M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Awashutumu Walimu Wa Sheria Na Mafarisayo
23 Kisha Yesu akawaambia ule umati wa watu pamoja na wana funzi wake: 2 “Walimu wa sheria na Mafarisayo wamechukua nafasi ya Musa, 3 kwa hiyo watiini na kufanya yote wanayowaambia mfa nye. Lakini msifuate matendo yao; kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. 4 Wao hufunga mizigo mikubwa na kuwabebesha watu, lakini wao wenyewe hawajaribu hata kunyoosha kidole kuisogeza!
5 “Wao hufanya mambo yao yote ili waonekane na watu. Wanavaa vipande vipana vya ngozi vilivyoandikwa sheria na kurefusha zaidi pindo za mavazi yao ya sala. 6 Wanapenda kukaa viti vya wageni wa heshima karamuni na viti vya mbele katika masinagogi. 7 Hupenda kuamkiwa masokoni na kuitwa ‘Rabi.’
8 “Lakini ninyi msipende kuitwa ‘Rabi’ kwa sababu mnaye rabi mmoja, na ninyi nyote ni ndugu. 9 Na msimwite mtu ye yote hapa duniani ‘baba’ kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni. 10 Hali kadhalika msipende kuitwa ‘mabwana’ kwa maana mnaye Bwana mmoja tu, yaani Kristo. 11 Aliye mkuu kuliko ninyi nyote atakuwa mtumishi wenu. 12 Ye yote anayejikuza atashushwa; na ye yote anayejinyenyekeza atainuliwa.
13 “Lakini ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wanafiki! Kwa maana mnafungia watu milango ya Ufalme wa mbinguni. Ninyi wenyewe hamuingii humo, wala hamruhusu wale ambao wange penda kuingia waingie. [
14 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnadhulumu nyumba za wajane, na kwa kujionyesha kuwa wema, mnasali sala ndefu. Kwa hiyo adhabu yenu itakuwa kubwa zaidi.”]
15 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja awe mfuasi wa dini yenu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya astahili kwenda Jehena mara mbili zaidi yenu!
16 “Ole wenu viongozi vipofu! Ninyi mnasema, ‘Mtu akiapa kwa Hekalu, kiapo hicho si kitu; lakini mtu akiapa kwa dhahabu iliyoko Hekaluni, itambidi atimize kiapo hicho.’ 17 Ninyi vipofu wajinga! Ni kipi kilicho bora zaidi, ni ile dhahabu au ni Hekalu ambalo ndilo linafanya dhahabu hiyo kuwa takatifu? 18 Pia mnasema, ‘Mtu akiapa kwa madhabahu, si kitu, lakini mtu akiapa kwa sadaka iliyoko madhabahuni itambidi atimize kiapo hicho.’ 19 Ninyi vipofu! Ni kipi bora zaidi, sadaka, au madhabahu ambayo ndio inafanya sadaka hiyo kuwa takatifu? 20 Kwa hiyo mtu anayeapa kwa madhabahu, anaapa kwa hiyo madhabahu na vitu vyote vilivyoko juu yake. 21 Na mtu anapoapa kwa Hekalu, anaapa kwa hilo Hekalu na huyo aishie ndani yake. 22 Naye anayeapa kwa mbingu anaapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketiye juu ya kiti hicho.
23 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Kwa maana mnatoa fungu la kumi la mnanaa, na bizari na jira; lakini mmepuuza mambo makuu zaidi ya sheria: haki, huruma na imani. Haya mlipaswa kuyafanya bila kusahau yale mengine. 24 Ninyi viongozi vipofu, mnachuja nzi lakini mnameza ngamia!
25 “Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Kwa maana mnasafisha kikombe na sahani kwa nje lakini ndani mmejaa ulafi na unyang’anyi. 26 Ninyi Mafarisayo vipofu! Kwanza safisheni kikombe na sahani kwa ndani, ndipo nje patakuwa safi.
27 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa juu yanaonekana maridadi lakini ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila aina ya uchafu. 28 Hali kadhalika, nje ninyi mnaonekana kwa watu kuwa wenye haki, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.
29 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kupamba makaburi ya wenye haki 30 mkisema, ‘Kama tungaliishi wakati wa baba zetu tusingel ishiriki katika kuwaua manabii !’ 31 Kwa kusema hivyo mnakiri kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii. 32 Haya basi, kamilisheni hiyo kazi waliyoianza baba zenu! 33 Ninyi nyoka, ninyi kundi la nyoka! Mtaepukaje hukumu ya Jehena? 34 Kwa sababu hiyo nawapelekea manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwatundika msalabani, wengine mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na wengine mtawatesa toka mji mmoja hadi mji mwingine. 35 Na kwa hiyo damu ya wote wenye haki ambayo imemwagwa hapa duniani, tangu damu ya Abeli, ambaye alikuwa hana hatia, hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia ambaye mlimwua kati kati ya Patakatifu na madhabahu, itakuwa juu yenu. 36 Nawaambia kweli haya yote yatatokea wakati wa kizazi hiki.”
Yesu Awaonya Watu Wa Yerusalemu
37 “Ninyi watu wa Yerusalemu; mnawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu! Nilitamani sana kuwakusanya wana wenu kama vile kuku akusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini hamkutaka! 38 Tazama nyumba yenu imeachwa tupu na ukiwa. 39 Kwa maana nawahakikishia kuwa, hamtaniona tena mpaka siku ile mtakaposema: ‘Amebarikiwa yeye anayekuja kwa jina la Bwana.
23 Paulo akawakazia macho wajumbe wa baraza, akasema, “Ndugu zangu, mimi nimeishi nikiwa na dhamiri safi kabisa siku zote mbele za Mungu, mpaka leo.” 2 Kuhani mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa karibu na Paulo wampige kofi mdomoni. 3 Ndipo Paulo akasema, “Mungu atakupiga, wewe ukuta uliopakwa chokaa! Unawe zaje kusikiliza kesi hii kwa mujibu wa sheria, na hapo hapo, kinyume cha sheria, unaamuru nipigwe?” 4 Wale watu waliokuwa wamesimama karibu wakamwambia Paulo, “Mbona unamtukana kuhani mkuu wa Mungu?” 5 Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kwamba yeye ni kuhani mkuu. Kwa maana Maandiko yanasema, ‘Usimseme vibaya kiongozi wa watu wako.’ ” 6 Paulo alipotambua ya kuwa baadhi ya wajumbe wa baraza walikuwa Masadukayo na wengine ni Mafarisayo alisema nao kwa sauti kubwa, “Ndugu zangu! Mimi ni Mfarisayo, mtoto wa Mafarisayo; na hapa nimeshitakiwa kuhusu tumaini juu ya ufufuo wa wafu.” 7 Aliposema haya, Mafarisayo na Masadukayo wakafarakana na baraza zima likagawanyika. 8 Kwa maana Masadukayo wanaamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho; lakini Mafarisayo wanaamini haya yote. 9 Kelele zikazidi sana; na baadhi ya waandishi wa sheria wa upande wa Mafarisayo, wakasimama wakiwapinga wengine wakasema, “Hatuoni kosa lo lote alilofanya mtu huyu! Huenda ikawa malaika au roho amezungumza naye kweli!” 10 Mabishano yalipozidi kuwa makali, yule jemadari aliogopa kuwa wangeweza kumrarua Paulo vipande vipande. Kwa hiyo akaamuru askari wakamtoe Paulo alipokuwa, arudishwe kwenye ngome ya jeshi. 11 Usiku uliofuata, Bwana akamtokea Paulo akasimama karibu naye akamwambia, “Jipe moyo! Kama ulivyonishuhudia hapa Yerusalemu, itakubidi unishuhudie na huko Rumi pia.”
Njama Za Wayahudi Kumwua Paulo
12 Kulipopambazuka Wayahudi wakala njama ya kumwua Paulo. Wakaweka nadhiri kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wamemwua Paulo. 13 Waliofanya mpango huu walikuwa zaidi ya watu arobaini. 14 Wakaenda kwa kuhani mkuu na wazee wakasema, “Tumeweka nad hiri ya pamoja kwamba hatutakula wala kunywa mpaka tumwue Paulo. 15 Kwa hiyo ninyi pamoja na baraza, pelekeni ombi kwa jemadari ili Paulo aletwe barazani, mtoe udhuru kwamba mnataka kuchunguza kesi yake kwa usahihi zaidi. Sisi tutakuwa tayari kumwua hata kabla hajakaribia kufika hapa.” 16 Basi kumbe binamu yake Paulo alisikia kuhusu mpango huu. Akaenda katika ngome ya jeshi akamweleza Paulo mambo haya. 17 Paulo akamwita mmoja wa wale maaskari akamwambia, “Mchukue kijana huyu kwa jemadari, ana neno la kumwambia.” 18 Yule askari akamchukua yule kijana mpaka kwa jemadari akamwambia, “Yule mfungwa Paulo aliniita akaniambia nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukuambia.” 19 Yule jemadari akamchukua yule kijana kando akamwuliza, “Unataka kuniambia nini?” 20 Naye akasema, “Wayahudi wameku baliana wakuombe kesho umpeleke Paulo kwenye Baraza lao kwa kisingizio kwamba wanataka kuchunguza kesi yake kwa uangalifu zaidi. 21 Lakini usikubali ombi lao kwa maana zaidi ya watu aro baini wamekula njama kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wamwue Paulo nao wamejiweka tayari kumvizia ukishakubali ombi lao.” 22 Yule jemadari akamruhusu yule kijana aende, akamwonya akisema, “Usimwambie mtu ye yote kwamba umenieleza habari hizi.”
Paulo Apelekwa Kaisaria Kwa Gavana Feliksi
23 Yule jemadari akawaita maaskari wawili akawaambia, “Tay arisheni askari mia mbili watakaokwenda Kaisaria pamoja na askari wa farasi sabini, na askari wa mikuki mia mbili; nanyi muwe tay ari kuondoka leo saa tatu za usiku. 24 Pia tayarisheni na farasi watakaotumiwa na Paulo, mumpeleke salama mpaka kwa gavana Feliksi.” 25 Kisha akaandika barua kwa Feliksi kama ifuatavyo: 26 “Mimi Klaudio Lisia, nakuandikia wewe gavana mtukufu Feliksi. Salamu. 27 Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi wakawa kar ibu kumwua, ndipo mimi nilipofika na askari wangu nikamwokoa kwa kuwa nilipata habari kwamba yeye ni raia wa Kirumi. 28 Nami nikampeleka mbele ya baraza lao ili nipate kujua kosa alilofanya. 29 Ndipo nikagundua ya kuwa alikuwa anashtakiwa kuhusu sheria yao, lakini hakuwa na kosa la kustahili kifo au kifungo. 30 Lakini nilipata habari kwamba kuna mpango wa kumwua nikaamua nimpeleke kwako mara moja, nikawaamuru washitaki wake walete mashtaka yao kwako.” 31 Basi wale askari wakamchukua Paulo usiku wakampeleka mpaka Antipatri kama walivyoamriwa. 32 Kesho yake wakarudi kituoni wakawaacha wale askari wa mikuki waendelee na safari pamoja na Paulo. 33 Walipofika Kaisaria walimpa Liwali ile barua na pia wakamkabidhi Paulo kwake. 34 Alipokwisha soma ile barua, alimwuliza Paulo ametoka jimbo gani. Alipofahamishwa kuwa anatoka Kilikia 35 alisema, “Nitasikiliza kesi yako mara tu washtaki wako watakapofika.” Akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi katika ikulu ya Herode.
Copyright © 1989 by Biblica