Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Gen for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Luka 1:39-80

Mariamu Aenda Kumtembelea Elizabeti

39 , 40 Baada ya siku chache, Mariamu aliharakisha kwenda mji mmoja katika milima ya Yudea. Akaingia nyumbani kwa Zakaria akamsalimu Elizabeti. 41 Naye aliposikia salaamu za Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake aliruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42 akasema kwa sauti kubwa: “Umebarikiwa wewe zaidi ya wanawake wengine wote, naye mtoto utakayemzaa amebari kiwa. 43 Sikustahili heshima hii ya kutembelewa na mama wa Bwana wangu! 44 Mara tu niliposikia salaamu zako, mtoto aliyeko tum boni mwangu aliruka kwa furaha. 45 Wewe umebarikiwa kwa kuwa uliamini kwamba Bwana atatimiza yale aliyokuambia.” 46 Mariamu akasema: “Namtukuza Bwana, 47 na roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu. 48 Kwa kuwa ameutambua unyonge wa mtumishi wake. Tangu sasa vizazi vyote wataniita niliyebarikiwa. 49 Kwa maana, yeye Mwenye Uwezo, amenitendea mambo ya ajabu! Jina lake ni taka tifu. 50 Rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwao wamchao. 51 Kwa mkono wake ametenda mambo makuu. Wenye kiburi mioyoni mwao amewatawanya. 52 Amewaangusha wafalme kutoka katika viti vyao vya enzi na kuwainua wanyonge. 53 Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri na matajiri amewafukuza mikono mitupu. 54 Amem saidia mtumishi wake Israeli, akiikumbuka rehema yake, 55 kama alivyowaahidi baba zetu Ibrahimu na uzao wake daima.” 56 Mar iamu akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyum bani kwake.

Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji

57 Ikawa siku za kujifungua kwake Elizabeti zilipotimia, alizaa mtoto wa kiume . 58 Habari zikawafikia majirani na jamaa jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu. Nao wakafurahi pamoja naye. 59 Mtoto alipokuwa na umri wa siku nane, watu wakaja kuhudhuria tohara yake. Wote wakataka wampe yule mtoto jina la Zakaria, yaani jina la baba yake. 60 Lakini mama yake akakataa na kusema, “La si hilo. Jina lake litakuwa Yohana.” 61 Wakamjibu, “Mbona hakuna mtu katika jamaa yako mwenye jina kama hilo?” 62 Basi wakaamua kumwuliza Zakaria kwa ishara kwamba yeye angependa mtoto aitwe nani. 63 Akaomba mahali pa kuandikia, naye akaandika: “Jina lake ni Yohana.” Watu wote wakastaajabu. 64 Papo hapo uwezo wa kusema ukamrudia Zakaria naye akaanza kumsifu Mungu. 65 Watu wote walioshuhudia jambo hili wakastaajabu mno, na habari hii ikaenea sehemu zote za wilaya ile ya Yudea. 66 Na kila aliyezisikia habari hizi aliwaza moyoni: “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.

Utabiri Wa Zakaria

67 Zakaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akata biri akisema: 68 “Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa kuwa amewajia watu wake ili awakomboe. 69 Naye ametusimamishia nguvu ya wokovu katika ukoo wa Daudi mtumishi wake; 70 kama alivy oahidi kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani: 71 kwamba atatuokoa na maadui zetu na kututoa kutoka katika mikono ya wote watuchukiao. 72 Aliahidi ataonyesha rehema kwa baba zetu na kukumbuka agano lake takatifu 73 aliloagana na baba yetu Ibrahimu: 74 kutuokoa kutoka katika mikono ya adui zetu na kutuwezesha kumtumikia pasipo woga, 75 katika utakatifu na haki mbele zake, siku zetu zote. 76 Na wewe mwanangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu, kwa kuwa utamtangulia Bwana na kumwandalia njia; 77 na kuwafahamisha watu wake juu ya wokovu utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao, 78 kwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu. Nuru ya jua itatujia kutoka mbinguni na 79 kuwaangazia wote waishio katika giza na katika uvuli wa mauti na kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.” 80 Yule mtoto akakua na kuko maa kiroho; akaishi nyikani hadi alipoanza kuwahubiria Waisraeli hadharani.

Error: Book name not found: Job for the version: Neno: Bibilia Takatifu
1 Wakorintho 2

Ujumbe Wa Msalaba

Nilipokuja kwenu ndugu zangu, sikuja kuhubiri siri ya mpango wa Mungu kwa kutumia ufasaha wa kuzungumza au hekima ya binadamu.

Kwa kuwa niliamua kwamba wakati nikiwa nanyi nitasahau kila kitu isipokuwa Yesu Kristo; Kristo aliyesulubiwa msalabani. Nilikuja kwenu nikiwa mdhaifu, mwenye woga na nikitetemeka sana. Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa na hekima na maneno ya kuwashawishi watu, bali ujumbe wangu ulidhihirisha wazi nguvu za Roho, ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali ijengwe katika nguvu ya Mungu.

Hekima Ya Mungu

Lakini miongoni mwa watu waliokua kiroho, tunafundisha maneno ya hekima, hii si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa nyakati hizi ambao watatoweka. Hekima tunayofundisha ni hekima ya siri ya Mungu ambayo imefichwa kwa wanadamu, na ambayo Mungu aliipanga kabla ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. Watawala wa nyakati zetu hawakuielewa hekima hii. Kwa maana kama wangeliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa Utukufu.

Lakini, kama Maandiko yasemavyo, “Hakuna aliyeona, hakuna aliyesikia, hakuna aliyewaza, kile ambacho Mungu amekiandaa kwa ajili ya watu wampendao.” 10 Lakini Mungu amekidhihirisha kwetu kwa njia ya Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu. 11 Kwa maana ni nani anajua mawazo ya mtu isipo kuwa roho aliye ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu anayeelewa mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. 12 Sisi hat ukupokea roho ya dunia hii bali Roho aliyetoka kwa Mungu ili tuweze kuelewa yale ambayo Mungu ametupatia bure. 13 Haya ndio tunayozungumzia, lakini si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, nasi tunafa fanua mambo ya kiroho kwa watu wa kiroho. 14 Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yanayotoka kwa Roho wa Mungu kwa sababu mambo hayo ni upuuzi kwake; na hawezi kuyaelewa kwa kuwa hayo yanaeleweka tu kwa msaada wa Roho.

15 Mtu wa kiroho anao uwezo wa kupima kila kitu, lakini yeye hapimwi na mtu. 16 “Kwa maana ni nani amefahamu mawazo ya Bwana ili apate kumshauri?” Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica