Book of Common Prayer
1 Salamu toka kwa mzee.[a]
Kwa rafiki mpendwa gayo, mtu ni mpendae kwa dhati.
2 Rafiki yangu mpendwa, najua kwamba unaendelea vizuri kiroho, kwa hiyo ninaomba kuwa mengine yote yaendelee vizuri pia nawe uwe na afya njema. 3 Baadhi ya waamini walikuja na kunieleza juu ya kweli[b] iliyo katika maisha yako. Waliniambia kuwa unaendelea kuifuata njia ya kweli. Hili lilinifanya nijisikie furaha sana. 4 Daima hili hunipa furaha iliyo kuu ninaposikia kuwa wanangu wanaifuata njia ya kweli.
5 Rafiki yangu mpendwa, inapendeza kuwa unaonesha uaminifu wako katika kazi yako yote miongoni mwa waaminio. Wengine ambao huwajui. 6 Hao waliliambia kanisa juu ya upendo ulio nao. Tafadhali wasaidie kuendelea na safari yao. Wasaidie katika njia ambayo itampendeza Mungu. 7 Safari hiyo waliyoenda ni ya kumtumikia Kristo. Hawakupokea msaada wowote kutoka kwa watu wasioamini. 8 Hivyo inatupasa kuwasaidia. Tunapowasaidia, tunashiriki kazi yao katika ile kweli.
9 Niliandika barua kwa kanisa, ila Diotrefe hasikilizi yale tunayosema. Yeye daima anataka kuwa kiongozi. 10 Nitakapokuja, nitaongea naye mbele ya kanisa juu ya hiki anachokifanya. Anadanganya na kusema mambo mabaya juu yetu, lakini hayo siyo yote. Anakataa kuwapokea na kuwasaidia wanaoamini wanaosafiri kwenda huko. Na hawaruhusu watu wengine kuwasaidia. Kama wakifanya hivyo, anawazuia wasikusanyike na kanisa tena.
11 Rafiki yangu mpendwa, usiige lililo baya; bali iga lililo jema. Yeyote anayetenda yaliyo mema hutoka kwa Mungu. Ila yeyote anayetenda maovu bado hajamjua Mungu.
12 Kila mtu azungumza yaliyo mema juu ya Demetrio, na kweli inakubaliana na yale wasemayo. Pia, twasema mema juu yake. Na unafahamu kuwa tusemayo ni kweli.
13 Nina mambo mengi nataka kukueleza. Lakini sipendi kutumia kalamu na wino. 14 Natumaini kukutembelea hivi karibuni. Hapo tunaweza kukaa pamoja na kuongea uso kwa uso. 15 Amani kwako. Rafiki walio pamoja nami hapa wakutumia upendo wao. Tafadhali wapatie upendo wetu kila rafiki waliopo huko.
Lawi (Mathayo) Amfuata Yesu
(Mt 9:9-13; Mk 2:13-17)
27 Baada ya hayo Yesu alitoka nje akamwona mtoza ushuru amekaa sehemu yake ya kukusanyia ushuru. Jina lake aliitwa Lawi. Yesu akamwambia, “Nifuate!” 28 Lawi akasimama, akaacha kila kitu na kumfuata Yesu.
29 Lawi akaandaa chakula cha usiku nyumbani kwake kwa kumheshimu Yesu. Mezani walikuwepo watoza ushuru wengi na baadhi ya watu wengine. 30 Lakini Mafarisayo na wale wanaofundisha sheria kwa ajili ya Mafarisayo wakaanza kulalamika kwa wafuasi wa Yesu wakisema, “Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi wengine?”
31 Yesu akawajibu, “Wagonjwa ndiyo wanaohitaji daktari, si wenye afya njema. 32 Sikuja kuwaambia wenye haki wabadilike, bali wenye dhambi.”
Swali Kuhusu Kufunga
(Mt 9:14-17; Mk 2:18-22)
33 Baadhi ya watu wakamwambia Yesu, “Wafuasi wa Yohana hufunga na kuomba mara kwa mara, vivyo hivyo wafuasi wa Mafarisayo. Lakini wafuasi wako hula na kunywa kila wakati.”
34 Yesu akawaambia, “Kwenye harusi huwezi kuwaambia marafiki wa bwana harusi wafunge wakati bwana harusi bado yuko pamoja nao. 35 Lakini muda ukifika na bwana harusi akaondolewa kwao. Watakuwa na huzuni, na watafunga.”
36 Yesu akawaambia mfano huu: “Hakuna anayekata kiraka kwenye vazi jipya na kukishona kwenye vazi la zamani. Ataharibu vazi jipya, na kiraka kutoka vazi jipya hakitakuwa sawa na vazi la zamani. 37 Pia hakuna mtu anayeweka divai mpya[a] katika viriba vya zamani. Divai mpya itavipasua, divai itamwagika, na viriba vitaharibika. 38 Daima mnaweka divai mpya kwenye viriba vipya. 39 Hakuna mtu ambaye baada ya kunywa divai ya zamani hutaka divai mpya. Kwa sababu husema, ‘Divai ya zamani ni nzuri.’”
© 2017 Bible League International