M’Cheyne Bible Reading Plan
24 Siku ya Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake wali chukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa wakaenda kaburini. 2 Wakakuta jiwe limeondolewa kwenye mlango wa kaburi. 3 Lakini walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu. 4 Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hilo, ghafla, watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa sana, wakasimama karibu nao. 5 Wale wanawake, kwa hofu, wakainamisha nyuso zao chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai mahali pa wafu? 6 Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa Gali laya, 7 kwamba ilikuwa lazima Mwana wa Adamu awekwe mikononi mwa watu waovu, asulubiwe na siku ya tatu afufuke.” 8 Wakayakumbuka maneno ya Yesu. 9 Waliporudi kutoka huko kaburini wakaeleza mambo haya kwa wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote. 10 Hao wanawake walikuwa ni Mariamu Magdalene, Yoana na Mariamu mama yake Yakobo pamoja na wengine waliofuatana nao. 11 Maelezo yao yalionekana kama upuuzi kwa hiyo hawakuwaamini. 12 Bali Petro akaondoka mbio, akaenda kaburini. Alipoinama, akaiona ile sanda, ila hakuona kitu kingine zaidi. Akarudi nyumbani akis taajabia yaliyotokea.
Yesu Awatokea Wanafunzi Wawili
13 Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu, 14 nao walikuwa wakizungumzia mambo yote yaliyotokea. 15 Wali pokuwa wakizungumza, Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao, 16 lakini wao hawakumtambua. 17 Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumzia wakati mnatembea?” Wakasimama , nyuso zao zikionyesha huzuni. 18 Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamwambia, “Nadhani ni wewe tu katika watu wote wanaoishi Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotokea siku hizi chache zilizopita.”
19 Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu “Mambo yaliyompata Yesu Mnazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele za wanadamu. 20 Makuhani wakuu na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa na wakamsulubisha. 21 Na sisi tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angeliikomboa Israeli. Zaidi ya hayo leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. 22 Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtua; walikwenda kaburini leo alfajiri 23 lakini hawakuukuta mwili wake. Waliporudi walisema wamewaona malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai. 24 Baadhi yetu walikwenda kaburini wakakuta mambo ni kama walivyoelezea wale wanawake, ila yeye mwenyewe hawakumwona.”
25 Kisha Yesu akawaambia, “Ninyi ni watu wajinga. Mbona mnaona ugumu kuamini mambo yote yaliyosemwa na Manabii? 26 Je, haikumpasa Kristo kuteswa na kwa njia hiyo aingie katika utukufu wake?” 27 Akawafafanulia maandiko yalivyosema kumhusu yeye, akianzia na maandiko ya Musa na kupitia maandiko yote ya manabii.
28 Walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea na safari. 29 Lakini wakamsihi akae nao wakisema, “Kaa hapa nasi kwa maana sasa ni jioni na usiku unain gia.” Basi akaingia ndani kukaa nao. 30 Alipokuwa nao mezani, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua! Lakini akatoweka, hawakumwona tena.
32 Wakaulizana, “Je, mioyo yetu haikuchangamka kwa furaha alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?” 33 Wakaondoka mara moja, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusany ika 34 wakisema, “Ni kweli Bwana amefufuka! Amemtokea Simoni.” 35 Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotokea njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate. Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
36 Wakati walipokuwa wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasi mama katikati yao akawasalimu, “Amani iwe nanyi.”
37 Wakashtuka na kuogopa wakidhani wameona mzimu. 38 Lakini akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna mashaka mioyoni mwenu? 39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu mwone kuwa ni mimi. Niguseni mwone. Mzimu hana nyama na mifupa kama mnion avyo.” 40 Aliposema haya aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula cho chote hapa?” 42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa, 43 akakichukua akakila mbele yao.
44 Akawaambia, “Haya ndiyo mambo niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi; kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika she ria ya Musa, katika Maandiko ya manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.” 45 Akawapa uwezo wa kuyaelewa Maandiko, 46 aka waambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. 47 Habari hii ya wokovu itatan gazwa kwanza Yerusalemu hadi kwa mataifa yote, kwamba: kuna msa maha wa dhambi kwa wote watakaotubu na kunigeukia mimi. 48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. 49 Na sasa nitawapelekea Roho Mtaka tifu kama alivyoahidi Baba yangu; lakini kaeni humu Yerusalemu mpaka mtakapopewa nguvu ya Roho Mtakatifu kutoka mbinguni.”
Yesu Apaa Mbinguni
50 Kisha akawaongoza nje ya mji mpaka Bethania, akainua mikono yake, akawabariki. 51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni. 52 Wakamwabudu na kisha wakarudi Yerus alemu wamejawa na furaha;
Wasaidieni Wakristo Wenzenu
9 Hakuna sababu ya kuwaandikia kuhusu msaada unaotolewa kwa ajili ya watu wa Mungu, 2 kwa kuwa ninajua mlivyo tayari kutoa, nami nimekuwa nikijivuna kwa ajili yenu kwa watu wa Makedonia, nikiwaambia kuwa ninyi wa Akaya mmekuwa tayari kutoa tangu mwaka jana. Ari yenu imewachochea wengi wao kuanza kutoa. 3 Lakini sasa nawatuma hawa ndugu ili kujivuna kwetu kuhusu mchango wenu kusije kukawa ni maneno matupu, bali muwe tayari kama nilivyosema mko tayari. 4 Isije ikawa nitakapokuja na watu wa Makedonia nikute hamko tayari niaibike, na ninyi zaidi, kwa kuwa nilishasema mko tayari. 5 Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kabla yangu, wafanye mipango yote ya matoleo ya zawadi mliyoahidi ili iwe tayari, si kama mchango wa kulazim ishwa bali kama zawadi ya hiari.
6 Kumbukeni kwamba, mtu anayepanda mbegu chache, atavuna mazao machache; na mtu anayepanda mbegu nyingi atavuna mazao mengi. 7 Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa kusita au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu anapenda mtu anayetoa kwa moyo. 8 Na Mungu anaweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili kila wakati muwe na kila kitu kwa kiasi cha kutosha na ziada kwa ajili ya kila kazi njema. 9 Kama Maandiko yanavyosema, “Yeye hutapanya kila mahali kuwapa maskini, haki yake hudumu milele.” 10 Na Mungu ambaye ndiye humpa mkulima mbegu za kupanda, na mkate kwa chakula, atawapa na kuzidisha mbegu mnazohitaji na kuziwezesha kukua zitoe mazao ya matendo mema ya haki. 11 Atawa fanya kuwa matajiri kwa kila hali ili mpate kuwa wakarimu kila wakati na kwa mchango wenu wa hiari kupitia kwetu, wengi wapate kumshukuru Mungu. 12 Huduma hii mnayofanya si kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watu wa Mungu, bali utaleta mbubujiko wa shukrani nyingi kwa Mungu tu. 13 Kwa kutoa kwenu, mtakuwa mnatoa uthibitisho wa uhakika wa imani yenu. Ndipo watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu unaoambatana na kukiri kwenu kwa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wa mchango wenu kwao na kwa wen gine wote. 14 Nao watawaombea kwa upendo mwingi kwa ajili ya neema kuu mliyopewa na Mungu. 15 Tumshukuru Mungu kwa ajili ya zawadi hii isiyoelezeka.
Copyright © 1989 by Biblica