Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Exod for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Luka 14

14 Siku moja ya sabato Yesu alipokuwa amekwenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, watu walikuwa wakimtazama kwa makini. Mtu mmoja mwenye ugonjwa wa kuvimba miguu na mikono akaja mbele yake. Yesu akawauliza walimu wa sheria na Mafari sayo, “Je, sheria inaruhusu kumponya mtu siku ya sabato au hairuhusu?” Wakakaa kimya. Basi Yesu akamshika yule mgonjwa akamponya, akamruhusu aende zake. Kisha akawauliza, “Kama mmoja wenu angekuwa na mtoto au ng’ombe wake ambaye ametumbukia katika kisima siku ya sabato, hamtamvuta mara moja na kumtoa?” Hawakuwa na la kujibu.

Alipoona jinsi wageni walioalikwa walivyokuwa wakichagua viti vya wageni wa heshima, akawaambia mfano huu: “Mtu akiku alika harusini, usikae kwenye kiti cha mgeni wa heshima. Inaweze kana kuwa amealika mheshimiwa akuzidiye, na yule aliyewaalika ninyi wawili akaja kukuambia, ‘Tafadhali mpishe huyu bwana.’ Ndipo kwa aibu utalazimika kwenda kukaa katika kiti cha nyuma kabisa. 10 Badala yake, unapoalikwa, chagua kiti cha nyuma; na mwenyeji wako akikuona atakuja akuambie, ‘Rafiki yangu, njoo kwe nye nafasi ya mbele zaidi.’ Kwa jinsi hii utakuwa umepewa heshima mbele ya wageni wote. 11 Kwa maana kila mtu anayejitukuza atash ushwa naye ajishushaye atatukuzwa.”

12 Kisha Yesu akamwambia yule aliyewaalika, “Uandaapo kar amu ya chakula cha mchana au jioni, usialike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako tajiri; ukifanya hivyo wao nao watakualika kwao na hivyo utakuwa umelipwa kwa kuwaalika. 13 Bali ufanyapo karamu, waalike maskini, vilema na vipofu; 14 nawe utapata baraka kwa sababu hawa hawana uwezo wa kukulipa.

Mfano Wa Karamu Ya Ufalme Wa Mbinguni

15 Mmoja wa wale waliokuwa mezani pamoja naye aliposikia maneno haya akamwambia, “Ana heri mtu atakayepata nafasi ya kula katika karamu ya Ufalme wa Mbinguni!” 16 Yesu akamjibu, ‘ ‘Mtu mmoja alikuwa anaandaa karamu kubwa, akaalika watu wengi. 17 Wakati wa sherehe ulipofika, akamtuma mtumishi wake akawaam bie walioalikwa, ‘Karibuni, kila kitu ni tayari sasa.’ 18 Lakini wote, mmoja mmoja, wakaanza kutoa udhuru. Wa kwanza akasema, ‘ Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’ 19 Mwingine akasema, ‘Nimenunua ng’ombe wa kulimia, jozi tano; nimo njiani kwenda kuwajaribu, tafadhali niwie radhi.’ 20 Na mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’

21 “Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’

22 “Baadaye yule mtumishi akamwambia ‘Bwana, yale uliyon iagiza nimefanya, lakini bado ipo nafasi.’ 23 Ndipo yule bwana akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda kwenye barabara na njia zilizoko nje ya mji uwalazimishe watu waje mpaka nafasi zote zijae. 24 Ninawaambia, hakuna hata mmoja wa wale niliowapelekea mwaliko rasmi atakayeionja karamu yangu.”

Gharama Ya Kuwa Mfuasi Wa Yesu

25 Wakati mmoja umati mkubwa wa watu ulipokuwa ukifuatana na Yesu, yeye aligeuka, akawaambia, 26 “Mtu ye yote anayekuja kwangu hawezi kuwa mfuasi wangu kama hatanipenda mimi zaidi ya baba yake na mama yake, mke wake na watoto, kaka zake na dada zake; naam, hata maisha yake mwenyewe. 27 Na ye yote asiyebeba msalaba wake na kunifuata hawezi kuwa mfuasi wangu.

28 “Ni nani kati yenu ambaye kama anataka kujenga, hatakaa kwanza na kufanya makisio ya gharama aone kama ana fedha za kutosha kukamilisha ujenzi? 29 Kwa maana ikiwa atajenga msingi halafu ashindwe kuendelea, wote watakaouona watamcheka 30 wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga lakini ameshindwa kumal iza!’

31 “Au tuseme mfalme mmoja anataka kwenda vitani kupigana na mfalme mwingine: si atakaa kwanza ajishauri kama yeye na jeshi lake lenye watu elfu kumi ataweza kupigana na yule anayekuja na watu elfu ishirini? 32 Kama hawezi, basi itambidi apeleke wajumbe wakati yule mfalme mwingine bado yuko mbali na kuomba masharti ya amani. 33 Hali kadhalika, hakuna mtu atakayeweza kuwa mfuasi wangu kama hataacha vyote alivyo navyo.”

Chumvi Isiyofaa

34 “Chumvi ni kitu kizuri. Lakini chumvi ikiwa imepoteza ladha yake, haiwezi kuwa chumvi tena. 35 Haifai kuwa udongo wala kuwa mbolea; watu huitupa nje. Mwenye nia ya kusikia na asikie!” Mfano Wa Kondoo Aliyepotea

Error: Book name not found: Job for the version: Neno: Bibilia Takatifu
1 Wakorintho 15

Kufufuka Kwa Kristo

15 Na sasa napenda kuwakumbusha ndugu zangu kuhusu Injili niliyowahubiria, mkaipokea na ambayo ndio msimamo wenu. Mnaoko lewa kwa Injili hii ikiwa mnashikilia imara neno nililowahubiria. Vinginevyo mtakuwa mmeamini bure. Kwa maana niliyopokea ndio niliyowapa ninyi, nayo ni muhimu sana: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama ilivy oandikwa katika Maandiko. Na kwamba alizikwa na kufufuka siku ya tatu, kama ilivyoandikwa katika Maandiko. Na kwamba alimto kea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili. Baadaye akawa tokea ndugu waamini zaidi ya mia tano kwa pamoja, na wengi wao wangali hai, ingawa wengine wameshakufa. Kisha akamtokea Yakobo, na ndipo akawatokea mitume wote. Na mwisho wa wote, akanitokea na mimi, ambaye ni kama nilizaliwa kwa hali isiyo ya kawaida.

Kwa maana mimi ni mdogo kuliko mitume wote, nisiyestahili kuitwa mtume kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu. 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya kazi kuliko mitume wote, ingawaje haikuwa mimi bali ni neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami. 11 Hivyo basi, kama ilikuwa ni mimi au ni wao, haya ndio tuliyohubiri, na haya ndio mliyoamini.

Kufufuka Kwa Wafu

12 Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu, inakuwaje baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu? 13 Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi Kristo hakufufuliwa. 14 Na ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, mahubiri yetu ni bure na imani yenu ni bure. 15 Na zaidi ya hayo, tunaonekana kuwa tunamshuhudia Mungu uongo, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu ya kuwa alimfufua Kristo kutoka kwa wafu. Na kumbe hakumfu fua, kama kweli wafu hawafufuliwi. 16 Kwa kuwa kama wafu hawa fufuliwi, basi hata Kristo hajafufuliwa. 17 Na ikiwa Kristo hajafufuliwa, imani yenu ni bure; nanyi bado mngali katika dhambi zenu. 18 Pia waamini wote waliokufa wakimwamini Yesu wamepotea. 19 Na kama imani yetu ndani ya Kristo ni kwa ajili ya maisha haya tu, basi sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wengine wo wote duniani. 20 Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, matunda ya kwanza ya wote waliolala. 21 Kwa maana kama vile kifo kilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja. 22 Kwa kuwa katika Adamu watu wote hufa, vivyo hivyo katika Kristo wote wata fanywa kuwa hai. 23 Lakini kila mmoja kwa mpango: Kristo ni mat unda ya kwanza ya ufufuo; kisha wale walio wake wakati atakapo kuja watafufuliwa. 24 Ndipo mwisho utafika, wakati ambao ataka bidhi Ufalme kwa Mungu Baba, akiisha angamiza kila mamlaka na uwezo na nguvu. 25 Kwa maana Kristo atamiliki mpaka Mungu ataka powaweka adui zake chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho kuan gamizwa ni kifo. 27 “Kwa maana Mungu ameweka kila kitu chini ya utawala wake, chini ya miguu yake.” Ni wazi kwamba maneno haya, “Kila kitu kimewekwa chini ya utawala wake,” hayamjumlishi na Mungu ambaye ameweka vitu vyote chini ya Kristo. 28 Vitu vyote vikishawekwa chini ya utawala wake, ndipo naye Mwana atakuwa chini ya Mungu ambaye ameviweka vitu vyote chini yake, ili Mungu awe yote katika yote.

29 Vinginevyo, kwa nini watu wanabatizwa kwa niaba ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, mbona watu wanabatizwa kwa niaba yao? 30 Na kwa upande wetu kwa nini tunajitia hatarini kila wakati? 31 Nakufa kila siku, nasema kweli ndugu zangu, kama ninavyojivuna kwa ajili yenu katika Kristo Yesu, Bwana wetu. 32 Kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso kwa sababu za kibinadamu, nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi, basi, “Tule na kunywa, kwa maana kesho tutakufa.” 33 Mtu asiwadanga nye, “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 34 Pateni tena fahamu, muache kutenda dhambi. Kwa maana baadhi yenu hawam jui Mungu; nasema mambo haya ili muone aibu.

Ufufuo Wa Mwili

35 Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wanafufuliwaje? Wata kuwa na mwili wa namna gani?” 36 Wapumbavu ninyi! Mnachopanda hakiwi hai tena kama hakikufa. 37 Unapopanda, hupandi mwili unaoutegemea, bali unapanda mbegu, pengine mbegu ya ngano au ya nafaka nyingine. 38 Lakini Mungu huipa hiyo mbegu umbo kama alivyochagua mwenyewe, na kila aina ya mbegu ina umbo lake. 39 Kwa maana nyama zote si za aina moja. Binadamu wana nyama ya aina moja, wanyama wana aina nyingine na hali kadhalika ndege na samaki wana nyama tofauti. 40 Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani; lakini uzuri wa miili ya mbinguni ni wa aina moja na uzuri wa miili ya duniani ni wa aina nyingine. 41 Jua lina uzuri wa aina moja, mwezi nao una uzuri wake na nyota pia; na nyota hutofautiana na nyota nyingine kwa uzuri.

42 Ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Mwili uliopandwa ni wakuharibika; utafufuliwa usioharibika; 43 unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu; unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu. 44 Unapandwa ukiwa mwili wa asili, unafufuliwa ukiwa mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia. 45 Kwa hiyo imeandikwa, “Adamu wa kwanza akawa kiumbe hai,” Adamu wa mwisho akawa roho inayohuisha. 46 Lakini si yule wa kiroho aliyekuja kwanza; bali ni yule wa mwili, na kisha yule wa kiroho. 47 Mtu wa kwanza alitokana na mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. 48 Na kama alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na alivyo mtu wa mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyochukua umbile la mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua umbile la yule mtu kutoka mbinguni. 50 Nawatangazia ndugu zangu kwamba nyama na damu haviwezi kurithi Ufalme wa Mungu, wala uharibifu hauwezi kurithi kutokuharibika.

51 Sikilizeni, nawaambia siri: sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa 52 ghafla, kufumba na kufumbua, tarumbeta ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa tarumbeta italia, wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. 53 Kwa maana hali hii ya kuharibika lazima ivae kutokuharibika, na hali hii ya kufa lazima ivae hali ya kutokufa. 54 Kwa hiyo, wakati kuharibika kutakapovaa kutokuharibika, na mwili wa kufa utakapovaa hali ya kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia, “Kifo kimemezwa na ushindi .” 55 “Mauti, ushindi wako uko wapi? Na uchungu wako uko wapi?” 56 Uchungu wa kifo ni dhambi, na nguvu ya dhambi ni sheria. 57 Lakini, Mungu ashukuriwe! Yeye anatupa tia ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

58 Kwa hiyo ndugu zangu, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, juhudi yenu si bure katika Bwana.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica