M’Cheyne Bible Reading Plan
11 Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomal iza, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tafadhali tufundishe kuomba kama Yohana Mbatizaji alivyowafundisha wana funzi wake.” 2 Akawaambia, “Mnapoomba, semeni hivi: Baba, Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje. 3 Utupatie chakula chetu kila siku. 4 Utusamehe dhambi zetu kwa kuwa na sisi tunawasamehe wote wanaotukosea. Na usitutie katika majaribu.” 5 Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu ana rafiki yake. Akamwendea usiku wa manane akamwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. 6 Nimefikiwa na rafiki yangu akiwa safarini nami sina chakula cha kumpa.’ 7 Yule aliyeko ndani akajibu, ‘Usinisumbue! Nimekwisha kufunga mlango. Na mimi na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka kukupa cho chote.’ 8 “Nawaambieni, hata kama huyo mtu hataamka na kumpa mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ameendelea kuomba bila kukata tamaa ataamka ampe kiasi anachohitaji. 9 Kwa hiyo nawaambia, ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni, nanyi mtafunguliwa mlango. 10 Kwa kuwa kila anayeomba hupewa; naye atafutaye, hupata; na kila abishaye, hufunguliwa mlango. 11 “Ni baba yupi miongoni mwenu, ambaye mtoto wake akimwomba samaki, atampa nyoka badala yake? 12 Au akimwomba yai atampa nge? 13 Ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi; atawapa Roho
Yesu Na Beelzebuli
14 Yesu alikuwa anamtoa pepo mtu mmoja ambaye alikuwa bubu. Pepo huyo alipotoka, yule mtu akaanza kusema! Watu wakashangaa. 15 Lakini wengine wakasema: “Anatoa pepo kwa uwezo wa Beelzeb uli, yule mkuu wa pepo wote.” 16 Wengine wakamjaribu kwa kum womba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.
17 Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, “Nchi yo yote iliyo na mgawanyiko wa vikundi-vikundi vinavyopingana au familia yenye mafarakano, huangamia. 18 Kama ufalme wa shetani ungekuwa umega wanyika wenyewe kwa wenyewe ungesimamaje? Nasema hivi kwa sababu mnasema ninaondoa pepo kwa uwezo wa Beelzebuli. 19 Kama mimi ninaondoa pepo kwa nguvu za Beelzebuli, wafuasi wenu je, wao huwaondoa pepo kwa uwezo wa nani? Wao watawaamulia. 20 Lakini kwa kuwa ninaondoa pepo kwa uwezo wa Mungu, basi Ufalme wa Mungu umewajia. 21 Mtu mwenye nguvu aliye na silaha anapoilinda nyumba yake, mali yake ni salama. 22 Lakini mtu mwenye nguvu zaidi akimshambulia na kumshinda, atamnyang’anya silaha alizozitegemea na kugawanya mali yote. 23 “Mtu ambaye hayuko upande wangu, anapingana nami, na mtu asiyekusanya pamoja nami, anatawanya.
24 “Pepo mchafu akimtoka mtu, anazunguka jangwani akitafuta mahali pa kupumzikia. Asipopata anasema, ‘Kwa nini nisirudi kwe nye nyumba yangu niliyotoka?’ 25 Akirudi, na kuikuta ile nyumba ni safi na imepangwa vizuri, 26 huenda kuwaleta pepo wengine saba wachafu kuliko yeye wakaingia na kuishi humo. Na hali ya sasa ya mtu huyo inakuwa mbaya kuliko ya kwanza.”
27 Alipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika umati akasema kwa nguvu, “ Amebarikiwa mama aliyekuzaa na kukunyon yesha.” 28 Yesu akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulifuata.”
Ishara Ya Yona
29 Umati wa watu ulipozidi kuongezeka, Yesu aliendelea kufundisha akisema, “Watu wa kizazi hiki ni waovu. Wanatafuta ishara lakini hawatapewa ishara yo yote isipokuwa ile ya nabii Yona. 30 Kwa maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo mimi Mwana wa Adamu nitakavyokuwa ishara kwa kizazi cha sasa. 31 Siku ya hukumu malkia wa Sheba atashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu yeye alisafiri kutoka mbali kuja kusikiliza hekima ya Sulemani. Lakini sasa, aliye mkuu kuliko Sulemani yuko hapa. 32 Siku ile ya hukumu, watu wa Ninawi watashuhudia kwamba watu wa sasa wana hatia kwa sababu Yona ali powahubiria waliacha dhambi zao. Lakini sasa aliye mkuu kuliko
Taa Ya Mwili
33 “Hakuna mtu awashaye taa akaificha au kuifunika, ila huiweka mahali pa juu ili watu wote wanaoingia waone nuru yake. 34 Jicho lako ni nuru ya mwili wako. Macho yakiwa mazima huan gaza mwili wako wote; lakini yakiwa mabovu, mwili wako pia uta kuwa katika giza. 35 Kwa hiyo hakikisha kwamba una nuru ndani yako, wala si giza. 36 Ikiwa mwili wako wote una nuru, bila sehemu yo yote kuwa gizani, basi utang’aa kabisa kama inavyokuwa wakati taa inapokuangazia.”
Yesu Awaonya Mafarisayo Na Wanasheria
37 Yesu alipomaliza kuzungumza, Farisayo mmoja alimkaribisha nyumbani kwake kwa chakula. Yesu akaingia na kuketi chakulani moja kwa moja. 38 Farisayo yule alipoona kwamba Yesu hakunawa kwanza kabla ya kula alishangaa. 39 Ndipo Bwana akamwambia, “Ninyi Mafarisayo mnasafisha kikombe na sahani kwa nje huku ndani mmejaa udhalimu na uovu. 40 Wajinga Ninyi! Hamjui kuwa yeye aliyetengeneza sehemu ya nje ndiye aliyetengeneza na ya ndani pia? 41 Watendeeni ukarimu maskini kwa kuwapa vilivyomo ndani ya vikombe na sahani zenu na kila kitu kitakuwa safi kwenu.
42 “Lakini ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnamtolea Mungu sehemu ya kumi ya mnanaa, mchicha na kila aina ya mboga lakini mnapuuza haki na kumpenda Mungu. Mngeweza kutoa matoleo hayo pasipo kusahau haki na upendo kwa Mungu.
43 “Ole wenu, Mafarisayo! Ninyi mnapenda kuketi viti vya mbele katika masinagogi na kusalimiwa kwa heshima masokoni! 44 Ole wenu! Kwa maana ninyi ni kama makaburi yasiyokuwa na alama, ambayo watu huyakanyaga pasipo kujua.”
45 Mwalimu mmoja wa sheria akasema, “Mwalimu, unapozungumza hivyo unatushutumu na sisi wanasheria!” 46 Yesu akamjibu, “Hata ninyi wanasheria, ole wenu! Mnawabebesha watu mzigo wa sheria ambazo hawawezi kuzitimiza; wala hamfanyi lo lote kuwa saidia iwe rahisi kwao kuzitimiza. 47 Ole wenu kwa kuwa mnawa jengea makaburi manabii waliouawa na babu zenu. 48 Kwa kufanya hivyo mnakiri kwamba mnaunga mkono kitendo hicho walichofanya babu zenu. Wao waliua na ninyi mnatengeneza makaburi.
49 “Ndio maana Mungu katika hekima yake alisema, ‘Nita wapeleka manabii na mitume, na baadhi yao watawaua na wengine watawatesa.’ 50 Kwa hiyo damu ya manabii wote iliyomwagika tangu mwanzo wa dunia itahesabiwa juu ya watu wa kizazi hiki; 51 tangu damu ya Abeli mpaka damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhabahu na mahali patakatifu. Nawaambia kweli, watu wa kizazi hiki wataadhibiwa kwa ajili yao wote. 52 Ole wenu ninyi wanashe ria kwa maana mmeuchukua ufunguo unaofungua nyumba ya maarifa. Ninyi wenyewe hamkuingia na wale waliokuwa wanaingia mkawazuia.”
53 Yesu alipoondoka hapo, walimu wa sheria na Mafarisayo wakawa wanampinga vikali na kumwuliza maswali mengi, 54 wakijar ibu kumtega ili aseme kitu ambacho watakitumia kumshitaki.
Karama Za Roho Mtakatifu
12 Sasa kuhusu karama za Roho Mtakatifu ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu. 2 Mnajua kwamba mlipokuwa hamumjui Mungu mlivutwa na kupotoshwa na sanamu bubu.
3 Kwa hiyo napenda mfahamu ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kukiri, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu. 4 Basi kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni mmoja. 5 Pia kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni mmoja. 6 Kisha kuna aina tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule anayeongoza kazi zote kwa kila mtu. 7 Roho Mtakatifu hudhi hirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote.
8 Maana mtu mmoja hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine hupewa neno la ufahamu kutoka kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine hupewa imani na huyo Roho na mwingine karama za kuponya. 10 Huyo huyo Roho humpa mwingine uwezo wa kufanya miujiza, mwin gine unabii, mwingine uwezo wa kutofautisha kati ya roho mbalim bali, mwingine aina za lugha na mwingine uwezo wa kutafsiri lugha. 11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.
Mwili Mmoja, Viungo Vingi
12 Kama vile mwili ulivyo mmoja lakini una viungo vingi, na viungo vyote ingawa ni vingi vinafanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo na Kristo. 13 Kwa maana tumebatizwa na Roho mmoja katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wagiriki, kama ni watumwa au watu huru; nasi tumepewa tunywe, huyo Roho mmoja.
14 Mwili si kiungo kimoja, bali una viungo vingi. 15 Kama mguu ungesema, “Kwa kuwa mimi si mkono basi mimi si sehemu ya mwili.” Hiyo isingefanya huo mkono usiwe sehemu ya mwili. 16 Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si sehemu ya mwili.” Hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili. 17 Kama mwili mzima ungelikuwa jicho, ungelisikiaje? Au kama mwili wote ungelikuwa sikio, ungelinusa namna gani? 18 Lakini kama mwili ulivyo, Mungu alipanga viungo vyote katika mwili, kimoja kimoja, kama alivyopenda. 19 Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja mwili ungekuwa wapi? 20 Kama mwili ulivyo, kuna viungo vingi, lakini mwili ni mmoja.
21 Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sikuhitaji!” Na kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sikuhitaji!” 22 Kinyume chake, vile viungo vya mwili ambavyo vinaonekana kuwa dhaifu ndivyo ambavyo ni vya muhimu sana. 23 Na vile viungo vya mwili ambavyo tunav iona havina heshima ndivyo tunavipa heshima ya pekee. Na vile viungo vya mwili ambavyo hatuwezi kuvionyesha, tunavitunza kwa adabu 24 ambayo vile viungo vyenye uzuri wa kuonekana havihi taji. Lakini Mungu ameviweka pamoja viungo vya mwili na akavipa heshima zaidi vile visivyokuwa na heshima, 25 ili pasiwe na mga wanyiko katika mwili, bali viungo vyote visaidiane kwa usawa. 26 Kama kiungo kimoja cha mwili kikiteseka, viungo vyote vinateseka pamoja; kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote vinafurahi pamoja.
27 Basi ninyi ni mwili wa Kristo, na kila mmoja wenu ni kiungo cha huo mwili. 28 Na Mungu ameteua katika kanisa, kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, kisha waponyaji, wasaidizi, watawala, wasemaji wa lugha mbalimbali. 29 Je, wote ni mitume? Au wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote wanafanya miujiza? 30 Je, wote wana karama ya kuponya? Wote wanasema kwa lugha ngeni? Wote wanatafsiri lugha? 31 Basi takeni kwa moyo karama zilizo bora. Nami nitawaonyesha njia iliyo bora kupita zote.
Copyright © 1989 by Biblica