Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

M’Cheyne Bible Reading Plan

The classic M'Cheyne plan--read the Old Testament, New Testament, and Psalms or Gospels every day.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Gen for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matayo 27

Yesu Apelekwa Kwa Pilato

27 Asubuhi na mapema, makuhani wakuu wote na wazee walifanya mkutano, wakashauriana jinsi ya kumwua. Wakamfunga, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato ambaye alikuwa gavana.

Majuto Ya Yuda

Yuda, ambaye alimsaliti Yesu, alipoona kuwa Yesu amehuku miwa alijuta. Akazirudisha zile fedha alizopewa kwa makuhani wakuu na wazee akawaambia, “Nimetenda dhambi kwa maana nimem saliti mtu asiye na hatia.” Wakamjibu, “Hilo latuhusu nini sisi? Ni shauri yako.”

Basi Yuda akazitupa zile fedha Hekaluni, akaondoka; akaenda akajinyonga.

Wale makuhani wakuu wakazichukua zile fedha wakasema, “Si halali kuchanganya fedha hizi na sadaka kwa sababu hizi ni fedha zenye damu.” Kwa hiyo baada ya kujadiliana waliamua kuzitumia kununua shamba la mfinyanzi, liwe mahali pa kuzikia wageni. Kwa hiyo shamba hili limeitwa ‘Shamba la damu’ hadi leo. Ndipo yakatimia yale aliyonena nabii Yeremia kwamba, “Walichukua vile vipande thelathini vya fedha, thamani aliyopangiwa na wana wa Israeli, 10 wakanunulia shamba la mfinyanzi kama Bwana alivyon iagiza.”

Yesu Mbele Ya Pilato

11 Yesu akapelekwa mbele ya gavana naye akamwuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Hayo umetamka wewe.” 12 Lakini makuhani wakuu na wazee walipomshtaki kwa mambo mengi hakujibu neno. 13 Ndipo Pilato akamwuliza, “Husikii mambo hayo yote wanayokushtaki nayo?” 14 Lakini Yesu hakujibu neno hata kwa shtaka moja. Gavana akashangaa sana.

15 Kila wakati wa sikukuu, gavana alikuwa na desturi ya kum fungua mfungwa mmoja atakayechaguliwa na watu. 16 Wakati huo alikuwapo mfungwa mmoja mwenye kujulikana sana, aliyeitwa Baraba. 17 Basi watu walipokusanyika, Pilato akawauliza, “Mnataka niwa fungulie nani; Baraba au Yesu aitwaye Kristo?” 18 Kwa sababu alijua kuwa Yesu aliletwa kwake kwa ajili ya wivu wa viongozi wa Wayahudi. 19 Alipokuwa ameketi kwenye kiti cha hukumu, mke wake alimpelekea ujumbe, “Usijihusishe katika kesi ya huyu mtu asiye na hatia. Leo nimehangaika sana katika ndoto kwa ajili yake.”

20 Basi makuhani na wazee wakawashawishi umati wa watu kwamba waombe Baraba afunguliwe na Yesu auawe. 21 Gavana akawau liza tena , “Ni yupi mnataka niwafungulie?” Wakajibu, “Bar aba!” 22 “Sasa nifanye nini na huyu Yesu aitwaye Kristo?” Wakajibu wote , “Asulubiwe!” 23 Akasema, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupiga kelele, “Asulubiwe.”

24 Pilato alipoona kwamba hakuna zaidi ambalo angeweza kufa nya na kwamba ghasia ilikuwa ikianza, akachukua maji, akanawa mikono mbele yao, akasema, “Sina hatia na damu ya mtu huyu. Jambo hili ni juu yenu.”

Jambo hili ni juu yenu.”

25 Watu wote wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu na juu ya watoto wetu!”

26 Basi akawafungulia Baraba, na baada ya kuamuru Yesu apigwe viboko, akamtoa asulubiwe.

Askari Wamdhihaki Yesu

27 Kisha askari wa gavana wakampeleka Yesu kwenye makao makuu ya gavana wakakusanya kikosi cha askari, wakamzunguka Yesu.

28 Wakamvua nguo zake, wakamvika kanzu ya rangi nyekundu. 29 Wakasokota taji ya miiba wakamvika kichwani. Wakamwekea fimbo mkono wake wa kulia, wakapiga magoti mbele zake wakamdhihaki wakisema, “Uishi maisha marefu, mfalme wa Wayahudi!” 30 Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga nayo kich wani. 31 Baada ya kumdhihaki, walimvua ile kanzu, wakamvika tena nguo zake. Kisha wakampeleka kumsulubisha.

Yesu Asulubishwa

32 Walipokuwa wakienda, walikutana na mtu mmoja wa Kirene aitwaye Simoni, wakambebesha ule msalaba kwa nguvu. 33 Na wali pofika sehemu iitwayo Golgotha, maana yake mahali pa Fuvu la Kichwa, 34 wakampa divai iliyochanganywa na nyongo ili anywe; lakini baada ya kuionja, akaikataa.

35 Walipokwisha kumsulubisha wakagawana nguo zake kwa kuzi pigia kura. 36 Kisha wakaketi, wakamchunga. 37 Juu ya kichwa chake, kwenye msalaba, wakaandika shtaka lake: ‘HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.’ 38 Wanyang’anyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja kulia kwake na mwingine kushoto kwake.

39 Watu waliokuwa wakipita njiani walimtukana, wakatikisa vichwa vyao 40 na kusema, “Si ulisema ungevunja Hekalu na kulijenga kwa muda wa siku tatu? Jiokoe basi! Kama wewe ni Mwana wa Mungu shuka msalabani.” 41 Hali kadhalika, makuhani wakuu, walimu wa sheria na wazee walimdhihaki, wakisema, 42 “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye si Mfalme wa Israeli? Ashuke kutoka msalabani nasi tutamwamini. 43 Anamwamini Mungu; basi Mungu na amwokoe sasa kama anamtaka. Kwa maana alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’ ” 44 Hata wale wanyang’anyi waliosulubiwa naye walimtukana kwa njia hiyo hiyo.

Kifo Cha Yesu

45 Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi nzima ilikuwa giza. 46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eli, Eli lama sabakthani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona ume niacha?”

47 Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama hapo waliposikia haya walisema, “Anamwita Eliya!” 48 Mmoja wao akaenda mbio akaleta sponji akaichovya kwenye siki akaiinua kwa mwanzi akamwekea mdo moni. 49 Lakini wengine wakasema, “Hebu tuone kama Eliya ata kuja kumwokoa.” [Na mwingine akachukua mkuki akamchoma ubavuni, pakatoka maji na damu].

50 Yesu akalia tena kwa sauti kuu, kisha akakata roho. 51 Wakati huo huo pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. 52 Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliofariki ili fufuka. 53 Walitoka makaburini na Yesu alipofufuka walikwenda Mji Mtakatifu wakawatokea watu wengi. 54 Basi yule jemadari na wale waliokuwa naye wakimlinda Yesu walipoona lile tetemeko na yote yaliyotokea, waliogopa wakasema, “Hakika, huyu alikuwa

Mwana wa Mungu!”

55 Wanawake wengi walio kuwa wamefuatana na Yesu tangu Gali laya wakimhudumia, nao walikuwapo wakitazama kwa mbali yote yali yotokea. 56 Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, Mariamu mama yake Yakobo na Yusufu na mama yao wana wa Zebedayo.

Yesu Azikwa Kaburini

57 Ilipofika jioni, alifika tajiri mmoja kutoka Arimathea aitwaye Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. 58 Akaenda kwa Pilato akaomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. 59-60 Yusufu alichukua mwili wa Yesu akauweka katika sanda safi akauzika katika kaburi lake jipya ambalo lilikuwa limechongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe kubwa akafu nika mlango wa kaburi, akaondoka. 61 Mariamu Magdalena na yule Mariamu mwingine walikuwa wamekaa mbele ya kaburi.

Walinzi Wa Kaburi

62 Siku iliyofuata, yaani siku iliyofuata ile siku ya Maan dalizi ya sabato, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato 63 wakamwambia, “Tunakumbuka kwamba yule mwongo alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 64 Tunaomba uamuru kwamba kabu ri liwekewe ulinzi hadi siku ya tatu. Vinginevyo wanafunzi wake wanaweza wakaja wakauiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Jambo hili likitokea uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya zaidi ya ule wa kwanza.” 65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari. Nendeni mkaweke ulinzi, mhakikishe pamekuwa salama kama mpendavyo.” 66 Wakaenda wakaweka ulinzi kaburini, wakaliwekea lile jiwe mhuri na kuwaweka askari walinzi.

Error: Book name not found: Esth for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 27

Paulo Asafirishwa Kwenda Rumi

27 Ilipoamuliwa kwamba twende Italia, walimkabidhi Paulo na wafungwa wengine kwa askari mmoja aitwaye Juliasi ambaye alikuwa wa kikosi cha Kaisari Agusto. Tulipakia meli iliyotoka Adrami tio ambayo ilikuwa ikielekea kwenye bandari zilizopo pwani ya Asia. Tukaanza safari yetu tukiongozana na Aristarko, Mmakedonia wa kutoka Thesalonike. Kesho yake tulifika Sidoni. Juliasi akamfanyia wema Paulo, akamruhusu aende kuwaona rafiki zake wam hudumie. Kutoka huko tuliendelea na safari yetu, na kwa kuwa tulikuwa tunakabili upepo, tukapitia upande wa kisiwa cha Kipro usioelekea upepo. Tukavuka bahari, kutoka upande wa Kilikia, na Pamfilia, tukafika Mira, katika jimbo la Likia. Yule askari akapata meli iliyokuwa inatoka Aleksandria ikielekea Italia, akatupakia humo. Tukasafiri pole pole kwa siku nyingi, na kwa shida na hatimaye tukafika karibu na bandari ya Nido. Lakini kwa kuwa upepo mkali ulikuwa ukivuma kutoka tulikokuwa tukielekea, hatukuweza kuendelea moja kwa moja na safari yetu, bali tulipitia upande wa pili wa Krete tukaizunguka ncha ya Salmone. Baada ya kuizunguka kwa shida tulifika sehemu iitwayo Bandari Nzuri, kar ibu na mji wa Lasea.

Tulikuwa tumepoteza muda mrefu baharini na kwa wakati huu safari ilikuwa ya hatari kwa maana majira ya kufunga yalikuwa yamekwisha pita. Paulo akawaonya marubani wa ile meli akasema, 10 ‘ ‘Mabwana, naona tukiendelea na safari hii patatokea maafa na hasara kubwa kwa meli na shehena na hata maisha yetu yatakuwa hatarini.” 11 Lakini yule askari akaamua kusikiliza zaidi ushauri wa nahodha na mwenye meli kuliko maneno ya Paulo. 12 Kwa kuwa ile bandari ilikuwa haifai kukaa wakati wa majira ya baridi, wengi wakashauri kwamba waendelee na safari na pengine kwa bahati wangeweza kufika Foinike. Hii ni bandari iliyoko katika kisiwa cha Krete na ambayo inatazama upande wa kusini-magharibi na kas kazini-magharibi, kwa hiyo wangeweza kukaa huko mpaka majira ya baridi yaishe.

Dhoruba Baharini

13 Upepo ulipoanza kuvuma taratibu toka kusini, wakadhani kuwa hii ilikuwa ni dalili nzuri kwamba wangeweza kuendelea na safari. Kwa hiyo wakang’oa nanga wakasafiri wakipita kando kando ya pwani ya kisiwa cha Krete. 14 Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali uitwao ‘Kaskazi-mashariki’ ukavuma toka nchi kavu; 15 ukaipiga ile meli, na kwa kuwa haikuwa rahisi kushindana nao, tukaiachilia meli isukumwe kuelekea kule upepo unakokwenda. 16 Hatimaye tukasafiri kupitia nyuma ya kisiwa kidogo kiitwacho Kauda, ambapo kwa kuwa tulikuwa tumekingiwa upepo na hicho kisiwa, tuliweza kwa shida kuifunga mashua ya kuokolea watu. 17 Watu walipokwisha ivuta mashua hiyo wakaiingiza katika meli, waliifunga kwa kamba kwenye meli. Kisha, kwa kuogopa kwamba wangesukumwa na upepo mkali na kukwama kwenye mchanga karibu na pwani ya Sirti, walishusha matanga wakaiacha meli ielee. 18 Kesho yake dhoruba kali iliendelea kuvuma, kwa hiyo wakaanza kuitupa shehena baharini. 19 Siku ya tatu wakaanza kutupa vifaa vya meli baharini kwa mikono yao wenyewe. 20 Kwa siku nyingi hatukuona jua wala nyota, na dhoruba kali ilikuwa inaendelea kuvuma. Kwa hiyo tukakata tamaa kabisa kwamba tungeokolewa.

21 Kwa kuwa walikuwa wamekaa siku kadhaa bila kula cho chote, Paulo akasimama kati yao akasema, “Mngenisikiliza wala msingeondoka Krete na kupata mkasa huu na hasara hii. 22 Lakini sasa nawaomba mjipe moyo. Hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake ila meli hii itaangamia. 23 Jana usiku, malaika wa Mungu wangu ambaye mimi namwabudu alisimama karibu yangu 24 akasema, ‘Usiogope Paulo; huna budi kujitetea katika kesi yako mbele ya Kaisari; na kwa neema yake, Mungu amekupa maisha ya watu wote wanaosafiri pamoja na wewe.’ 25 Kwa hiyo muwe na matu maini kwa maana nina imani kwa Mungu kwamba mambo yatakuwa kama nilivyoambiwa. 26 Lakini hata hiyo meli yetu itakwama kwenye kisiwa fulani. ”

27 Siku ya kumi na nne, mnamo saa sita za usiku, tulipokuwa bado tunasukumwa na upepo katika bahari ya Adria, mabaharia wali hisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu. 28 Kwa hiyo wakapima kina cha bahari wakakuta kilikuwa mita thelathini na tano hivi, na baada ya kitambo kidogo wakapima tena wakapata kina cha mita ishirini na sita hivi. 29 Wakaogopa kwamba meli yetu ingegonga kwenye miamba, kwa hiyo wakashusha nanga nne nyuma ya meli, wakawa wanaomba kupambazuke. 30 Mabaharia walikuwa wanataka kutoroka kutoka mle melini, wakashusha mashua baharini wakidanga nya kuwa walikuwa wanakwenda kuweka nanga upande wa mbele ya meli. Ndipo 31 Paulo akawaambia wale maaskari na maofisa wao, “Hawa watu wasipobaki katika meli, hamtaweza kuokolewa.” 32 Basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua kwenye meli wakaiacha mashua ichukuliwe baharini. 33 Mapambazuko yalipokaribia, Paulo akawasihi watu wote wale chakula akisema, “Leo ni siku ya kumi na nne mmekuwa katika wasiwasi bila kula cho chote. 34 Kwa hiyo nawasihi mle chakula kwa maana mnakihi taji ili muweze kuishi. Hakuna mmoja wenu atakayepoteza hata unywele mmoja kichwani mwake.” 35 Baada ya maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula. 36 Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chak ula. 37 Ndani ya meli tulikuwa jumla ya watu mia mbili na sabini na sita. 38 Baada ya wote kula chakula cha kutosha, wakapunguza uzito wa meli kwa kutupa ngano baharini.

39 Kulipokucha, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga ambako walitaka waielekeze meli kama ingewezekana, ili wafike pwani. 40 Kwa hiyo wakatupa nanga zote baharini, wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli, na kutweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani. 41 Lakini ile meli ikagonga mwamba ikakwama kwenye mchanga na upande wa mbele wa meli uka banwa kwenye mwamba wala usingeweza kuondolewa tena. Na upande wa nyuma ulivunjika vipande kwa nguvu ya yale mawimbi. 42 Wale askari walikuwa wamepanga kuwaua wafungwa wote ili wasije wakaogelea hadi pwani na kutoroka. 43 Lakini yule Ofisa wa maas kari alitaka kumwokoa Paulo, kwa hiyo akawazuia wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, na waogelee kuelekea pwani; 44 na wengine wajishikize kwenye vipande vya meli waelee navyo. Kwa jinsi hii, watu wote waliokolewa wakafika nchi kavu.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica