M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili
10 Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa mamlaka ya kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina. 2 Majina ya hao wanafunzi kumi na wawili ni haya: 3 wa kwanza, Simon, ambaye aliitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo, mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; Filipo na Bartholomayo; Tomaso na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; 4 Simoni Mkanaani; na Yuda Iskariote ambaye baadaye alimsaliti Yesu. 5 Yesu aliwatuma hawa kumi na wawili, akawaagiza, “Msiende kwa watu wa mataifa wala msiingie mji wo wote wa Wasamaria. 6 Bali waendeeni kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. 7 Na mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia; 8 Waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepo kea bure, toeni bure. 9 Msichukue dhahabu, wala fedha wala sarafu za shaba katika mikanda yenu. 10 Msichukue mikoba ya safari, wala koti la pili, wala viatu, wala fimbo: kwa maana mfanyakazi anastahili riziki yake.
11 “Mkiingia katika mji au kijiji cho chote, mtafuteni mtu mwaminifu mkae kwake mpaka mtakapoondoka. 12 Kila nyumba mtakay oingia, toeni salamu. 13 Kama watu wa nyumba hiyo wanastahili, amani yenu na ikae kwao; na kama hawastahili, amani yenu itawaru dia ninyi. 14 Na kama mtu ye yote akikataa kuwapokea au kusiki liza maneno yenu, mtakapoondoka katika nyumba hiyo au mji huo, kung’uteni mavumbi yatakayokuwa miguuni mwenu. 15 Nawaambieni hakika, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Sodoma na Gomora kuliko itakavyokuwa kwa mji huo.”
Yesu Awatayarisha Wanafunzi Wake Kwa Mateso
16 “Ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo muwe werevu kama nyoka na wapole kama hua. 17 Jihadharini na watu, kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga viboko kwenye masinagogi yao. 18 Mtapelekwa mbele ya magavana na wafalme kwa ajili yangu mkatoe ushuhuda mbele yao na mbele ya watu wa mataifa. 19 Lakini mtakapokamatwa, msihangaike mkifiki ria mtakalosema; kwa maana mtaambiwa la kusema wakati huo. 20 Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkizungumza bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akisema kupitia kwenu. 21 Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe, na baba atamsaliti mwanae auawe. Watoto nao wataasi wazazi wao na kusababisha wauawe. 22 Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ataokoka. 23 Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kwa maana nawaambieni hakika, hamtamaliza kuipitia miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu hajafika.
24 “Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake wala mtumishi hamzidi bwana wake. 25 Inatosha ikiwa mwanafunzi atakuwa kama mwalimu wake na mtumishi kama bwana wake. Ikiwa wamethubutu kum wita bwana mwenye nyumba Beelzebuli, je, si watawasema vibaya zaidi jamaa ya mwenye nyumba?”
Anayestahili Kuogopwa
27 Ninalo waambia gizani, ninyi litamkeni mwangani: na lile mnalosikia likinong’onwa, litangazeni mkiwa mmesimama kwenye paa la nyumba. 28 Msiwaogope wale wawezao kuua mwili lakini hawawezi kuua roho; ila mwogopeni yeye ambaye anaweza kuiangamiza roho na mwili katika moto wa Jehena. 29 Mbayuwayu wawili huuzwa kwa sarafu moja tu. Lakini hata mmoja wao hawezi kuanguka pasipo Baba yenu kupenda. 30 Hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa. 31 Kwa hiyo msiogope; kwa maana ninyi mna thamani kubwa zaidi kuliko mbayuwayu wengi. 32 Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni. 33 Lakini ye yote atakayenikana mbele ya watu, mimi pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.”
Gharama Ya Kumfuata Yesu
34 “Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali vita. 35 Kwa maana nimekuja kuleta kutokuele wana kati ya mtu na baba yake, na kati ya binti na mama yake, na kati ya mkwe na mama mkwe wake. 36 Na maadui wakubwa wa mtu watakuwa watu wa nyumbani kwake. 37 Ye yote anayempenda baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Na ye yote ampendaye mwanae au binti yake kuliko anavyoni penda mimi, hastahili kuwa wangu. 38 Na ye yote asiyechukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. 39 Ata kayeng’ang’ania nafsi yake ataipoteza lakini aipotezae nafsi yake kwa ajili yangu ataipata.”
Watakaopokea Tuzo
40 “Mtu ye yote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi; na ye yote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye ali yenituma. 41 Mtu anayemkaribisha nabii kwa kuwa ni nabii, atapo kea tuzo ya nabii; na mtu anayemkaribisha mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapokea tuzo ya mwenye haki. 42 Na mtu ata kayetoa japo kikombe cha maji kwa mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, basi ninawaambieni hakika, hatakosa tuzo yake.”
Mungu Ajibu Sala Ya Kornelio
10 Katika mji wa Kaisaria aliishi afisa mmoja wa jeshi ambaye alikuwa kamanda wa kikosi cha Italia, jina lake Kornelio. 2 Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na jamii yake yote. Alitoa msaada kwa ukarimu kwa watu na kumwomba Mungu mara kwa mara.
3 Alasiri moja, mnamo saa tisa, malaika wa Mungu alimjia katika ndoto na kumwita, “Kornelio!” 4 Kornelio akamtazama yule malaika kwa hofu akasema, “Ni nini Bwana?” Malaika akasema, “Sala zako na sadaka ulizotoa kwa maskini zimefika mbinguni, na Mungu amezikumbuka. 5 Sasa tuma watu Jopa wakamlete Simoni ait waye Petro. 6 Yeye hivi sasa anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi kando ya bahari.” 7 Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye ali poondoka, Kornelio aliwaita watumishi wake wawili na mlinzi wake mmoja aliyekuwa mcha Mungu, 8 na baada ya kuwasimulia mambo yote yaliyotokea, akawatuma waende Jopa.
9 Kesho yake, walipokuwa wanaukaribia mji, Petro alipanda juu ghorofani kuomba mnamo saa sita. 10 Alipokuwa akisali aliona njaa akatamani kupata chakula. Lakini wakati kilipokuwa kinaan daliwa, alisinzia akaota ndoto. 11 Akaona katika ndoto mbingu zimefunguka na kitu kama shuka kubwa ikishushwa kwa ncha zake nne. 12 Ndani ya ile shuka walikuwemo aina zote za wanyama na nyoka na ndege. 13 Kisha sauti ikamwambia Petro, “Inuka, uchinje na ule mnyama ye yote umpendaye kati ya hawa.” 14 Petro akajibu, “La Bwana! Sijawahi kula cho chote ambacho kimetajwa na sheria zetu za Kiyahudi kuwa ni kichafu.” 15 Ile sauti ikarudia kusema naye mara ya pili, “Usiite cho chote alichokitakasa Bwana kuwa ni kichafu.” 16 Hii ilitokea mara tatu, ndipo ile shuka ikarudishwa mbinguni.
17 Petro alikuwa bado akijiuliza maana ya mambo haya aliyoy aona, wakati wale watu waliokuwa wametumwa na Kornelio walipofika kwenye nyumba ya Simoni mtengenezaji ngozi. 18 Wakabisha hodi na kuuliza kama Simoni aliyeitwa Petro alikuwa anaishi hapo.
19 Wakati huo Petro alikuwa akifikiria juu ya ile ndoto, Roho Mtakatifu akamwambia, “Wako watu watatu wamekuja kukuta futa. 20 Shuka chini ukaonane nao na usione shaka kwenda nao kwa kuwa nimewatuma kwako.” 21 Petro akashuka, akawaendea wale watu akawaambia, “Mimi ndiye mnayemtafuta. Mnataka nini?” 22 Wao wakamjibu, “Tumetumwa na Kamanda Kornelio ambaye ni mtu mwema anayemcha Mungu na kusifiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagi zwa na malaika wa Mungu akukaribishe nyumbani kwake, ili asiki lize maneno utakayomwambia.” 23 Petro aliwakaribisha walale kwake. Kulipokucha akaandamana nao pamoja na baadhi ya ndugu waamini wa pale Jopa.
Petro Nyumbani Kwa Kornelio
24 Kesho yake wakawasili Kaisaria. Kornelio alikuwa akiwan goja pamoja na ndugu zake na marafiki wa karibu ambao alikuwa amewaalika. 25 Petro alipokuwa akiingia ndani, Kornelio alikuja kumlaki, akapiga magoti. 26 Lakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama! Mimi ni mwanadamu tu.” 27 Petro alipokuwa akizungumza naye aliingia ndani ambapo alikuta watu wengi wamekusanyika. 28 Petro akawaambia, “Mnajua kwamba sheria ya Wayahudi hairu husu Myahudi kuwatembelea au kuchangamana na watu wa mataifa men gine kama hivi nifanyavyo. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwone mtu ye yote kuwa mchafu au asiyefaa. 29 Ndiyo sababu ulipotuma nije sikusita. Kwa hiyo naomba unieleze kwa nini ume niita.” 30 Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa mchana. Mara akatokea mtu aliyevaa nguo za kung’ara akasimama mbele yangu. 31 Akasema, ‘Kornelio, maombi yako yamesikiwa na Mungu, naye amekumbuka msaada wako kwa maskini. 32 Basi tuma watu waende Jopa wakamwite Simoni aitwaye Petro. Yeye ni mgeni katika nyumba ya Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko sehemu za pwani.’ 33 Ndio sababu nilituma watu kwako mara moja, nawe umefanya vizuri kuja. Basi sasa tuko hapa wote mbele ya Mungu kuyasikiliza yote ambayo Mungu amekuamuru kutuambia.”
Hotuba Ya Petro
34 “Ndipo Petro alianza kwa kusema, “Sasa naamini ya kuwa Mungu hana upendeleo. 35 Yeye huwakubali watu wa kila taifa wam chao na kutenda haki. 36 Huu ndio ujumbe ambao Mungu aliwapele kea watu wa Israeli, kuhusu Habari Njema za amani kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye ni Bwana wa wote. 37 Ninyi bila shaka mnafa hamu mambo yaliyotokea sehemu zote za Yudea, kuanzia Galilaya tangu wakati wa mahubiri ya Yohana Mbatizaji. 38 Mnafahamu jinsi Mungu alivyompa Yesu wa Nazareti Roho Mtakatifu na uwezo, na jinsi alivyozunguka kila mahali akifanya mema na kuponya wote waliokuwa wakiteswa na nguvu za shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye. 39 Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyofanya katika nchi ya Wayahudi na Yerusalemu. Walimwua kwa kumtundika msalabani. 40 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu siku ya tatu na akamwezesha kuonekana na watu. 41 Hakuonekana kwa watu wote, lakini alionekana kwa mashahidi ambao Mungu aliwachagua, yaani sisi ambao tulikula na kunywa naye baada ya kufufuka kwake. 42 Naye alituamuru kuhubiri kwa watu wote, na kushuhudia kwamba yeye ndiye aliyechaguliwa na Mungu kuwahukumu walio hai na wafu. 43 Manabii wote walishuhudia juu yake, kwamba kila mtu amwami niye atasamehewa dhambi katika jina lake.”
Mataifa Wapokea Roho Mtakatifu
44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo, Roho Mtakatifu ali washukia wote waliokuwa wakisikiliza. 45 Wale Wayahudi waamini waliokuwa wamekuja na Petro walishangaa sana kuona kuwa Mungu aliwapa watu wa mataifa kipawa cha Roho Mtakatifu. 46 Kwa kuwa waliwasikia wakisema kwa lugha mpya na kumtukuza Mungu kwa ukuu wake. Ndipo Petro akasema, 47 “Je, kuna mtu anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.” 48 Kwa hiyo akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Wakamsihi Petro akae nao kwa siku chache.
Copyright © 1989 by Biblica