M’Cheyne Bible Reading Plan
Wataalamu Wa Nyota Wafika Kumwona Mtoto Yesu
2 Basi Yesu alipozaliwa katika mji wa Betlehemu huko Yudea, wakati wa utawala wa mfalme Herode, wataalamu wa mambo ya nyota kutoka Mashariki walifika Yerusalemu wakawa wakiuliza, 2 kutoka kwao kuhusu wakati kamili ambao ile nyota ilionekana.
3 Mfalme Herode alipopata habari hizi alifadhaika sana na watu wote wa Yerusalemu wakawa na hali ya wasiwasi. 4 Herode akaitisha mkutano wa makuhani wakuu na waandishi, akawataka wamweleze mahali ambapo Kristo angezaliwa.
5 Wakamjibu, “Atazaliwa Betlehemu ya Yudea, kwa maana nabii aliandika hivi kuhusu jambo hili: 6 ‘Nawe Betlehemu, katika nchi ya Yuda, wewe si wa mwisho miongoni mwa watawala wa Yuda; kwa maana atatoka mtawala kwako atakayetawala watu wangu Israeli.’ ”
7 Ndipo Herode akawaita wale wataaamu wa nyota kwa siri aka pata uhakikisho 8 Halafu akawatuma Bethlehemu akiwaagiza, “Nendeni mkamtafute huyo mtoto kwa bidii, na mkishampata, mnile tee habari ili na mimi niende kumsujudia.”
9 Baada ya kumsikiliza mfalme, wale wataalamu wa nyota wakaendelea na safari, na mbele yao wakaiona ile nyota waliyoiona mashariki ikiwatangulia, nao wakaifuata mpaka iliposimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto. 10 Walipoiona ile nyota walijawa na furaha isiyoelezeka.
11 Walipoingia ndani ya ile nyumba walimwona mtoto na mama yake Mariamu, wakainama chini kwa heshima kubwa wakamwabudu. Kisha wakafungua mikoba yao, wakampa zawadi: dhahabu, uvumba na manemane. 12 Na baada ya kuonywa katika ndoto wasirudi kwa Her ode , wakarudi makwao kwa kupitia njia nyingine.
Yosefu, Maria Na Mtoto Yesu Wakimbilia Misri
13 Walipokwisha kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto akamwambia, “Amka, umchukue mtoto na mama yake mkimbilie Misri na mkae huko mpaka hapo nitakapowaambia; kwa maana mfalme Herode ataanza msako wa kumtafuta huyu mtoto ili amwue.” 14 Kwa hiyo akaamka, akamchukua mtoto na mama yake usiku, wakaelekea Misri 15 na wakakaa huko mpaka Herode alipo fariki. Na hivyo likatimia neno alilosema Bwana hupitia nabii: ‘Nilimwita mwanangu kutoka Misri.’
16 Herode alipogundua kwamba wale wataalamu wa nyota wame mdanganya, alikasirika sana, akawatuma watu kuwaua watoto wote wa kiume wenye umri wa miaka miwili kwenda chini katika mji wa Betlehemu na sehemu zote za jirani, kufuatana na ule muda ambao wale wataalamu walikuwa wamemhakikishia. 17 Ndipo maneno yaliy osemwa hupitia nabii Yeremia yakatimia kama alivyosema:
18 “Sauti ilisikika huko Rama, kilio cha uchungu na maom bolezo; Raheli akiwalilia wanae; hakukubali kufarijiwa kwa sababu walikuwa wamekufa.”
19 Lakini Herode alipofariki, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto huko Misri, 20 akamwambia, “Amka mchukue mtoto na mama yake, mrudi katika nchi ya Israeli kwa sababu wale waliotaka kumwua mtoto wamefariki.”
21 Basi Yosefu akaamka, akamchukua mtoto na mama yake wakar udi nchi ya Israeli. 22 Lakini alipopata habari kwamba Arkelao alikuwa akimiliki huko Yudea mahali pa baba yake Herode, aliogopa kwenda huko; na baada ya kuonywa tena katika ndoto, aliondoka akaenda wilaya ya Galilaya. 23 Akaenda kuishi katika mji ulioitwa Nazareti, na hivyo yakatimia yale yaliyosemwa kupitia manabii kwamba, “Ataitwa Mnazareti.”
Kushuka Kwa Roho Mtakatifu
2 Ilipofika siku ya Pentekoste, waamini wote walikuwa wameku tana mahali pamoja. 2 Ghafla, sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliwashukia kutoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wamekaa. 3 Pakatokea kitu kama ndimi za moto ambao uligawanyika ukakaa juu ya kila mmoja wao. 4 Wote walijazwa Roho Mtakatifu wakaamza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kusema.
5 Wakati huo walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka nchi zote za dunia. 6 Waliposikia kelele hizi, walikusany ika kwa wingi. Wote walishangaa kwa sababu waliwasikia waamini wakiongea lugha ya kila mmoja wao.
7 Wakastaajabu sana, wakasema, “Hawa wote wanaozungumza ni Wagalilaya. 8 Imekuwaje basi tunawasikia wakinena lugha ya kila mmoja wetu? 9 Hapa kuna Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia, Pom filia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi. 11 Watu wen gine wametoka Krete na Uarabuni. Sisi sote tunasikia watu hawa wakisema katika lugha zetu wenyewe mambo makuu ya ajabu aliyofa nya Mungu.” 12 Wakiwa wameshangaa wakaulizana, “Ni nini maana ya mambo haya?” 13 Lakini wengine waliwadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa divai mpya!”
Mahubiri Ya Petro
14 Ndipo Petro akasimama na wale mitume kumi na mmoja, aka hutubia ule umati wa watu kwa sauti kuu akasema, “Wayahudi wen zangu na ninyi nyote mkaao Yerusalemu. Nisikilizeni kwa makini niwaambie jambo hili maana yake ni nini! 15 Hawa watu hawakulewa kama mnavyodhania, kwa maana sasa ni mapema mno, saa tatu asu buhi. 16 La, jambo hili lilitabiriwa na Nabii Yoeli aliposema, 17 ‘Mungu alisema, siku za mwisho nitawamiminia binadamu wote Roho yangu: wavulana wenu na binti zenu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wataota ndoto. 18 Ndio, hata watumishi wangu wa kiume na wa kike nitawamiminia Roho yangu, nao watata biri. 19 Nami nitafanya maajabu angani, na duniani nitaonyesha ishara, damu na moto na moshi mnene. 20 Jua litageuka kuwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya siku ya Bwana kuwa dia, siku ambayo itakuwa ya kutisha. 21 Lakini ye yote ata kayetubu na kukiri jina la Bwana, ataokoka.’
22 “Nawasihi ninyi Waisraeli mnisikilize. Yesu wa Nazareti alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa njia ya miujiza, maajabu na ishara, kama ninyi wenyewe mjuavyo. 23 Huyu Yesu ali tiwa mikononi mwenu kwa mpango na makusudi ya Mungu aliyoyafahamu tangu awali. Nanyi mlimwua kwa kumtundika na kumpigilia misumari msalabani, mkisaidiwa na watu waovu. 24 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu hata kifo kisingaliweza kumzuia. 25 Daudi alisema hivi juu yake, ‘Nilimwona Bwana akiwa mbele yangu wakati wote, Bwana yuko upande wangu wa kulia ili nisiogope. 26 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao una matumaini ya uzima. 27 Kwa maana wewe Bwana hutaniacha kuzimu; wala hutaacha mtakatifu wako ateseke na kuoza. 28 Wewe umenionyesha njia inifikishayo uzimani. Na uwepo wako ukiwepo nami nitajawa na furaha.’
29 “Ndugu zangu, nataka niwaambie wazi kwamba mfalme Daudi alikufa na kuzikwa, na kaburi lake lipo hata leo. 30 Lakini ali kuwa nabii, na alijua ya kuwa Mungu aliahidi kwa kiapo kwamba angempa mmoja wa uzao wake kiti chake cha ufalme. 31 Kwa hiyo Daudi akaona mambo ambayo yangetokea, akatamka juu ya kufufuka kwa Kristo, kwamba asingeachwa kuzimu, wala mwili wake usingehar ibiwa kwa kuoza. 32 Huyu Yesu, Mungu alimfufua, na sisi ni mash ahidi wa tukio hilo.
33 “Basi akiwa ametukuzwa na kukaa upande wa kulia wa Mungu, alipokea Roho Mtakatifu aliyeahidiwa na Baba yake. Huyo Roho Mtakatifu ndiye aliyetumiminia haya mnayoyaona na kuyasikia. 34 Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini alisema, ‘Bwana alim wambia Bwana wangu: kaa upande wangu wa kulia, 35 mpaka nitaka powafanya maadui zako kiegemezo cha miguu yako.’
36 “Basi nataka niwahakikishie Waisraeli wote ya kuwa, Mungu amemfanya huyu Yesu ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa ndiye
Ongezeko La Waamini
37 Watu waliposikia maneno haya yaliwachoma moyoni, wakawau liza Petro na wale mitume wengine, “Tufanye nini ndugu zetu?” 38 Petro aliwajibu, “Tubuni, muache dhambi na kila mmoja wenu abatizwe katika jina la Yesu Kristo, ili msamehewe dhambi zenu; nanyi mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu. 39 Kwa maana ahadi hii ilitolewa na Mungu kwa ajili yenu na watoto wenu, na wale wote walio nchi za mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu anamwita kwake.”
40 Petro aliwasihi kwa maneno mengine mengi na kuwaonya akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kiovu.” 41 Wote waliopokea ujumbe wa Petro walibatizwa na zaidi ya watu elfu tatu wal iongezeka katika kundi la waamini siku hiyo.
Ushirika Wa Waamini
42 Waamini hawa walitumia muda wao wakifundishwa na mitume, wakiishi pamoja katika ushirika, wakila pamoja na kusali. 43 Watu wote wakajawa na hofu kwa maana miujiza mingi na maajabu yalifanywa na mitume.
44 Waamini wote waliishi pamoja na kushirikiana kila kitu walichokuwa nacho kwa pamoja. 45 Waliuza mali zao na vitu waliv yokuwa navyo wakagawiana fedha walizopata, kila mtu akapata kadiri ya mahitaji yake. 46 Siku zote waliendelea kuabudu katika Hekalu na kushiriki chakula cha Bwana nyumbani mwao na kula pamoja kwa furaha na shukrani, 47 huku wakimsifu Mungu na kupendwa na watu wote. Na kila siku Bwana alikuwa akiongeza katika kundi lao watu aliokuwa akiwaokoa.
Copyright © 1989 by Biblica