Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Gen for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Marko 2

Yesu Amponya Mtu Aliyepooza

Baada ya siku kadhaa Yesu alirudi Kapernaumu; watu waka pata habari kuwa amerudi nyumbani. Wakakusanyika kwa wingi isibaki nafasi hata mlangoni! Naye akawahubiria. Wakaja watu wanamletea Yesu mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. Waliposhindwa kumfikia Yesu kwa ajili ya msongamano wa watu, wakatoboa tundu darini, wakamshusha ndani yule aliyepooza kwa kitanda alichokuwa amelalia.

Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mgonjwa, “Mwa nangu, dhambi zako zimesamehewa.” Baadhi ya walimu wa sheria waliokuwepo wakawaza mioyoni mwao, “Mbona mtu huyu anasema maneno haya? Anakufuru! Hajui kuwa ni Mungu peke yake awezaye kusamehe dhambi?”

Yesu akatambua mawazo yao, kwa hiyo akawaambia, “Kwa nini mnawaza hivyo? Ni jambo gani lililo rahisi zaidi, kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’? Au, ‘Inuka, chukua kitanda chako uende’? 10 Lakini ili kuwahakikishia kwamba mimi Mwana wa Adamu ninao uwezo hapa duniani wa kusamehe dhambi,” - akamwambia yule aliyepooza 11 “Nakuambia, inuka, chukua kitanda chako uende nyumbani.”

12 Yule mtu aliyekuwa amepooza akainuka, akachukua kitanda chake akatembea mbele yao wote! Tukio hili likawashangaza watu wote, wakamsifu Mungu, wakasema, “Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!”

Yesu Amwita Mathayo

13 Yesu akaenda tena kando kando ya Ziwa la Galilaya. Umati wa watu ukamfuata naye akaanza kuwafundisha. 14 Alipokuwa aki tembea, akamwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi katika kibanda cha kukusanyia kodi, akamwambia, “Nifuate”. Lawi akatoka, akamfuata Yesu. 15 Yesu alipokuwa akila chakula nyumbani kwa Lawi, watoza ushuru wengi pamoja na wenye dhambi walikuwa wameketi mezani pamoja naye na wanafunzi wake; kwa maana watu wengi wa aina hii walikuwa wamemfuata. 16 Baadhi ya walimu wa sheria ambao wali kuwa Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, wakawauliza wanafunzi wake, “Yesu anawezaje kula na watoza ushuru na wenye dhambi?” 17 Yesu aliposikia haya aka waambia, “Wenye afya nzuri hawahitaji daktari, bali wagonjwa wanamhitaji. Sikuja kuwaalika wenye haki, bali wenye dhambi.”

Yesu Afundisha Kuhusu Kufunga

18 Wakati mmoja wanafunzi wa Yohana pamoja na Mafarisayo walikuwa wamefunga. Baadhi ya watu wakaja kwa Yesu wakamwuliza, “Mbona wanafunzi wa Yohana na wa Mafarisayo hufunga na wako hawafungi?”

19 Yesu akawajibu, “Inawezekanaje wageni wa bwana harusi wafunge wakati bwana harusi yungali nao? Maadamu bwana harusi yupo, haiwezekani wafunge. 20 Lakini wakati utafika ambapo bwana harusi atachukuliwa. Siku hiyo ndipo watakapofunga.

21 “Hakuna mtu anayeshonea kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, ile nguo iliyochakaa itachanika zaidi pale penye kiraka kipya na kuharibika zaidi. 22 Wala hakuna mtu anayeweka divai mpya katika viriba vya zamani. Akifa nya hivyo, ile divai mpya itavipasua hivyo viriba, kwa hiyo ata poteza divai na viriba pia. Divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya.”

Yesu Afundisha Kuhusu Sabato

23 Siku moja ya sabato, Yesu pamoja na wanafunzi wake, wal ikuwa wakipita katikati ya mashamba ya ngano. Wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya ngano. 24 Mafarisayo wakamwambia, “Mbona wanafanya jambo ambalo si halali kufanywa siku ya sabato?”

25 Yesu akawaambia, “Hamjasoma alivyofanya Daudi wakati yeye na wafuasi wake walipokuwa na njaa? 26 Aliingia katika nyumba ya Mungu wakati Abiatha akiwa kuhani mkuu, akala mkate wa sadaka walioruhusiwa kuula ni makuhani peke yao - na akawagawia wafuasi wake.” 27 Kisha akawaambia, “Sabato iliwekwa kwa faida ya mwanadamu, lakini mwanadamu hakuwekwa kwa ajili ya sabato. 28 Na mimi, Mwana wa Adamu, ni Bwana hata wa sabato.”

Error: Book name not found: Esth for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Warumi 2

Hukumu Ya Mungu

Kwa hiyo huna udhuru wo wote, hata ukiwa nani, unapowahu kumu wengine. Kwa maana unapowahukumu wengine unajihukumu mwe nyewe, kwa kuwa wewe uliye hakimu unafanya mambo hayo hayo. Tunajua kwamba hukumu ya Mungu huwafikia kwa halali wote wanaotenda mambo haya. Je, wewe uliye binadamu tu, unapowahuku mu watu wanaofanya mambo hayo na huku wewe mwenyewe pia unafanya hayo hayo, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? Au labda unad harau wingi wa huruma, uvumilivu na subira ya Mungu, ukasahau kwamba wema wake una shabaha ya kukufanya utubu?

Lakini kwa sababu ya ugumu na ukaidi wa moyo wako usioku bali kutubu, unajiwekea ghadhabu kwa siku ile ambapo ghadhabu ya Mungu na hukumu yake ya haki itadhihirishwa. Siku hiyo, Mungu atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake. Wale ambao hutenda wema wakati wote na kutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyo haribika, Mungu atawapa uzima wa milele. Lakini wote watafu tao kujinufaisha, wanaokataa kweli na kufuatauovu, watapokea ghadhabu na hasira ya Mungu. Kwa maana kila binadamu atendaye uovu atapata mateso na shida, kuanzia kwa Myahudi na kisha kwa mtu wa mataifa mengine. 10 Lakini Mungu atawapa utukufu, heshima na amani wote watendao mema; Wayahudi kwanza na kisha watu wa mataifa mengine. 11 Kwa maana Mungu hana upendeleo.

12 Watu wote waliotenda dhambi pasipokuwa na sheria ya Musa wataangamia pasipo sheria; na wale wote waliotenda dhambi chini ya sheria ya Musa watahukumiwa kwa sheria iyo hiyo. 13 Kwa maana wanaohesabiwa haki mbele ya Mungu si wale wanaosikia bali ni wal ewanaotii maagizo ya sheria. 14 Watu wa mataifa mengine ambao hawana sheria ya Musa, wanapoamua kutenda yale ambayo yameagizwa na sheria kwa kuongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa wamejiwekea sheria, ingawa hawana sheria ya Musa. 15 Kwa jinsi hii matendo yao yanaonyesha kwamba yale yaliyoagizwa katika she ria ya Musa yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia hush uhudia hivyo; kwa maana mawazo yao mara nyingine huwashtaki na mara nyingine huwatetea. 16 Kwa hiyo, kama Habari Njema ninay ohubiri inavyosema, hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile ambayo Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo, atayahukumu mawazo ya siri ya wanadamu.

Wayahudi Na Sheria Ya Musa

17 Na wewe je? Wewe unayejiita Myahudi: unaitegemea sheria ya Musa na kujisifia uhusiano wako na Mungu; 18 unajua mapenzi ya Mungu na unatambua lililo bora kutokana na hiyo sheria. 19 Kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu na mwanga kwa wale walioko gizani; 20 mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa watoto wachanga, kwa kuwa una hakika kwamba ndani ya hiyo sheria mna maarifa na kweli yote: 21 wewe unayewafundisha wengine, mbona hujifunzi mwenyewe? Wewe unayehubiri kwamba watu wasiibe, wewe huibi? 22 Wewe unayewaambia watu wasizini, wewe huzini? Wewe uchukiaye miungu ya sanamu, huibi katika mahekalu? 23 Wewe unayejisifia sheria, humwaibishi Mungu kwa kuvunja sheria? 24 Kwa maana Maandiko yanasema, “Kwa ajili yenu ninyi Wayahudi, jina la Mungu linatukanwa miongoni mwa mataifa ya watu wasiom jua Mungu.”

25 Kutahiriwa kuna thamani tu iwapo unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, umekuwa kama hukutahiriwa. 26 Kwa hiyo kama watu ambao hawakutahiriwa wanatimiza maagizo ya she ria, je, Mungu hatawahesabu kuwa kama waliotahiriwa? 27 Ndipo wale ambao kimwili hawakutahiriwa lakini wanatii sheria watawa hukumu ninyi mlio na Maandiko ya sheria nakutahiriwa lakini mna vunja sheria. 28 Kwamaana Myahudi wa kweli si yule anayeonekana kwa dalili za nje, wala tohara ya kweli si kitu cha kimwili. 29 Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ya kweli ni jambo la moyoni, jambo la kiroho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa jinsi hii anapata sifa kutoka kwa Mungu, wala si kutoka kwa wanadamu.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica