M’Cheyne Bible Reading Plan
Mfano Wa Karamu Ya Harusi
22 Yesu akazungumza nao tena kwa kutumia mifano, akasema, 2 “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja ali yemwandalia mwanae karamu ya harusi. 3 Akawatuma watumishi wake wakawaite wageni walioalikwa lakini wakakataa kuja. 4 Akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni waalikwa kwamba karamu iko tayari, nimekwisha chinja fahali wangu na ng’ombe wanono kwa ajili yenu, karibuni karamuni.’ 5 Lakini waalikwa wakadharau, mmoja akaenda shambani kwake, mwingine akaenda kwenye miradi yake, 6 na wengine wakawakamata wale watumishi wakawatendea mambo ya aibu na kuwaua.
7 “Yule mfalme akakasirika, akapeleka jeshi lake likawaanga miza wale wauaji na kuteketeza mji wao. 8 Kisha akawaambia watum ishi wake, ‘Karamu ya harusi ni tayari, lakini wale niliowaalika hawakustahili kuja karamuni. 9 Kwa hiyo nendeni katika njia panda mkawaalike harusini wote mtakaowakuta.’ 10 Wale watumishi wakaenda mabarabarani wakawakusanya wote waliowakuta, wema na wabaya. Ukumbi wa sherehe ya harusi ukajaa wageni.
11 “Lakini mfalme alipoingia kutazama wageni, alimwona mle ndani mtu mmoja ambaye hakuwa amevaa vazi la harusi. 12 Mfalme akamwuliza, ‘Rafiki, umeingiaje humu bila vazi la harusi?’ Yule mtu hakuwa na la kusema. 13 Basi mfalme akawaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mikono na miguu mkamtupe nje kwenye giza. Huko kutakuwa na kilio na kusaga meno.’ 14 Kwa maana walioitwa ni wengi lakini walioteuliwa ni wachache.”
Kuhusu Kulipa Kodi
15 Mafarisayo walifanya mbinu za kumtega Yesu katika mafundi sho yake. 16 Wakatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode wakam wambie, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu wa haki na unafundisha njia za Mungu kwa uaminifu bila kumjali mtu, kwa maana cheo si kitu kwako. 17 Basi tuambie, wewe unaonaje? Ni halali, au si halali kulipa kodi kwa Kaisari?”
18 Yesu alifahamu hila yao kwa hiyo akawaambia, “Ninyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19 Nionyesheni sarafu mnayolipia kodi.” Wakamletea sarafu. 20 Yesu akawauliza, “Picha hii na sahihi hii ni za nani?” 21 Wakamjibu, “Ni za Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kais ari; na ya Mungu mpeni Mungu.”
22 Waliposikia haya wakashangaa; wakamwacha, wakaondoka.
Ufufuo Wa Wafu
23 Siku hiyo hiyo Masadukayo, wale wanaoamini kwamba wafu hawafufuki, walikuja kwa Yesu wakamwuliza, 24 “Mwalimu, Musa alitufundisha kwamba mtu akifariki pasipo kupata watoto, ndugu yake amwoe huyo mjane ili ampatie kaka yake watoto. 25 Hapa kwetu walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, kisha akafariki na kwa kuwa hakuwa na watoto, yule mjane alichukuliwa na ndugu yake. 26 Ikatokea hivyo hivyo kwa yule ndugu wa pili hadi wote saba wakamwoa huyo mjane bila kupata watoto. 27 Baadaye, yule mjane naye akafariki. 28 Sasa tuambie, siku ile ya ufufuo, ata hesabiwa kuwa ni mke wa nani? Maana aliolewa na wote saba!”
29 Yesu akawajibu, “Mnakosea kwa sababu hamjui Maandiko wala uwezo wa Mungu. 30 Wakati wa ufufuo, watu hawataoa wala kuolewa; kwa maana watakuwa kama malaika wa mbinguni. 31 Na kuhusu ufufuo wa wafu, hamjasoma Mungu alivyowaambia kwamba, 32 ‘Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? Yeye si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.”
33 Ule umati wa watu waliposikia hayo, walishangazwa sana na mafund isho yake.
Amri Kuu Kuliko Zote
34 Mafarisayo waliposikia kwamba Yesu alikuwa amewanyamazi sha Masadukayo, walikutana wakamjia pamoja. 35 Mmoja wao, mtaalamu wa sheria akajaribu kumtega kwa kumwuliza, 36 “Mwali mu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote?”
37 Yesu akamjibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote.’ 38 Hii ndio amri kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili inafanana nayo, nayo ni hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ 40 Amri hizi mbili ndio msingi wa sheria zote na Maandiko ya manabii.”
Kristo Ni Mwana Na Bwana Wa Daudi
41 Mafarisayo walipokuwa pamoja Yesu aliwauliza, 42 “Mnaonaje kuhusu Kristo? Yeye ni mwana wa nani?” Wakamjibu, “Yeye ni mwana wa Daudi.”
43 Akawaambia, “Inakuwaje basi kwamba Daudi anapozungumza kwa Roho anamwita Kristo ‘Bwana,’ kwa kusema, 44 ‘Bwana alimwam bia Bwana wangu: keti upande wangu wa kulia mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.’ 45 Kama Daudi anamwita ‘Bwana 46 Hakuna aliyeweza kumjibu Yesu hata neno moja. Na tangu siku hiyo hakuna aliyethubutu tena kum wuliza maswali.
Ushuhuda Wa Paulo Kwa Wayahudi Wa Yerusalemu
22 “Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu.” 2 Waliposikia akisema kwa lugha ya Kiebrania, wakatulia zaidi, naye akasema, 3 “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kili kia, lakini nimekulia hapa Yerusalemu, nikiwa mwanafunzi wa Gamalieli. Nilielimishwa kwa kufuata utaratibu maalumu wa sheria za baba zetu, nikiwa na ari ya kumheshimu Mungu kama ninyi mlivyo siku hii ya leo. 4 Niliwatesa wafuasi wa ‘Njia’ mpaka wakafa. Niliwakamata, waume kwa wake, nikawafunga na kuwaweka gerezani. 5 Kuhani mkuu na baraza zima la wazee ni mashahidi wangu kuhusu jambo hili. Wao ndio walionipa barua za kupeleka kwa ndugu zao huko Dameski. Kwa hiyo nilikwenda kuwakamata wafuasi wa ‘Njia’ niwalete Yerusalemu kama wafungwa ili waadhibiwe. 6 Nilipokuwa nimekaribia kufika Dameski, mnamo muda wa kama saa sita mchana, kulitokea mwanga mkali kutoka mbinguni ukaangaza pande zote kuni zunguka. 7 Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, ‘Sauli! Sauli! Mbona unanitesa?’ 8 Nikajibu, ‘Wewe ni nani Bwana?’ Naye akajibu, ‘Mimi ni Yesu wa Nazareti unayemtesa.’
9 “Wale watu niliokuwa nikisafiri nao waliona ule mwanga, lakini hawakuelewa ile sauti ya yule aliyekuwa akisema nami. 10 Nikauliza, ‘Nifanye nini Bwana?’ Naye Bwana akaniambia, ‘Inuka uingie Dameski na huko utaambiwa mambo yote uliyopangiwa kufanya.’ 11 Nilikuwa sioni kwa sababu ya ule mwanga mkali kwa hiyo wenzangu wakanishika mkono wakaniongoza na hivyo tukafika Dameski. 12 “Mtu mmoja aitwaye Anania, mtu wa dini, aliyeshika sana sheria zetu, na ambaye aliheshimiwa sana na Wayahudi wote wa Dameski, 13 alinijia akasimama karibu yangu akasema, ‘Ndugu Sauli, pokea tena uwezo wa kuona!’ Na wakati ule ule nikaweza kuona tena, nikamwona Anania. 14 Akasema, ‘Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe ufahamu mapenzi yake, umwone yeye Mwenye Haki na usikie akisema nawe kwa sauti yake mwenyewe. 15 Kwa kuwa utakuwa shahidi wake kwa watu wote uwaambie yote uliyoyaona na kuyasikia. 16 Sasa basi, mbona unakawia? Simama ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako kwa kuliitia jina lake.” ’
Wito Wa Paulo Kuwahubiri Mataifa
17 “Niliporudi Yerusalemu nikawa naomba Hekaluni 18 nilim wona katika ndoto akiniambia ‘Harakisha uondoke Yerusalemu upesi kwa sababu watu hawa hawatakubali ushuhuda wako juu yangu.’ 19 Nikajibu, ‘Bwana, wanajua jinsi nilivyokuwa nikienda katika masinagogi nikawafunga gerezani na kuwapiga wale waliokuamini wewe. 20 Na hata shahidi wako Stefano alipokuwa anauawa mimi nilikuwa nimesimama kando nikikubaliana na kitendo hicho na nikashika mavazi ya wale waliomwua. 21 Akaniambia, ‘Nenda, kwa maana nitakutuma mbali, kwa watu wa mataifa.”
22 Watu walimsikiliza Paulo mpaka hapo; kisha wakapaaza tena sauti zao wakasema, “Mwondosheni duniani! Mtu kama huyu hasta hili kuishi!” 23 Walipoendelea kupiga kelele na kupeperusha nguo zao na kutupa mavumbi juu hewani, 24 yule jemadari akaamuru wale askari wake wamwingize Paulo katika ngome na wamhoji na kum chapa viboko ili aeleze vizuri kwa nini wale Wayahudi walikuwa wanampigia makelele. 25 Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia askari aliyekuwa karibu naye, “Je, ni halali kumpiga raia wa Kirumi kabla hajahu kumiwa kwa kosa lo lote?” 26 Yule askari aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari akamwuliza, “Unajua unalolifanya? Huyu mtu ni raia wa Kirumi.” 27 Kwa hiyo yule jemadari akaja akamwuliza Paulo, “Niambie, wewe ni raia wa Kirumi?” Paulo aka jibu, “Ndio.” 28 Yule jemadari akasema, “Mimi nilinunua uraia wangu kwa fedha nyingi.” Paulo akamjibu, ‘ ‘Lakini mimi ni Mrumi wa kuzaliwa.” 29 Wale wote waliokuwa wamejiandaa kumhoji wakaondoka haraka haraka na yule jemadari akaingiwa na hofu, kwa maana alitambua ya kuwa alikuwa amemfunga raia wa Kirumi kinyume cha sheria.
Paulo Apelekwa Mbele Ya Baraza
30 Kesho yake yule jemadari alimfungua Paulo zile kamba ali zofungwa akaamuru makuhani wakuu na baraza lote likutane. Akamleta Paulo mbele yao ili apate kujua kwa nini Wayahudi wali kuwa wanamshtaki.
Copyright © 1989 by Biblica