Book of Common Prayer
Mkaribieni Mungu
19 Hivyo ndugu na dada, tuko huru kabisa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu. Tunaweza kufanya hivi bila hofu kwa sababu ya sadaka ya damu ya Yesu. 20 Tunaingia kwa njia mpya ambayo Yesu alitufungulia. Ni njia iliyo hai inayotuelekeza kupitia pazia; yaani mwili wa Yesu. 21 Na tunaye kuhani mkuu zaidi anayeisimamia nyumba ya Mungu. 22 Ikiwa imenyunyiziwa kwa damu ya Kristo, mioyo yetu imewekwa huru kutokana na dhamiri yenye hukumu, na miili yetu imeoshwa kwa maji safi. Hivyo mkaribieni Mungu kwa moyo safi, mkijaa ujasiri kwa sababu ya imani katika Kristo. 23 Tunapaswa kuling'ang'ania tumaini tulilonalo, bila kusitasita kuwaeleza watu juu yake. Tunaweza kumwamini Mungu kuwa atatimiza aliyoahidi.
Saidianeni Ninyi kwa Ninyi Kuwa Imara
24 Tunahitaji kumfikiria kila mtu kuona jinsi tunavyoweza kuhamasishana kuonesha upendo na kazi njema. 25 Tusiache kukutana pamoja, kama wanavyofanya wengine. Hapana, tunahitaji kuendelea kuhimizana wenyewe. Hili linazidi kuwa muhimu zaidi na zaidi kadri mnavyoona ile Siku inakaribia.
Msigeuke Mbali ya Mwana wa Mungu
26 Kama tutaamua kuendelea kutenda dhambi baada ya kujifunza ukweli, ndipo hakutakuwa sadaka nyingine itakayoondoa dhambi. 27 Tukiendelea kutenda dhambi, kitakachokuwa kimebaki kwetu ni wakati wa kutisha wa kuingoja hukumu na moto wa hasira utakaowaangamiza wale wanaoishi kinyume na Mungu. 28 Yeyote aliyekataa kuitii Sheria ya Musa alipatikana ana hatia kutokana na ushuhuda uliotolewa na mashahidi wawili au watatu. Watu wa jinsi hiyo hawakusamehewa. Waliuawa. 29 Hivyo fikiri jinsi watu watakavyostahili kuhukumiwa zaidi ambao wanaonesha kumchukia mwana wa Mungu; watu wanaoonesha kuwa hawana heshima kwa sadaka ya damu iliyoanzisha agano jipya na mara moja ikawatakasa au wale wanaomkashifu Roho wa neema ya Mungu. 30 Tunajua kuwa Mungu alisema, “Nitawaadhibu watu kwa ajili ya makosa wanayofanya”;(A) nitawalipa tu Pia alisema, “BWANA atawahukumu watu wake.”(B) 31 Ni jambo la kutiisha kukutana na hukumu kutoka kwa Mungu aliye hai.
2 Huko Yerusalemu kulikuwa na bwawa lenye mabaraza matano. Kwa Kiaramu liliitwa Bethzatha.[a] Bwawa hili lilikuwa karibu na Lango la Kondoo. 3 Wagonjwa wengi walikuwa wamelala katika mabaraza pembeni mwa bwawa. Baadhi yao walikuwa wasiyeona, wengine walemavu wa viungo, na wengine waliopooza mwili.[b] 4 Nyakati zingine malaika wa Bwana alishuka bwawani na kuyatibua maji. Baada ya hapo, mtu wa kwanza aliyeingia bwawani aliponywa ugonjwa aliokuwa nao.[c] 5 Mmoja wa watu waliolala hapo alikuwa mgonjwa kwa muda wa miaka thelathini na minane. 6 Yesu alimwona akiwa amelala hapo na kutambua kuwa amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu sana. Hivyo akamwuliza, “Je, unataka kuwa mzima?”
7 Yule mgonjwa akajibu, “Bwana, hakuna mtu wa kunisaidia kuingia kwenye bwawa mara maji yanapotibuliwa. Najitahidi kuwa wa kwanza kuingia majini. Lakini ninapojaribu, mtu mwingine huniwahi na kuingia majini kabla yangu.”
8 Kisha Yesu akasema, “Simama juu! Beba kirago chako na utembee.” 9 Mara hiyo, mtu huyo akapona. Akabeba kirago chake na kuanza kutembea.
Siku yalipotokea haya yote ilikuwa ni Siku ya Sabato.[d] 10 Hivyo baadhi ya Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato. Kulingana na sheria yetu wewe hauruhusiwi kubeba mkeka katika siku ya Sabato!”
11 Lakini yeye akajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Beba mkeka wako uende.’”
12 Wakamwuliza, “Ni nani aliyekuambia kubeba mkeka wako na kutembea?”
13 Lakini yule mtu aliyeponywa hakuwa amemfahamu ni nani. Walikuwepo watu wengi hapo, na Yesu alikwisha kuondoka.
14 Baadaye, Yesu akamwona huyo mtu Hekaluni na akamwambia, “Tazama, umepona sasa. Kwa hivyo uache kutenda dhambi tena, la sivyo jambo baya zaidi laweza kukupata.” 15 Kisha huyo mtu akaondoka na kurudi kwa wale Wayahudi waliomuuliza. Naye aliwaeleza kuwa Yesu ndiye aliyemponya.
16 Yesu alikuwa anayafanya yote haya katika siku ya Sabato. Hivyo Wayahudi hao wakaanza kumsumbua asiendelee. 17 Lakini yeye akawaambia, “Baba yangu hajawahi kuacha kufanya kazi, hivyo nami pia nafanya kazi.” 18 Hili likawafanya waongeze juhudi ya kumwua. Wakasema, “Mwanzoni mtu huyu alikuwa anavunja sheria kuhusu siku ya Sabato. Kisha akasema kwamba Mungu ni Baba yake! Yeye anajifanya kuwa yuko sawa na Mungu.”
© 2017 Bible League International