M’Cheyne Bible Reading Plan
1 1 0Wakati alipokuwa akifukiza uvumba umati mkubwa wa watu walikuwa nje wakiomba. 2 wakitumia maelezo ya wale wal ioshuhudia mambo haya kwa macho yao na wale waliotabiri habari hizo. 3 Lakini, mimi pia, nimezichunguza habari hizi kuanzia mwanzo. Nami nimeona ni vema nikuandikie kwa mpango, muhtasari huu, 4 ili upate kuwa na hakika ya mambo yote uliyofundishwa.
Utabiri Kuhusu Yohana Mbatizaji
5 Historia ya mambo haya ilianzia katika jamaa ya kuhani mmoja Myahudi aliyeitwa Zakaria. Yeye aliishi wakati Herode ali pokuwa mfalme wa Yudea na alihudumu katika kikundi cha ukuhani cha Abia. Mkewe Zakaria aliitwa Elizabeti naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni. 6 Zakaria na Elizabeti walikuwa watu wenye kumcha Mungu, wakitii amri zake zote na kutimiza maagizo yake yote kika milifu. 7 Lakini hawakuwa na watoto, maana Elizabeti alikuwa tasa; na wote wawili walishapita umri wa kuzaa. 8-9 Siku moja, kikundi cha Zakaria kilikuwa na zamu Hekaluni na Zakaria alikuwa anafanya huduma yake ya ukuhani kwa Mungu. Walipopiga kura, kama ilivyokuwa desturi, ili wamchague atakayeingia kufukiza uvumba madhabahuni, Zakaria alichaguliwa. 11 Ghafla, malaika wa Bwana akamtokea Zakaria. Akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia uvumba. 12 Zakaria alipomwona huyo mal aika alishtuka akajawa na hofu.
13 Lakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zakaria! Kwa maana Mungu amesikia maombi yako, na mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yohana. 14 Nawe utakuwa na furaha kubwa moyoni wakati huo na watu wengi watashangilia kuzaliwa kwake. 15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana, hataonja divai wala kinywaji cho chote cha kulevya; atajazwa Roho Mtakatifu hata kabla ya kuzaliwa kwake. 16 Naye atawavuta Wayahudi wengi warudi kwa Bwana, Mungu wao. 17 Yeye atamtangulia Bwana akiongozwa na Roho na nguvu ya nabii Eliya. Atawapatanisha akina baba na watoto wao. Atawarejesha waasi katika njia ya wenye haki na kuandaa watu wa Bwana kwa ajili ya kuja kwake.” 18 Zakaria akamwambia mal aika, “Jambo hilo linawezekanaje? Mimi ni mzee na mke wangu pia ana umri mkubwa!” 19 Malaika akamjibu, akamwambia, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu. Yeye ndiye aliyenituma kwako nikuambie habari hizi njema. 20 Sikiliza! Kwa sababu huku niamini, utakuwa bubu, hutaweza kusema mpaka maneno yangu yataka pothibitishwa wakati mtoto huyo atakapozaliwa.” 21 Wakati mambo haya yakitokea mle Hekaluni, watu waliokuwa nje wakimngojea Zakaria walikuwa wakishangaa kwa nini alikawia kutoka. 22 Hati maye alipotoka hakuweza kusema nao. Wakatambua ya kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Kwa kuwa alikuwa bubu, akawaashiria kwa mikono. 23 Muda wake wa zamu Hekaluni ulipomalizika, akarudi nyumbani kwake. 24 Kisha baada ya muda si mrefu, Elizabeti mkewe alipata mimba, naye akajificha kwa miezi mitano akisema: 25 “Bwana amekuwa mwema kwangu. Maana ameniondolea aibu yangu mbele za watu.”
Kuzaliwa Kwa Yesu Kwatabiriwa
26 Miezi sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alim tuma malaika Gabrieli aende katika mji wa Nazareti, ulioko Gali laya, 27 kwa msichana bikira aliyeitwa Mariamu. Yeye alikuwa ameposwa na mtu mmoja aliyeitwa Yusufu, wa ukoo wa Mfalme Daudi.
28 Malaika Gabrieli alimtokea Mariamu, akamwambia: “Sal aamu, ewe binti uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”
29 Mariamu alifadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, maana ya salamu hizi ni nini. 30 Ndipo malaika akamwam bia, “Usiogope, Mariamu, Mungu amependezwa nawe. 31 Sikiliza, utapata mimba, nawe utazaa mtoto wa kiume; na utamwita jina lake Yesu. 32 Mtoto huyo atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu. Na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Mfalme Daudi, baba yake. 33 Atatawala juu ya nyumba ya Yakobo daima; na ufalme wake hau takuwa na mwisho!”
34 Mariamu akamwuliza malaika, “Lakini, nitapataje mimba, na mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu ata kujilia na nguvu za Mungu zitakufunika kama kivuli, na kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu na ataitwa Mwana wa Mungu. 36 Tena, miezi sita iliyopita binamu yako Elizabeti, aliyeitwa tasa, amepata mimba ingawa ni mzee sana. 37 Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilo wezekana.”
38 Mariamu akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema.’ ’ Kisha malaika akaondoka.
1 Kutoka kwa Paulo, aliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Yesu Kristo, na Sosthene ndugu yetu.
2 Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wote waliota kaswa katika Kristo Yesu, wakaitwa wawe watakatifu, pamoja na wengine wote ambao kila mahali wanalikiri jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wao na Bwana wetu. 3 Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Baraka Zitokazo Kwa Kristo
4 Ninamshukuru Mungu wakati wote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema aliyowapa ndani ya Kristo Yesu. 5 Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kunena kwenu, katika maarifa yote, 6 kama ushuhuda wetu kumhusu Yesu ulivyothibitishwa ndani yenu. 7 Kwa hiyo hamjapungukiwa na karama yo yote ya kiroho wakati mnangoja kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 8 Yeye atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita muwe na ushirika na Mwanae, Yesu Kristo, Bwana wetu.
Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa
10 Nawasihi ndugu zangu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane ninyi kwa ninyi, na pasiwepo na utengano kati yenu. Muungane pamoja kikamilifu katika kuwaza na katika kuamua. 11 Kwa maana ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa watu wa nyumbani kwa Kloe kwamba kuna ugomvi kati yenu. 12 Maana yangu ni kwamba: mmoja wenu anasema, “Mimi ni wa Paulo,” mwin gine, “Mimi ni wa Apolo,” mwingine, “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine, “Mimi ni wa Kristo.”
13 Je, Kristo amegawanyika? Je, ni Paulo aliyewafia msala bani? Au mlibatizwa kwa jina la Paulo? 14 Namshukuru Mungu kwa sababu sikumbatiza mtu ye yote isipokuwa Krispo na Gayo. 15 Kwa hiyo hakuna mtu kati yenu anayeweza kusema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 16 Ndiyo nakumbuka, pia niliwabatiza Stefano na watu wa nyumbani kwake. Lakini zaidi ya hao sikumbuki kama nilimbatiza mtu mwingine. 17 Kwa maana Kristo hakunituma kubatiza bali kuhu biri Injili na nifanye hivyo pasipo kutumia maneno ya hekima ya kibinadamu, ili nguvu ya kifo cha Kristo msalabani iwe dhahiri.
Kristo Ni Hekima Na Nguvu Ya Mungu
18 Kwa maana ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa watu wanaopo tea. Lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19 Maan diko yanasema, “Nitaharibu hekima ya watu wenye hekima na kuzi kataa akili za wenye akili.” 20 Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi bingwa wa mjadala wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa ni ujinga? 21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, wanadamu hawakuweza kumjua Mungu kwa kutumia hekima yao; badala yake, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wote waaminio kwa upuuzi wa lile neno linalohubiriwa. 22 Way ahudi wanataka ishara, Wagiriki wanatafuta hekima. 23 Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa msalabani, ujumbe ambao ni kikwazo kwa Wayahudi, na kwa Wagiriki ni upuuzi. 24 Lakini kwa walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu. 25 Kwa maana huu ‘ujinga’ wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
26 Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa Mungu alipowaita. Si wengi mlikuwa na hekima kwa kipimo cha kibinadamu. Si wengi mli kuwa na vyeo na si wengi mlikuwa wa jamaa za kifahari. 27 Lakini Mungu alichagua vitu ambavyo huhesabiwa kuwa vya kijinga ulimwen guni ili awaaibishe wenye hekima; Mungu alichagua vitu vidhaifu vya ulimwengu huu ili awaaibishe wenye nguvu. 28 Mungu alichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa humu duniani, vitu ambavyo si kitu, ili avibatilishe vile ambavyo vinaonekana kuwa vya maana; 29 ili mtu ye yote asijisifu mbele yake. 30 Mungu ndiye chanzo cha uhai wenu ndani ya Kristo Yesu. Amemfanya yeye kuwa hekima yetu, haki yetu na utakaso na ukombozi 31 Kwa hiyo, kama Maan diko yasemavyo: “Mtu ye yote anayetaka kujisifu, basi ajisifu kwa ajili ya Bwana.”
Copyright © 1989 by Biblica