M’Cheyne Bible Reading Plan
Yesu Ajaribiwa Na Shetani
4 Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu mpaka nyikani ili akajaribiwe na shetani. 2 Akakaa huko siku arobaini akifunga, pasipo kula kitu cho chote mchana na usiku, hatimaye akaona njaa. 3 Ndipo shetani akamjia akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”
4 Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno analotamka Mungu.’ ”
5 Ndipo shetani akampeleka Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerus alemu, akamweka juu ya mnara wa Hekalu, 6 akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa kuwa imeandikwa, ‘Atawaagiza malaika wake wakuhudumie,’ na, ‘Watakuinua juu mikononi mwao ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.’ ”
7 Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”
8 Kwa mara nyingine shetani akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia na fahari zake, 9 kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukipiga magoti na kuniabudu.”
10 Yesu akamwambia, “Ondoka hapa shetani! Kwa maana imean dikwa, ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako na utamtumikia yeye peke yake.’ ” 11 Ndipo shetani akamwacha, na malaika wakaja wakamhu dumia.
Yesu Aanza Kuhubiri
12 Yesu aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ameka matwa na kuwekwa gerezani, alirudi Galilaya. 13 Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu karibu na ziwa, katika eneo la Zabuloni na Naftali. 14 Utabiri wa nabii Isaya ukatimia, kama alivyosema: 15 “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya watu wa mataifa - 16 watu wale waishio katika giza wameona nuru kuu; na kwa wale wanaoishi katika nchi ya giza la mauti, nuru imewaangazia.” 17 Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”
Yesu Awaita Wanafunzi Wanne
18 Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya ziwa la Galilaya aliwaona ndugu wawili, Simoni ambaye aliitwa Petro na Andrea ndugu yake. Walikuwa katika mashua wakitupa nyavu zao baharini kwa maana wao walikuwa wavuvi.
19 Yesu akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya muwe wavuvi wa watu.” 20 Wakaziacha nyavu zao mara moja, wakamfuata.
21 Alipoendelea mbele kidogo, aliwakuta ndugu wengine wawili, Yakobo na Yohana, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo wakishona nyavu zao; akawaita. 22 Wakaacha nyavu zao mara moja, wakamfuata.
Yesu Ahubiri Na Kuponya Wagonjwa
23 Yesu alizunguka Galilaya yote, akifundisha katika masi nagogi na kuhubiri Habari Njema ya Ufalme wa mbinguni, na kupo nya kila ugonjwa na kila udhaifu. 24 Kwa hiyo sifa zake zilienea sehemu zote za Siria. Nao wakamletea wagonjwa wote, waliosumbu liwa na maradhi mbalimbali na maumivu, watu waliopagawa na mashe tani, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya.
25 Umati mkubwa wa watu ukamfuata kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na kutoka ng’ambo ya mto Yordani.
Petro Na Yohana Wakamatwa
4 Walipokuwa bado wanasema na watu, makuhani, mkuu wa walinzi wa Hekalu na Masadukayo waliwajia wakiwa 2 wamekasirika kwa sababu Petro na Yohana walikuwa wakiwafundisha watu kwamba kufu fuka kwa Yesu kunadhihirisha kwamba wafu watafufuka. 3 Wakawaka mata wakawaweka jela mpaka kesho yake kwa maana ilikuwa jioni. 4 Lakini wengi wa wale waliosikia mahubiri yao waliamini; idadi ya wanaume walioamini ilikuwa kama elfu tano.
5 Siku ya pili yake viongozi wa Kiyahudi, wazee na waandishi wa sheria walikusanyika Yerusalemu. 6 Walikuwepo Kuhani Mkuu Anasi, Kayafa , Yohana, Aleksanda na ndugu zake Kuhani Mkuu. 7 Wakawaleta wale mitume wawili katikati yao wakawauliza, “Ni kwa uwezo gani au mmetumia jina la nani kufanya jambo hili?” 8 Petro, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu akajibu, “Waheshimiwa viongozi na wazee wa watu, 9 kama mnatuhoji kuhusu mambo mema aliyotendewa kilema, na jinsi alivyoponywa, tungependa ninyi na watu wote wa 10 Israeli mfahamu kwamba, ni kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha lakini Mungu akam fufua kutoka kwa wafu, kwa uwezo wa Yesu, huyu mtu anasimama mbele yenu akiwa mzima kabisa. 11 Huyu Yesu ndiye ‘lile jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilikataa, ambalo limekuwa jiwe kuu la pembeni.’ 12 Wokovu unapatikana kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani ambalo wamepewa wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina hilo peke yake tunaweza kuokolewa!”
Ujasiri Wa Petro Na Yohana Washangaza Watu
13 Wale viongozi na wazee walipoona ujasiri wa Petro na Yohana na kufahamu ya kuwa walikuwa watu wa kawaida wasio na elimu walishangaa sana. Wakatambua kwamba hawa watu walikuwa na Yesu. 14 Lakini kwa kuwa walimwona yule kilema aliyeponywa ame simama nao hawakuweza kusema lo lote kupinga maneno yao. 15 Wakawaamuru watoke nje ya ule ukumbi. 16 Kisha wakaanza kuulizana, “Tuwafanye nini watu hawa? Hatuwezi kukanusha muujiza huu mkubwa walioufanya ambao ni dhahiri kwa kila mtu Yerusalemu. 17 Lakini tunaweza kuzuia jambo hili lisiendelee kuenezwa kwa watu kama tukiwakanya wasiseme tena na mtu ye yote kwa jina la Yesu.” 18 Kwa hiyo wakawaita tena ndani wakawaamuru wasiseme au kufundisha watu tena kwa jina la Yesu.
Bora Kumtii Mungu Kuliko Wanadamu
19 Ndipo Petro na Yohana wakawajibu, “Ninyi amueni wenyewe lililo bora kutenda mbele za Mungu: kuwatii ninyi au kumtii Mungu. 20 Lakini sisi hatuwezi kuacha kusema yale tuliyoyaona na kuyasikia.”
21 Wale viongozi wakawaonya tena kwa vitisho, kisha waka waacha waende. Hawakuona njia ya kuwaadhibu kwa kuwa waliwaogopa wale watu ambao walishuhudia ule muujiza uliotendeka, nao wali kuwa wakimsifu Mungu. 22 Na yule mtu aliyeponywa alikuwa na umri wa zaidi ya miaka arobaini.
23 Mara Petro na Yohana walipoachiliwa, walirudi kwa waamini wenzao wakawaeleza waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee. 24 Waamini wote waliposikia maneno yao walimwomba Mungu kwa pamoja wakasema, “Wewe Bwana Mtukufu, uliyeumba mbingu na nchi na bahari na kila kiumbe kilichopo, 25 wewe ulitamka kwa njia ya Roho wako mtakatifu kupitia kwa baba yetu Daudi mtumishi wako, aliposema, ‘Mbona mataifa wanaghadhabika, na watu wanawaza mambo yasiyo na maana? 26 Wafalme wa dunia wamejiandaa na watawala wamekusanyika wampinge Bwana na Masihi wake.’ 27 Ndiyo sababu katika mji huu Herode na Pontio Pilato walikutana na Waisraeli wote na watu wa mataifa juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, 28 wakaamua kumfanyia yale yote ambayo wewe ulikuwa umekusudia tangu awali na kupanga kwa uweza wako yatendeke.
29 “Sasa Bwana, sikia vitisho vyao na utuwezeshe sisi wat umishi wako kuhubiri neno lako kwa ujasiri mkuu; 30 na unyooshe mkono wako ili tuweze kuponya wagonjwa na kutenda ishara na miu jiza kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.” 31 Walipokwisha kusali, nyumba waliyokuwa wamekutania ikatikisika na wote wakaja zwa na Roho Mtakatifu, wakahubiri neno la Mungu kwa ujasiri. 32 Waamini wote walikuwa na nia moja na moyo mmoja, wala hakuna aliyeona mali aliyokuwa nayo kuwa yake, bali walishirikiana vitu vyote kwa pamoja. 33 Na kwa uwezo mkubwa mitume wakashuhudia kwa ujasiri habari za kufufuka kwa Bwana Yesu. Mungu akawapa wote neema kuu. 34 Wala hakuwepo mtu ye yote miongoni mwa waamini aliyepungukiwa na kitu kwa sababu wale waliokuwa na mashamba na nyumba waliuza vyote wakaleta fedha waliyopata 35 kwa wale mitume; kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake.
36 Ndivyo ilivyokuwa kwamba Yusufu ambaye mitume walimwita Barnaba, maana yake Mwana wa Faraja, wa ukoo wa Lawi kutoka kisiwa cha Kipro 37 aliuza shamba alilokuwa nalo akaleta fedha alizopata kwa wale mitume.
Copyright © 1989 by Biblica