M’Cheyne Bible Reading Plan
10 Baada ya hayo, Yesu akawachagua wafuasi wengine sabini na wawili akawatuma wawili wawili katika kila mji na kila sehemu aliyokusudia kwenda. 2 Akawaambia, “Mavuno ni mengi lakini wafanya kazi ni wachache, kwa hiyo mwombeni Bwana wa mavuno awapeleke wavunaji zaidi katika shamba lake. 3 Haya, nendeni. Ninawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu. 4 Msichukue mkoba wala mfuko, wala viatu; na msipoteze muda kumsalimu mtu ye yote njiani. 5 Mkiingia nyumba yo yote kwanza semeni, ‘Amani iwe kwenu.’ 6 Kama aishiye humo ni mwenye kupenda amani basi baraka hiyo itakaa naye, la sivyo, itawarudia. 7 Kaeni katika nyumba hiyo mkila na kunywa kile watakachowapa kwa sababu kila mfany akazi anastahili kulipwa mshahara. Msihamehame kutoka nyumba hadi nyumba. 8 Mkienda katika mji mkapokelewa: kuleni mtakachoandal iwa; 9 waponyeni wagonjwa na waambieni: ‘Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu.’
10 “Lakini mkiingia katika mji msikaribishwe, nendeni katika mitaa yake mkaseme: 11 ‘Hata mavumbi ya mji wenu yaliyoko miguuni mwetu tunayakung’uta juu yenu; lakini fahamuni ya kwamba Ufalme wa Mungu umekuja karibu yenu!’ 12 “Nawahakikishia kwamba siku ile Mungu atakapouhukumu ulimwengu adhabu ya Sodoma itakuwa nafuu kuliko ya mji huo! 13 Ole wenu watu wa Korazini na wa Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifany ika Tiro na Sidoni watu wa huko wangalitubu zamani, wakivaa magu nia na kujimwagia majivu kama dalili ya majuto. 14 Lakini siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Tiro na Sidoni kuliko kwenu. 15 Na ninyi je, watu wa Kapernaumu, mnafikiri mtainuliwa juu hadi mbinguni? La, Mungu atawatupa chini hadi kuzimuni. 16 “Ye yote atakayewasikiliza ninyi amenisikiliza mimi, naye awakataaye amenikataa. Lakini anikataaye mimi amemkataa yeye aliyenituma.”
17 Wale wanafunzi sabini na wawili wakarudi wakiwa na furaha. Wakamwambia Yesu, “Bwana, tukilitumia jina lako, hata pepo wanatutii!” 18 Akawajibu, “Nimemwona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni. 19 Nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na kushinda nguvu zote za yule adui; wala hakuna kitu cho chote kitakachoweza kuwadhuru. 20 Lakini msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii, ila furahini kwa kuwa majina yenu yamean dikwa mbinguni.”
21 Wakati huo, Yesu akiwa amejawa na furaha ya Roho Mtaka tifu, akasema, “Ninakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya ambayo umewaficha wenye elimu na wenye hekima umependa kuwafunulia wale wakuaminio kama watoto wadogo. Na haya yote yamefanyika kwa mapenzi yako Baba. 22 Baba yangu amenika bidhi mambo yote. Hakuna anayemfahamu Mwana isipokuwa Baba: na hakuna anayemfahamu Baba isipokuwa Mwana na wale ambao Mwana ame penda humdhihirisha Baba kwao.” 23 Basi Yesu akawageukia wana funzi wake akawaambia faraghani, “Mmebarikiwa kuona mambo haya mnayoyaona! 24 Nawaambie ni kweli, manabii wengi na wafalme wal itamani kuona mnayoyaona na kusikia mnayoyasikia lakini hawaku pata nafasi hiyo.” Mfano Wa Msamaria Mwema
25 Mwalimu mmoja wa sheria alisimama akajaribu kumpima Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?” 26 Yesu akamjibu, “Sheria inasemaje? Unaitafsiri vipi?” 27 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote. Na umpende jirani yako kama unavyojipenda mwe nyewe.” 28 Yesu akamwambia, “Jibu lako ni sahihi. Fanya hivyo nawe utaishi.” 29 Lakini yule mwalimu wa sheria akitaka kuon yesha kwamba hoja yake ilikuwa na maana zaidi, akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”
30 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja aliteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Njiani akashambuliwa na majambazi; wakamwibia kila kitu alichokuwa nacho, wakampiga wakamwacha karibu ya kufa. 31 litokea kwamba kuhani mmoja alikuwa anapitia njia ile. Ali pomwona huyo mtu, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo. 32 Vivyo hivyo Mlawi mmoja naye alipopita, alimwona, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo.
33 “Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri kupitia njia hiyo alipomkuta, alimwonea huruma, 34 akamwendea akasafisha maj eraha yake kwa divai na mafuta, akayafunga. Kisha akamweka kwenye punda wake akaenda naye mpaka nyumba ya wageni ambapo alimtunza. 35 Kesho yake, yule Msamaria alipokuwa anaondoka, akampa mwenye nyumba ya wageni fedha akamwomba amtunze yule mgonjwa na akaahidi kulipa gharama yo yote ya ziada atakaporudi.
36 “Unadhani ni yupi kati ya hawa watatu alikuwa jirani yake yule mtu aliyeshambuliwa na majambazi?”
37 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesu akasema, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”
Yesu Awatembelea Martha na Mariamu
38 Wakati Yesu na Wanafunzi wake walipokuwa wakiendelea na safari yao ya kwenda Yerusalemu, walifika katika kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha Yesu nyum bani kwake. 39 Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Mariamu ambaye aliketi chini karibu na Yesu akisikiliza mafundisho yake.
40 Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote. Kwa hiyo alikuja kwa Yesu akalalamika, “Bwana, hujali kwamba mdogo wangu ameniachia kazi zote? Mwambie aje anisaidie!” 41 Bwana akamjibu, “Martha! Martha! Mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? 42 Unahitaji kujua kitu kimoja tu. Mariamu amechagua kil icho bora, na hakuna mtu atakayemnyang’anya.” Yesu Awafundisha Wanafunzi Wake Kuomba
Utaratibu Wa Kuabudu
11 Niigeni mimi, kama mimi ninavyomuiga Kristo. 2 Ninawasifu kwa sababu mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kuwa mnashika mafundisho niliyowakabidhi. 3 Lakini napenda muelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo. 4 Kwa hiyo mwanamume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anaaib isha kichwa chake. 5 Na mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo kufunika kichwa chake, anaaibisha kichwa chake, ni sawa kama ame nyoa nywele zote kichwani. 6 Kama mwanamke hataki kufunika kichwa chake, nywele zake zinyolewe; na kama ni aibu kwa mwanamke kunyoa kichwa chake, au kukata nywele zake, basi afunike kichwa chake. 7 Mwanamume asifunike kichwa chake kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. 8 Kwa maana mwanamume hakuumbwa kutoka kwa mwanamke, bali mwanamke ame toka kwa mwanamume. 9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwa namke, bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume. 10 Hii ndio sababu inampasa mwanamke afunike kichwa chake na kwa ajili ya malaika. 11 Lakini katika Bwana mwanamke hawezi kufanya lo lote pasipo mwanamume, wala mwanamume hawezi kufanya lo lote pasipo mwanamke. 12 Kwa maana kama vile mwanamke alivyoumbwa kutoka kwa mwanamume, vivyo hivyo sasa mwanamume anazaliwa na mwanamke. Lakini vitu vyote vinatoka kwa Mungu.
13 Amueni wenyewe, je, ni sawa kwa mwanamke kumwomba Mungu akiwa hakufunika kichwa chake? 14 Je, maumbile ya asili hayatu fundishi kuwa ni aibu kwa mwanamume kuwa na nywele ndefu? 15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni sifa kwake. Kwa maana mwanamke amepewa nywele ndefu za kumfunika. 16 Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makanisa ya Mungu hatutambui desturi nyingine.
Chakula Cha Bwana
17 Kuhusu maagizo yafuatayo, siwezi kuwasifu kwa sababu mikutano yenu inaleta madhara zaidi kuliko mema. 18 Kwanza, mna pokutana kama kanisa nasikia kwamba kuna mgawanyiko kati yenu, na kwa kiasi fulani naamini ndivyo ilivyo. 19 Bila shaka lazima pawe na tofauti miongoni mwenu ili wale walio wa kweli waweze kuonekana.
20 Mnapokutana pamoja hamli chakula cha Bwana. 21 Kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anaendelea na chakula chake bila kun goja wengine, na mmoja anabaki na njaa wakati mwingine analewa. 22 Je, hamwezi mkala na kunywa kwenye nyumba zenu? Au mnadharau kanisa la Mungu na kuwafedhehesha wasio na kitu? Niwaambie nini?
Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, sitawasifu!
23 Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale maagizo niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alitwaa mkate, 24 naye akiisha kushukuru , akaumega, akasema, “Huu ndio mwili wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” 25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho wangu.” 26 Maana kila mlapo mkate huu na kunywa katika kikombe hiki, mnatangaza kifo cha Bwana mpaka atakapokuja.
27 Kwa hiyo mtu ye yote anayekula mkate huo au kukinywea kikombe hicho isivyostahili, atakuwa na hatia juu ya mwili na damu ya Bwana. 28 Kila mtu ajichunguze mwenyewe, na ndipo aule mkate na kukinywea kikombe. 29 Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30 Na hii ndio sababu wengi wenu ni wagonjwa na dhaifu, na wengine wamekufa. 31 Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingalihukumiwa. 32 Tunapohukumiwa na Bwana, anaturudi ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. 33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mnapokutana pamoja kula, ngojaneni. 34 Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani ili mnapokutana pamoja msije mkahukumiwa. Na nitakapokuja nitawapa maagizo zaidi.
Copyright © 1989 by Biblica