M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Anatabiri Kubomolewa Kwa Hekalu
13 Alipokuwa akitoka nje ya Hekalu, mmojawapo wa wanafunzi wake akamwambia, “Mwalimu, ona jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo maridadi!”
2 Yesu akamjibu, “Unayaona majengo haya yalivyo makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalobaki juu ya jingine, yote yatabomo lewa.”
Yesu Anawaambia Wafuasi Wake Wajiandae Kwa Mateso
3 Alipokuwa ameketi kwenye mlima wa Mizeituni akiliangalia Hekalu, Petro, Yakobo na Yohana walimwuliza faraghani, 4 “Tafadhali tuambie, mambo haya yatatokea lini, na ni ishara gani zitaonyesha kuwa karibu yatatimia?” 5 Yesu akaanza kuwaeleza: “Jihadharini mtu asije akawadanganya. 6 Wengi wata kuja wakilitumia jina langu na kusema, ‘Mimi ndiye’ na wata wadanganya wengi. 7 Na mkisikia habari za vita na uvumi juu ya vita, msishtuke. Mambo haya hayana budi kutokea, lakini mwisho utakuwa bado. 8 Mataifa yatapigana na falme kushambuliana. Matetemeko ya ardhi yatatokea sehemu mbalimbali na kutakuwa na njaa. Lakini huu utakuwa kama maumivu ya mwanzo tu ya uchungu wa uzazi. 9 Lakini ninyi jihadharini. Kwa maana watu watawapeleka mahakamani na mtapigwa mijeledi katika masinagogi. Mtashtakiwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ndipo mtaweza kutoa ushuhuda kuhusu Habari Njema. 10 Lakini kabla mwisho kufika, Habari Njema itahubiriwa kwa mataifa yote. 11 “Mtakapokamatwa na kupelekwa mahakamani, msihangaike kuhusu mtakalosema. Semeni lo lote litakalowajia wakati huo, kwa sababu maneno mtakayosema si yenu bali yatatoka kwa Roho Mtaka tifu.
12 “Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae. Watoto watawaasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 13 Kila mtu atawachukia kwa ajili yangu; lakini atakayevumilia mpaka mwisho, ataokolewa.
14 “Mtakapoona ile ‘sanamu ya chukizo’ imesimama mahali isipostahili - msomaji na aelewe maana yake -basi wale walioko Yudea wakimbilie milimani. 15 Mtu aliyeko juu ya nyumba asiter emke kuingia ndani kuchukua cho chote. 16 Aliyeko shambani asi rudi nyumbani kuchukua koti lake. 17 Ole wao akina mama waja wazito na watakaokuwa wakinyonyesha siku hizo! 18 Ombeni mambo haya yasitokee wakati wa masika. 19 Kwa maana siku hizo itaku wapo dhiki kuu ambayo haijapata kutokea tangu dunia ilipoumbwa, wala haitatokea tena. 20 Na kama Bwana hakuufupisha muda huo wa dhiki, hakuna mtu ambaye angesalimika; lakini kwa ajili ya watu wake aliowachagua, ameufupisha muda huo.
21 “Na wakati huo mtu akiwaambia, ‘Tazama, Kristo huyu hapa’ au , ‘Tazama, yule pale,’ msiamini. 22 Kwa maana watatokea makristo wa uongo na manabii wa uongo nao watafanya ishara na miujiza ili kuwadanganya hata wale waliochaguliwa na Mungu, kama ikiwezekana. 23 Kwa hiyo jihadharini kwa maana nimewaambia mambo haya kabla hayajatokea.”
Kuja Kwa Mwana Wa Adamu
24 “Siku hizo, baada ya hiyo dhiki, jua litatiwa giza na mwezi hautatoa mwanga wake. 25 Nyota zitaanguka kutoka mbinguni na nguvu za anga zitatikisika. 26 Ndipo watu wote wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utu kufu. 27 Nami nitawatuma malaika wawakusanye watu wangu kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa nchi hadi mwisho wa mbi ngu.
28 “Sasa jifunzeni jambo hili kutoka kwa mtini: mwonapo matawi ya mtini yakianza kulainika na kutoa majani, mnatambua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. 29 Hali kadhalika mtaka poyaona mambo haya yanatokea, tambueni kwamba mimi Mwana wa Adamu, ni karibu kuja. 30 Ninawaambieni hakika, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo haya kutokea. 31 Mbingu na nchi zita toweka, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.”
Hakuna Ajuaye Siku Wala Saa
32 “Hakuna ajuaye siku hiyo itakuwa lini au saa ngapi; hata malaika mbinguni hawajui wala mimi Mwana sijui, isipokuwa Mungu Baba peke yake. 33 “Jiandaeni, muwe macho. Kwa maana hamjui wakati mambo haya yatakapotokea. 34 Ni kama mtu anayesafiri na kuwaachia wat umishi wake madaraka, kila mtu na wajibu wake; kisha akamwambia mlinzi wa mlango awe macho. 35 Kesheni basi, kwa sababu hamjui ni lini bwana mwenye nyumba atarudi. Anaweza akaja jioni, au usiku wa manane au alfajiri au mapambazuko. 36 Kama akija gha fla, pasipo ninyi kumtazamia, asije awakute mmelala. 37 Na haya ninayowaambia ninyi nawaambia watu wote: Kesheni!”
Kutii Mamlaka
13 Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. 3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. 4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.
6 Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala. 7 Wal ipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.
Upendo Na Sheria
8 Msiwe na deni la mtu ye yote; isipokuwa deni la kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria. 9 Kwa maana amri zisemazo: Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 10 Upendo haumfanyii jirani jambo baya, kwa hiyo upendo unakamilisha sheria zote.
11 Fanyeni hivi mkitambua kuwa sasa tumo katika wakati gani. Huu ni wakati wa kuamka kutoka usingizini, kwa maana wokovu wetu umekaribia zaidi sasa kuliko wakati tulipoamini kwa mara ya kwanza. 12 Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Kwa hiyo tutupe kando matendo ya giza, tuvae silaha za nuru. 13 Tuishi maisha ya heshima kama inavyopasa wakati wamchana: si kwa ulafi na ulevi; si kwa ufisadi na uasherati; si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, na msitoe nafasi kwa miili yenu yenye asili ya dhambi, kutimiza tamaa zake.
Copyright © 1989 by Biblica