M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Na Mwanamke Msamaria
4 Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kuba tiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana. 2 Lakini kwa hakika Yesu hakubatiza, wanafunzi wake ndio waliokuwa wakibatiza watu. 3 Bwana alipopata habari hizi aliondoka Yudea akarudi Galilaya. 4 Katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.
5 Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu. 6 Kisima cha Yakobo kilikuwa hapo na kwa kuwa Yesu alikuwa amechoka kutokana na safari, aliketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
7 Mama mmoja Msamaria akaja kuteka maji na Yesu akamwambia, “Naomba maji ya kunywa.” 8 Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula. 9 Yule mama akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” -Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria. 10 Yesu akamjibu, “Kama ungelifahamu Mungu anataka kukupa nini, na mimi ninayekuomba maji ya kunywa ni nani, ungeliniomba nikupe maji ya uzima.”
11 Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kuchotea maji na kisima hiki ni kirefu . Hayo maji ya uzima utay apata wapi? 12 Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”
13 Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. 14 Lakini ye yote atakayekunywa maji nitakay ompa mimi, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa kama chemchemi itakayobubujika maji yenye uhai na kumpa uzima wa milele.”
15 Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuchota maji!”
16 Yesu akamjibu, “Nenda kamwite mumeo, kisha uje naye hapa.” 17 Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Yesu akamwam bia, “Umesema kweli kuwa huna mume. 18 Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanamume unayeishi naye sasa si mume wako!”
19 Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. 20 Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu lakini ninyi Way ahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”
21 Yesu akamjibu, “Mama, niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. 22 Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwab udu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. 23 Lakini wakati unakuja, tena umekwisha timia, ambapo wale wanaoabudu inavyostahili watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu kwa njia hii ndio anaowataka Baba. 24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” 25 Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masihi, aitwaye Kristo, anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”
26 Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye Masihi.”
Masihi.”
27 Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kum wona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemwuliza, “Unataka nini kwake?” au “Kwa nini unazungumza naye?”
28 Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaam bia watu, 29 “Njooni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote nili yowahi kufanya! Je, yawezekana huyu ndiye Masihi?”
30 Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.
31 Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau cho chote.”
32 Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”
33 Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?” 34 Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma, na kuikamilisha kazi yake. 35 Si mnao msemo kwamba, ‘Bado miezi minne tutavuna’? Hebu yaangalieni mashamba, jinsi mazao yalivyoiva tayari kuvunwa! 36 Mvunaji hupokea ujira wake, naye hukusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele. Kwa hiyo aliyepanda mbegu na anayevuna, wata furahi pamoja. 37 Ule msemo wa zamani kwamba , ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. 38 Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi hiyo; ninyi mmefaidika kutokana na jasho lao!”
39 Wasamaria wengi walimwamini kutokana na ushuhuda wa yule mama alipowaambia kwamba, “Ameniambia mambo yote niliyowahi kutenda.” 40 Kwa hiyo wale Wasamaria walipokuja, walimsihi akae kwao, naye akakaa kwa siku mbili. 41 Watu wengi zaidi wakamwa mini kutokana na ujumbe wake. 42 Wakamwambia yule mama, sasa hatuamini tu kwa sababu ya yale uliyotuambia bali kwa kuwa tumem sikia sisi wenyewe, na tunajua hakika kwamba yeye ni Mwokozi wa ulimwengu.”
Yesu Amponya Mtoto Wa Afisa
43 Zile siku mbili zilipokwisha, Yesu aliondoka kwenda Gali laya. 44 Yesu mwenyewe alikwisha sema kwamba nabii haheshimiki nchini kwake. 45 Lakini alipofika, Wagalilaya walimpokea vizuri baada ya kuona mambo aliyofanya huko Yerusalemu wakati wa siku kuu, maana na wao walihudhuria.
46 Alikwenda tena mjini Kana katika Galilaya, kule alipo geuza maji kuwa divai. Na huko Kapernaumu alikuwapo afisa mmoja ambaye mtoto wake alikuwa mgonjwa. 47 Huyo afisa alipopata habari kuwa Yesu alikuwa amefika Galilaya kutoka Yudea, alikwenda akamwomba aje kumponya mwanae ambaye alikuwa mgonjwa karibu ya kufa.
48 Yesu akamwambia, “Ninyi watu hamwezi kuamini pasipo kuona ishara na miujiza?”
49 Yule afisa akajibu, “Bwana, tafadhali njoo kabla mwa nangu hajafa.” 50 Yesu akamwambia, “Nenda nyumbani, mwanao ataishi.” Yule afisa akaamini maneno ya Yesu, akaondoka kurudi nyumbani. 51 Alipokuwa bado yuko njiani, alikutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanae alikuwa mzima. 52 Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.” 53 Yule baba akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao ataishi.” Kwa hiyo yeye, pamoja na jamaa yake yote wakamwamini Yesu.
54 Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Yudea.
Maonyo Ya Mwisho Na Salamu
13 Hii itakuwa ni safari yangu ya tatu kuja kwenu. “Shitaka lo lote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.” 2 Niliwaonya wale waliotenda dhambi na wengine wote, na sasa nawaonya tena nikiwa siko nanyi kama nilivyowaonya wakati nili powatembelea mara ya pili, kwamba nikija tena sitawahurumia. 3 Kwa kuwa mnataka kupata ushahidi kuwa Kristo anazungumza kupi tia kwangu, hiyo itakuwa ushahidi wangu. Yeye si mdhaifu anapow ashughulikia bali ni mwenye nguvu ndani yenu. 4 Kwa maana alisu lubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Hali kadhalika sisi ni wadhaifu ndani yake, lakini kwa nguvu za Mungu tutaishi pamoja naye ili tuweze kuwahudumia.
5 Jichunguzeni mwone kama mnashika imani yenu. Jipimeni. Je, hamtambui ya kuwa Kristo yuko ndani yenu, au pengine mmeshindwa kufikia kipimo hicho? 6 Natumaini mtagundua ya kuwa sisi hatu kushindwa kufikia kipimo hicho. 7 Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda jambo lo lote ambalo ni kosa; si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaone kana kuwa tumeshindwa. 8 Kwa maana hatuwezi kufanya lo lote kupinga kweli, bali kuithibitisha kweli. 9 Tunafurahi wakati wo wote sisi tunapokuwa wadhaifu na ninyi mkawa wenye nguvu. Tuna choomba ni kwamba mpate kukomaa katika imani. 10 Nawaandikieni haya wakati nikiwa mbali ili nitakapokuja nisiwe na sababu ya kuwa mkali katika kutumia madaraka ambayo Bwana amenipa kuwa jenga, na sio kuwagandamiza. 11 Hatimaye ndugu zangu, kwaherini. Sahihisheni mwenendo wenu, pokeeni ushauri wangu; sikilizaneni ninyi kwa ninyi; kaeni kwa amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 12 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. 13 Watakatifu wote wanawasalimu.
Copyright © 1989 by Biblica