M’Cheyne Bible Reading Plan
15 Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya mkutano pamoja na wazee na walimu wa sheria, na Baraza zima likafanya mashauri. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. 2 Pilato akamwuliza, “Wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe ndiye uliyesema maneno hayo.” 3 Makuhani wakuu wakamsh taki kwa mambo mengi. 4 Pilato akamwuliza tena, “Huna la kujibu?
Unasikia mashtaka yao!”
5 Yesu hakusema neno. Pilato akashangaa.
Yesu Ahukumiwa Kifo
6 Ilikuwa desturi wakati wa sherehe za Pasaka kumfungulia mfungwa ye yote ambaye watu walimtaka . 7 Wakati huo, mtu mmoja aitwaye Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na wahalifu wen gine kwa makosa ya kusababisha uasi ambapo mauaji yalitokea. 8 Basi watu waliokusanyika walimjia Pilato wakamwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi wakati wa Pasaka. 9 Pilato akawauliza, “Mnataka nimfungue huyu mfalme wa Wayahudi?” 10 Alikuwa ana fahamu kwamba wakuu wa makuhani walikuwa wanamwonea Yesu wivu ndio sababu wakamshtaki kwake. 11 Lakini makuhani wakuu wakawa chochea watu wamwombe awafungulie Baraba.
12 Pilato akawauliza tena watu, “Nimfanye nini huyu mtu mnayemwita mfalme wa Wayahudi?” 13 Wakapiga kelele, “Msulub ishe!” 14 Akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, “Msulubishe!”
15 Pilato alitaka kuwaridhisha watu, kwa hiyo akamfungulia Baraba; na baada ya kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa asulub ishwe.
Maaskari Wamdhihaki Yesu
16 Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17 Wakamvika Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika. 18 Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!” 19 Wakampiga kwa fimbo kichwani, wakamte mea mate. Wakamdhihaki kwa kupiga magoti kama vile wanamheshimu mfalme. 20 Walipokwisha kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake. Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe.
Yesu Asulubishwa
21 Walipokuwa wakienda kumsulubisha, njiani walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, raia wa Kirene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufas. Alikuwa anakuja mjini kutoka shamba. Wakamla zimisha abebe msalaba wa Yesu. 22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, -yaani Mahali pa Fuvu la Kichwa.
23 Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini akaikataa. 24 Basi wakamsulubisha, wakagawana nguo zake kwa kuzipigia kura kuamua kila mtu achukue nini.
25 Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26 Tangazo la mashtaka yake liliandikwa maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.” 27 Majambazi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wa kushoto. [ 28 Na kwa njia hii yale Maandiko yasemayo, “Alihesabiwa pamoja na wenye hatia,” yalitimia.] 29 Watu waliokuwa wakipita, walimtukana na kutikisa vichwa vyao kwa mzaha wakasema, “Si ulikuwa ukisema kwamba unaweza kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? 30 Shuka msalabani basi, ujiokoe mwenyewe!” 31 Hali kadhalika makuhani wakuu na walimu wa sheria walimdhihaki wakisema, “Ali waokoa wengine lakini anashindwa kujiokoa mwenyewe. 32 Kristo mfalme wa Wayahudi ashuke basi msalabani ili tupate kuona na kuamini!” Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia walimtukana.
Kifo Cha Yesu Msalabani
33 Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu. 34 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” 35 Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, “Mnamsikia? Anamwita
Eliya!”
36 Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!”
37 Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.
39 Yule askari aliyekuwa amesimama mbele ya msalaba alipoona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
40 Walikuwapo pia wanawake walio kuwa wakiangalia mambo haya kwa mbali. Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na pia Salome . 41 Hawa walifuatana na Yesu alipokuwa Galilaya na kumhudumia. Pia walikuwapo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja naye Yerusalemu.
Mazishi Ya Yesu
42 Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi, siku moja kabla ya Pasaka, 43 Yusufu wa Arimathea alijikaza akamwendea Pilato akamwomba auchukue mwili wa Yesu. Yeye alikuwa ni mjumbe wa Baraza aliyeheshimika, ambaye alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. 44 Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu amekwisha kufa. Kwa hiyo akamwita askari amhakikishie kuwa kweli amekufa. 45 Baada ya kuhakikishiwa na yule askari kwamba kweli amekufa, Pilato alimpa Yusufu ruhusa ya kuuchukua mwili wa Yesu. 46 Basi Yusufu alinunua sanda ya kitani, akautoa mwili wa Yesu msalabani; akamzungushia sanda, akamweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe akaufunika mlango wa kaburi. 47 Mariamu Magdalena na Mariamu mama wa Yose walipaona mahali alipozikwa Yesu.
15 Sisi tulio imara katika imani, hatuna budi kuchukuliana na udhaifu wa wale ambao si imara. Tusitafute kujipendeza wenyewe. 2 Kila mmoja wetu anapaswa kumpendeza jirani yake ili kumjenga katika imani. 3 Kwa maana hata Kristo hakujipendeza mwenyewe bali alikuwa kama ilivyoandikwa: “Matusi yote waliyoku tukana wewe yalinipata mimi.” 4 Kwa maana mambo hayo yaliyoan dikwa zamani, yaliandikwa kutufundisha, ili tukiwa na subira na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini. 5 Na Mungu aliye chanzo cha subira na faraja awajalie ninyi moyo wa umoja miongoni mwenu mnapomfuata Kristo Yesu, 6 ili kwa pamoja na kwa sauti moja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Kuhusu Umoja
7 Mpokeane ninyi kwa ninyi kama Kristo alivyowapokea, ili Mungu apate kutukuzwa. 8 Maana nawaambia kwamba, Kristo alikuwa mtumishi kwa Waisraeli ili kuonyesha kuwa Mungu ni mwaminifu,na kuthibitisha ahadi alizowapa baba zetu. 9 Na pia ili watu wa mataifa mengine wamtukuze Mungu kwa huruma yake. Kama yasemavyo Maandiko: “Kwa sababu hii nitakutukuza kati ya watu wa mataifa, nitaimba nyimbo za kulisifu jina lako.” 10 Na tena yanasema, “Ninyi watu wa mataifa, furahini pamoja na watu wa Mungu.” 11 Na tena: “Msifuni Bwana enyi watu wote wa mataifa, watu wote wamsifu.” 12 Na tena Isaya anasema:“Shina la Yese lita chipuka, atatoka huko atakayetawala mataifa yote; na watu wa ma taifa watamtumaini.”
13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha na amani katika kumwamini, ili kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, mpate kuwa na tumaini tele.
Huduma Ya Paulo Kwa Mataifa
14 Mimi nimeridhika ndugu zangu kuwa ninyi mmejaa wema, mnao ufahamu wote, tena mnaweza kujengana. 15 Lakini kuhusu mambo fulani nimewaandikia kwa ujasiri nikiwa na shabaha ya kuwa kumbusha kwa sababu Mungu amenipa neema maalumu. 16 Amenichagua kuwa mtumishi wa Kristo Yesu kwa watu wa mataifa wasiomjua Mungu, nitoe huduma ya kikuhani kwa kuitangaza Injili ya Mungu, ili watu wa mataifa wawe sadaka inayokubaliwa na Mungu na iliy otakaswa na Roho Mtakatifu.
17 Kwa hiyo nina sababu ya kujisifu ndani ya Kristo kwa huduma yangu kwa Mungu. 18 Hata sitasema juu ya jambo lo lote isipokuwa katika yale tu ambayo Kristo mwenyewe ameyafanikisha kwa kunitumia, katika maneno na matendo yangu, akawavuta watu wa mataifa wamtii akitumia 19 nguvu za ishara na miujiza, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo kuanzia Yerusalemu mpaka kando kando ya Iliriko nimekwisha kuhubiri Injili ya Kristo kwa ukamilifu. 20 Shabaha yangu imekuwa nisihubiri mahali ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwin gine. 21 Lakini kama ilivyoandikwa, “Wale ambao hawajaambiwa habari zake, wataona na wale ambao hawajasikia wataelewa.”
Paulo Apanga Kwenda Roma
22 Hii ndio sababu nimezuiliwa mara nyingi nisiweze kuja kwenu.
23 Lakini maadamu sasa nimemaliza kazi yangu pande hizi, na kwa kuwa kwa miaka mingi nimetamani sana kuja kwenu, 24 natu maini kuwaona nikiwa safarini kwenda Spania, nifurahi kwa muda pamoja nanyi, kisha mnipatie msaada kwa safari hiyo. 25 Ila sasa nakwenda kupeleka msaada kwa watu wa Mungu walioko Yerusalemu. 26 Maana makanisa ya Makedonia na Akaya yameamua kutoa mchango wao kuwasaidia watu wa Mungu wasiojiweza walioko huko Yerusalemu. 27 Wamependa kufanya hivyo lakini kwa kweli ni wajibu wao, maana kama watu wa mataifa mengine wameshiriki katika baraka za kiroho za Waisraeli, wanawajibika kuwahudumia Waisraeli katika mahitaji yao ya kimwili. 28 Kwa hiyo baada ya kukamilisha kazi hii na kuhakikisha kuwa wamepokea kila kitu kilichokusanywa, nitakwenda Spania kupitia kwenu. 29 Ninafahamu kwamba nitakapokuja kwenu, nitawaletea wingi wa baraka za Kristo.
30 Basi, ndugu zangu, nawasihi kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kwa ajili ya upendo uletwao na Roho, muwe pamoja nami mkiniombea kwa Mungu. 31 Ombeni niepushwe na wale wasioamini walioko Uyahudi, na kwamba huduma yangu huko Yerusalemu ipate kukubaliwa na watu wa Mungu; 32 ili kwa mapenzi ya Mungu niweze kuja kwenu kwa furaha, niburudishwe pamoja nanyi. 33 Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.
Copyright © 1989 by Biblica