M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Amponya Mtu Aliyepooza
9 Yesu akaingia katika mashua akavuka ziwa, akafika katika mji wa kwao. 2 Watu wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye kitanda chake. Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mtu ali yepooza, “Mwanangu, jipe moyo; dhambi zako zimesamehewa.” 3 Baadhi ya walimu wa sheria wakawaza moyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” 4 Lakini Yesu alifahamu mawazo yao. Akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5 Kwani ni lipi lililo rahisi: kusema ‘Dhambi zako zimesamehewa 6 Lakini, nitawathibitishia kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Akamwambia yule aliyepo oza, “Simama, chukua kitanda chako uende nyumbani.” 7 Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani. 8 Watu walipoyaona haya, wakaogopa, wakamtukuza Mungu ambaye alitoa uwezo wa jinsi hii kwa wanadamu.
Yesu Amwita Mathayo
9 Yesu alipoondoka hapo, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi katika ofisi ya kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate”. Mathayo akainuka, akamfuata. 10 Wakati Yesu alipo kuwa ameketi mezani kula chakula katika nyumba fulani, watoza kodi wengi na wenye dhambi walikuja kula pamoja naye na wanafunzi wake. 11 Mafarisayo walipoona mambo haya wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini mwalimu wenu anakula na watoza kodi na wenye dhambi?” 12 Lakini Yesu alipowasikia aliwaambia, “ Watu wenye afya hawahitaji daktari, lakini wagonjwa wanamhitaji. 13 Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya, ‘Napenda huruma na wala sio sadaka za kuteketeza.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”
Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga
14 Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walikuja kwa Yesu wakamwuli za, “Mbona sisi na Mafarisayo tunafunga lakini wanafunzi wako hawafungi?” 15 Yesu akawajibu, “Hivi inawezekana wageni wali oalikwa harusini kuomboleza wakati bwana harusi yuko nao? Wakati utafika ambapo bwana harusi ataondolewa kwao. Hapo ndipo wataka pofunga. 16 Hakuna mtu anayeweka kiraka kipya kwenye nguo kuu kuu, kwa maana kile kiraka kitachanika kutoka kwenye nguo hiyo na tundu litakalotokea litakuwa kubwa zaidi ya lile la mwanzo. 17 Wala watu hawahifadhi divai mpya kwenye viriba vikuukuu; wakifanya hivyo, viriba vitapasuka na divai itamwagika. Lakini divai mpya huwekwa katika viriba vipya na kwa njia hiyo divai na viriba husalimika.”
Yesu Amponya Mwanamke Aliyetokwa Damu
18 Wakati Yesu akiwa anawaambia haya, akaja afisa fulani akapiga magoti mbele yake, akamwambia, “Binti yangu amefariki lakini tafadhali uje umwekee mkono wako juu yake naye atakuwa hai.” 19 Yesu akasimama akamfuata. Wanafunzi wake pia wakaan damana naye.
20 Akatokea mwanamke mmoja ambaye alikuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja nyuma ya Yesu akagusa upindo wa nguo yake, 21 kwa maana alisema moyoni mwake, “Nikigusa tu nguo yake, nitaponywa.” 22 Yesu akageuka, na alipomwona akamwambia, “Binti, jipe moyo, imani yako imekuponya.” Na wakati huo huo yule mwanamke akapona.
Yesu Amfufua Binti Wa Afisa
23 Yesu alipofika nyumbani kwa yule afisa, aliwakuta waom bolezaji wanapiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele. 24 Akawaambia, “Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala.” Wakamcheka kwa dhihaka. 25 Lakini watu walipok wisha tolewa nje, aliingia ndani akamshika mkono yule binti, naye akaamka. 26 Habari hizi zikaenea wilaya ile yote.
Yesu Aponya Vipofu
27 Yesu alipoondoka pale, vipofu wawili walimfuata wakipiga kelele kwa nguvu, “Mwana wa Daudi, tuhurumie.” 28 Alipoingia ndani wale vipofu walimfuata. Akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kuwafanya muone?” Wakamjibu, “Ndio Bwana.” 29 Ndipo Yesu akagusa macho yao akasema, “Na iwe kwenu kama mnavyo amini.” 30 Macho yao yakafunguka. Naye akawaonya, “Angalieni mtu ye yote asijue jambo hili.” 31 Lakini wao walipoondoka walieneza sifa zake katika ile wilaya yote.
Yesu Amponya Bubu
32 Walipokuwa wakiondoka, watu walimletea mtu bubu, ali yekuwa amepagawa na pepo. 33 Na yule pepo alipofukuzwa, yule aliyekuwa bubu aliweza kusema. Ule umati wa watu wakastaajabu, wakasema, “Jambo kama hili halijawahi kuonekana katika Israeli.” 34 Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo kwa uwezo wa mkuu wa pepo.”
Wafanyakazi Ni Wachache
35 Yesu akazunguka kwenye miji yote na vijiji vyote akifundi sha katika masinagogi na kuhubiri Habari Njema za Ufalme, na kuponya kila ugonjwa na kila udhaifu. 36 Alipoona umati wa watu, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanateseka pasipo msaada, kama kondoo wasio na mchungaji.
37 Akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini wafa nyakazi ni wachache; 38 basi mwombeni Bwana wa mavuno ili awape leke wafanyakazi kwenye mavuno yake.”
Kuokoka Kwa Sauli
9 Wakati huu wote Sauli alikuwa bado anaendelea na vitisho vyake vya kuwaangamiza kabisa wanafunzi wa Bwana. Akaenda kwa Kuhani Mkuu, 2 akamwomba ampe barua ya kumtambulisha kwa masina gogi ya huko Dameski, ili akiwapata wafuasi wa ile ‘Njia 3 Basi katika safari yake, alipokuwa akikaribia Dameski, ghafla nuru kutoka mbinguni iliangaza kumzunguka! 4 Akaanguka chini! Na aka sikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona unanitesa?” 5 Sauli akajibu, “Ni nani wewe, Bwana?” Ile sauti ikasema, “Mimi ni Yesu ambaye unamtesa. 6 Lakini sasa inuka uingie mjini nawe utaambiwa la kufanya.” 7 Wale waliokuwa wakisafiri na Sauli wakasimama kwa mshangao, wala hawakuweza kusema neno kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. 8 Sauli akainuka na alipojaribu kufungua macho, hakuweza kuona kitu. Basi wakamshika mkono wakamwongoza mpaka Dameski. 9 Na kwa muda wa siku tatu akawa haoni kabisa, na hakula kitu wala kunywa cho chote.
10 Huko Dameski alikuwepo mfuasi mmoja jina lake Anania. Bwana akamwita Anania katika ndoto, “Anania! ” Akaitika, “Nipo hapa Bwana.” 11 Bwana akamwambia, “Amka uende barabara iitwayo Nyofu ukaulizie katika nyumba ya Yuda kuhusu mtu aitwaye Sauli wa Tarso. Yeye hivi sasa anaomba, na katika maono anamwona mtu 12 aitwaye Anania akija na kuweka mikono juu yake ili aweze kuona tena.” 13 Anania akajibu, “Bwana, nimesikia kutoka kwa watu wengi mambo ya kutisha ambayo mtu huyu anawatendea wataka tifu wako huko Yerusalemu. 14 Naye amekuja hapa Dameski akiwa na kibali kutoka kwa Kuhani Mkuu awakamate wote wanaotaja jina lako.” 15 Lakini Bwana akamwambia Anania, “Nenda, kwa maana nimemchagua awe mtumishi wangu wa kulitangaza jina langu kwa mataifa na wafalme na kwa wana wa Israeli; 16 nami nitamwonyesha atakavyoteseka sana kwa ajili ya jina langu .” 17 Anania akaenda, akaingia mle nyumbani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu yangu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea njiani ame nituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.” 18 Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka machoni mwa Sauli, akapata kuona tena. Akasimama, akabatizwa. 19 Kisha akala chak ula, akapata nguvu tena. Alikaa siku kadhaa pamoja na wanafunzi huko Dameski na 20 bila kukawia akaenda katika sinagogi akawash uhudia watu kwamba, “Yesu ni Mwana wa Mungu.”
Sauli Ahubiri Dameski
21 Watu wote waliomsikia Sauli walishangaa wakasema, “Huyu si yule mtu aliyekuwa akiwatesa watu waliotaja jina la Yesu huko Yerusalemu, na ambaye amekuja hapa kwa shabaha ya kuwakamata na kuwapeleka wakiwa wamefungwa kwa makuhani wakuu?” 22 Lakini Sauli alizidi kuhubiri kwa nguvu zaidi akathibitisha kabisa kwamba Yesu ndiye Kristo; hata Wayahudi walioishi Dameski hawa kuwa na lo lote la kupinga. 23 Baada ya siku nyingi kupita, Way ahudi walifanya mpango wa kumwua Sauli. 24 Lakini Sauli akapata habari za mpango huo. Wayahudi walikuwa wakilinda milango yote ya kutokea mjini, mchana na usiku ili akitoka wamwue. 25 Lakini wanafunzi wake wakamtoa nje ya mji usiku kwa kumpitisha mahali palipokuwa na nafasi katika ukuta wa mji, akiwa ndani ya kapu kubwa.
Sauli Atoa Ushuhuda Wake Yerusalemu
26 Sauli alipofika Yerusalemu alijaribu kujiunga na waamini lakini wao walimwogopa kwa maana hawakuamini ya kuwa kweli ali kuwa amemwamini Yesu. 27 Lakini Barnaba akamchukua Sauli akampeleka kwa wale mitume akawaeleza jinsi Sauli alivyokutana na Yesu njiani akienda Dameski na Yesu akasema naye. Pia akawaeleza jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski. 28 Kwa hiyo Sauli akakaa nao akishirikiana nao na aki hubiri wazi wazi kwa jina la Yesu kila mahali huko Yerusalemu.
29 Lakini alipowahubiria Wayahudi wenye asili ya Kigiriki na kubishana nao, wao waliamua kumwua. 30 Waamini wengine walipo pata habari hizi walimchukua hadi Kaisaria wakamsafirisha kwenda Tarso. 31 Ndipo kanisa katika Yudea yote, Galilaya na Samaria likawa na wakati wa amani. Kanisa likapata nguvu likienenda katika kicho cha Bwana; na kwa msaada wa Roho Mtakatifu, idadi yake ikazidi kuongezeka.
Petro Amponya Ainea
32 Petro alipokuwa akiwatembelea waamini sehemu mbalimbali alifika kwa watu wa Mungu walioishi huko Lida. 33 Akamkuta mtu mmoja aitwaye Ainea, ambaye alikuwa amepooza na kwa muda wa miaka minane alikuwa hajaondoka kitandani. 34 Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo anakuponya; inuka utandike kitanda chako.” Na mara Ainea akainuka. 35 Wakazi wote wa Lida na Sharoni wali pomwona Ainea akitembea walimgeukia Bwana.
Petro Amfufua Dorkasi
36 Huko Jopa kulikuwa na mwanafunzi mwanamke aliyeitwa Tabita au kwa lugha ya Kigiriki, Dorkasi, yaani paa. Huyu mama alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. 37 Hata hivyo aliugua akafa. Wakamwosha na kumlaza katika chumba cha ghorofani. 38 Kwa kuwa Jopa hapakuwa mbali sana na Lida, wanafunzi waliposikia kuwa Petro yuko Lida, waliwatuma wenzao wawili wakamwambie, “Tafadhali njoo huku pasipo kukawia.” 39 Kwa hiyo Petro akaharakisha akaenda nao Jopa. Alipowasili wakampeleka hadi kwenye chumba alipokuwa amelazwa marehemu Dor kasi. Wajane wengi walikuwa wamemzunguka marehemu wakilia na kuonyesha mavazi ambayo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa hai. 40 Petro akawatoa wote nje, kisha akapiga magoti akaomba; akaugeukia ule mwili akasema, “Tabita, Amka!” Dorkasi akafumbua macho na alipomwona Petro, akaketi. 41 Petro akamshika mkono akamsaidia kusimama. Ndipo alipowaita wale waamini na wajane aka wakabidhi Dorkasi akiwa hai. 42 Habari hizi zilienea sehemu zote za Jopa. Na watu wengi wakamwamini Bwana. 43 Petro akakaa Jopa kwa muda mrefu, akiishi na mtengenezaji ngozi mmoja aitwaye
Copyright © 1989 by Biblica