kwanza. 14 Lakini ninyi hamku nidharau wala kunikataa ingawa udhaifu wa mwili wangu ulikuwa mzigo kwenu. Bali mlinipokea vizuri kama malaika wa Mungu, na kama Kristo Yesu. 15 Ile furaha mliyokuwa nayo iko wapi sasa? Naweza kushuhudia kwamba wakati ule mlikuwa tayari hata kung’oa macho yenu mnipe. 16 Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa sababu nawaambieni ukweli?
17 Hao watu wanaoshughulika ili muwe upande wao nia yao si nzuri. Wanataka kuwatenganisha na sisi ili muwajali wao zaidi. 18 Ni vema watu wanapowahangaikia kwa bidii kama shabaha ya kufanya hivyo ni nzuri, na kama wanafanya hivyo wakati wote, isiwe tu wakati nikiwa nanyi. 19 Watoto wangu wadogo, najisikia kwa mara nyingine kama mama mwenye uchungu wa kuzaa, nikitamani kwamba Kristo aumbike ndani yenu. 20 Natamani ningekuwa pamoja nanyi sasa, pengine ningebadilisha msemo wangu. Kwa maana nata tanishwa na hali yenu.
21 Niambieni, ninyi mnaotaka kutawaliwa na sheria, je, hamu elewi sheria inavyosema? 22 Kwa maana imeandikwa katika Maandi ko kwamba Abrahamu alikuwa na watoto wawili: mtoto mmoja alizal iwa na mwanamke mtumwa, na wa pili alizaliwa na mwanamke huru. 23 Lakini, mtoto wa mwanamke mtumwa alizaliwa kwa mapenzi ya mwili na yule wa mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu. 24 Mambo haya yanaweza kueleweka kama mfano. Kwa maana hao mama wawili ni mfano wa maagano mawili: agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika mlima wa Sinai, wakazaliwa watoto wa utumwa; huyo ni Hajiri. 25 Hajiri sasa anawakilisha mlima Sinai ulioko Arabuni, na ni mfano wa Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. 26 Lakini Yerusalemu ya mbinguni ni huru, nayo ndio mama yetu. 27 Kwa maana imeandikwa: “Furahi wewe uliyetasa usiyeweza kuzaa; piga kelele, ulie kwa furaha wewe usiyepatwa na maumivu ya uzazi; kwa maana watoto wa yule ali yeachwa ni wengi kuliko watoto wa yule aliye na mume.”
28 Sasa ndugu zangu, sisi kama Isaki, tu watoto wa ahadi. 29 Lakini, kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivy omtesa yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa. 30 Lakini Maandiko yanasemaje? “Mfukuze mwanamke mtumwa pamoja na mwanae; kwa sababu mtoto wa mtumwa hawezi kurithi pamoja na mtoto wa mwanamke huru.” 31 Kwa hiyo ndugu zangu, sisi si watoto wa mtumwa bali wa mwanamke huru. Uhuru Ndani Ya Kristo
Copyright © 1989 by Biblica