M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Alisha Watu Elfu Nne
8 Muda si mrefu baadaye, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia, 2 “Ninawaonea huruma hawa watu. Wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu sasa na hawana chakula. 3 Nikiwaruhusu waende bila kula, watazimia njiani na baadhi yao wametoka mbali.”
4 Wanafunzi wake wakamjibu, “Lakini hapa nyikani tutapata wapi chakula cha kutosha kuwalisha?”
5 Yesu akawauliza, “Mna mikate mingapi?” Wakajibu, “Saba.”
6 Akawaambia watu wakae chini. Kisha akaichukua ile mikate saba na baada ya kushukuru akaimega, akawapa wanafunzi wake wawa gawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. 7 Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. 8 Watu walikula wakatosheka na baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu saba. 9 Na watu waliokula walikuwa wapata elfu nne. Baada ya kuwaaga, 10 aliin gia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake akaenda sehemu za Dal manutha.
11 Mafarisayo wakaja, wakaanza kumhoji Yesu. Ili kumtega, wakamwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 12 Akahuzunika moyoni, akawaambia, “Kwa nini kizazi hiki kinataka ishara? Nawaambieni kweli, hakitapewa ishara yo yote.” 13 Kisha aka waacha, akarudi kwenye mashua, akavuka hadi ng’ambo ya pili.
Chachu Ya Mafarisayo Na Ya Herode
14 Wanafunzi walikuwa wamesahau kuleta mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. 15 Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.”
16 Wakaanza kujadiliana wao kwa wao wakasema,“Anasema hivi kwa kuwa hatukuleta mikate.”
17 Yesu alifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mna zungumzia kuhusu kutokuwa na mikate? Bado hamtambui wala kuelewa? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? 18 Mbona mna macho lakini mnashindwa kuona, na masikio lakini mnashindwa kusikia? Je hamkumbuki? 19 Nilipoimega mikate mitano kuwalisha watu elfu tano, mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.” 20 “Na nilipomega mikate saba kuwalisha watu elfu nne mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Saba.” 21 Aka wauliza, “Je, bado tu hamwelewi?”
Yesu Amponya Kipofu Huko Bethsaida
22 Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta kipofu mmoja wakamsihi Yesu amguse. 23 Yesu akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Yesu akamwuliza, “Unaona cho chote?”
24 Yule kipofu akaangalia, akasema, “Ninaona watu; wanaonekana kama miti ikitembea.”
25 Yesu akamwekea tena mikono machoni. Ndipo akaona vizuri. Macho yake yakapona kabisa akaweza kuona kila kitu sawa sawa.
26 Yesu akamruhusu aende nyumbani kwake akisema, “Hata kijijini usipitie.”
27 Yesu na wanafunzi wake wakaondoka kwenda katika vijiji vya Kaisaria Filipi. Walipokuwa njiani Yesu akawauliza, “Watu husema mimi ni nani?”
28 Wakamjibu, “ Baadhi husema wewe ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya na wengine husema wewe ni mmojawapo wa manabii.”
29 Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani?” Petro akajibu, ‘ ‘Wewe ndiye Kristo.”
30 Akawaonya wasim wambie mtu ye yote habari zake.
Yesu Azungumza Juu Ya Kifo Chake
31 Akaanza kuwafundisha wanafunzi wake kuwa yeye, Mwana wa Adamu, atapata mateso mengi na kukataliwa na wazee, na makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na baada ya siku tatu atafufuka. 32 Aliyasema haya wazi wazi. Ndipo Petro akam chukua kando akaanza kumkemea. 33 Lakini Yesu alipogeuka na kuwatazama wanafunzi wake alimkaripia Petro akamwambia, “Ondoka mbele yangu, shetani! Mawazo yako hayako upande wa Mungu bali upande wa wanadamu.”
34 Ndipo akawaita wale watu pamoja na wanafunzi wake aka waambia, “Mtu ye yote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwe nyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 35 Kwa maana mtu ye yote aipotezaye nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya kuitangaza Habari Njema, ataiokoa. 36 Mtu atafaidi nini kama atapata ulimwengu wote lakini akayaangamiza maisha yake? 37 Au mtu atatoa nini apate tena maisha yake? 38 Mtu ye yote atakayenionea aibu mimi na maneno yangu katika kizazi hiki kiovu na kisichomjali Mungu, na mimi, Mwana wa Adamu, nitamwonea aibu wakati nitakapokuja katika utu kufu wa Baba yangu na malaika watakatifu.”
Maisha Ya Kiroho
8 Kwa hiyo basi, sasa hakuna tena hukumu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu. 2 Kwa maana sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru kutokana na sheria ya dhambi na mauti. 3 Mungu amefanya lile ambalo sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ya udhaifu wa mwili wetu wa asili. Mungu aliihukumu dhambi kwa kumtuma Mwana wake wa pekee katika hali ya mwili kama sisi, ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi. 4 Kwa kufanya hivyo, Mungu ametutimizia matakwa ya haki ya sheria kwa kuwa sasa maisha yetu yanaongozwa na Roho na wala hatuishi tena kwa kufuata mata kwa ya mwili.
5 Kwa maana wale waishio kwa kuongozwa na asili yao ya dhambi, hukaza mawazo yao kwenye mambo ya mwili; bali wale waishio kwa kuongozwa na Roho hukaza mawazo yao katika mambo ya Roho. 6 Matokeo ya mawazo yaliyotawaliwa na tamaa za mwili ni kifo lakini mawazo yaliyotawaliwa na Roho huleta uzima na amani. 7 Watu wenye mawazo yaliyotawaliwa na mambo ya mwili ni adui wa Mungu. Watu kama hao hawakubali kutii sheria ya Mungu, na kwa kweli hawawezi. 8 Watu wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kum pendeza Mungu .
9 Lakini ninyi hamuishi kwa kufuata matakwa ya mwili, bali mnaongozwa na Roho; ikiwa kweli Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. Mtu ye yote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo. 10 Lakini kama Kristo anaishi ndani yenu, ingawa miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, roho zenu zinaishi kwa sababu mmek wisha kuhesabiwa haki. 11 Na ikiwa Roho wa Mungu ambaye alimfu fua Yesu kutoka kwa wafu anaishi ndani yenu, Mungu aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataipatia uzima miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya huyo Roho wake ambaye anaishi ndani yenu. 12 Kwa hiyo ndugu zangu, hatuwajibiki tena kuishi kama miili yetu inavyotaka. 13 Kwa maana mkiishi kama mwili unavyotaka mta kufa,lakini kama mkiangamiza matendo ya mwili kwa nguvu ya Roho, mtaishi.
14 Kwa maana wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu ni wana wa Mungu. 15 Hamkupewa Roho anayewafanya kuwa tena watumwa wa hofu. Lakini mmepokea Roho anayewafanya kuwa wana. Na kwa Roho huyo tunaweza kumwita Mungu, “Abba! Baba!” 16 Ni Roho mwenyewe anayeshuhudia pamoja na roho zetu kwamba sisi ni wana wa Mungu. 17 Na ikiwa sisi ni wana, basi tu warithi. Sisi ni warithi wa Mungu tutakaorithi pamoja na Kristo iwapo tutateseka pamoja naye ili pia tutukuzwe pamoja naye.
Utukufu Ujao
18 Nayahesabu mateso tunayopata sasa kuwa si kitu yakilin ganishwa na utukufu utakaodhihirishwa kwetu. 19 Viumbe vyote vinangoja kwa hamu kudhihirishwa kwa wana wa Mungu. 20 Kwa maana viumbe vilifanywa kuwa duni kabisa, si kwa kupenda kwake, bali kwa mapenzi ya Mungu; hata hivyo kulikuwa na matumaini 21 kwamba siku moja viumbe vyote vitawekwa huru kutoka katika utumwa wa kuharibika na vipewe uhuru na utukufu wa watoto wa Mungu.
22 Tunajua kwamba mpaka sasa viumbe vyote vimekuwa vikilia kwa uchungu mkali kama ule wa uzazi. 23 Na si hivyo tu, hata sisi ambao tuna matunda ya kwanza ya Roho tunalia kwa uchungu tukisu biri kwa hamu kufanywa kuwa wana wa Mungu, miili yetu itakapowek wa huru kabisa.
24 Kwa maana tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alichonacho? 25 Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatunacho, basi tunakingoja kwa subira.
26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno. 27 Na Mungu ambaye ana chunguza mioyo yetu anafahamu mawazo ya Roho kwa maana Roho huwaombea watakatifu kufuatana na mapenzi ya Mungu. 28 Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, wale ambao wameitwa kufuatana na mapenzi yake. Mungu hufanya hivyo kwa faida yao. 29 Wale ambao Mungu alikwisha kuwachagua tangu mwanzo, pia aliwateua wafanane na Mwanae, ili Mwana awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Na wale ambao Mungu aliwateua tangu awali pia ali waita; na wale aliowaita pia aliwahesabia haki; na wale aliowahesabia haki aliwapa utukufu wake.
Upendo Wa Mungu
31 Tuseme nini basi kuhusu haya yote? Ikiwa Mungu yuko upande wetu ni nani atakayetupinga? 32 Ikiwa Mungu hakumwacha Mwanae bali alimtoa kwa ajili yetu sote, hatatupatia pamoja na Mwanae, vitu vyote? 33 Ni nani atawashtaki wale ambao Mungu amewachagua? Ni Mungu mwenyewe ambaye anawahesabia kuwa hawana hatia. 34 Ni nani basi atakayewahukumu? Yesu Kristo mwenyewe ndiye aliyekufa, na zaidi ya hayo, yeye ndiye aliyefufuliwa akawa hai, na ambaye sasa amekaa upande wa kulia wa Mungu, naye anatuombea. 35 Ni nani atakayetutenganisha na upendo wa Kristo? Ni shida? Au taabu? Au mateso? Au njaa? Au umaskini? Au hatari? Au Kifo? Hapana. 36 Kama Maandiko yasemavyo: “Kwa aji li yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.” 37 Lakini katika mambo yote haya sisi ni washi ndi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye aliyetu penda. 38 Kwa maana nina hakika kuwa, si kifo wala uzima; si malaika wala mashetani; si mambo ya sasa wala mambo yajayo au mamlaka nyingineyo yote; 39 si mambo yaliyo juu wala yaliyo chi ni sana; wala hakuna kitu kingine cho chote kati ya vitu vyote alivyoumba Mungu kitakachoweza kututenga na upendo wa Mungu ulio ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu.
Copyright © 1989 by Biblica