Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Zech for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
1 Wakorintho 3:10-23

10 Nami kama mjenzi stadi nilijenga msingi wa nyumba hiyo kwa kutumia karama alizonipa Mungu. Wengine wanajenga pia katika msingi huo. Lakini kila mtu lazima awe mwangalifu kwa namna anavyojenga. 11 Yesu Kristo ndiye msingi uliokwishajengwa, na hakuna yeyote anayeweza kujenga msingi mwingine. 12 Watu wanaweza kujenga juu ya msingi huo kwa kutumia dhahabu, fedha, vito vya thamani, mbao, nyasi au majani. 13 Kila kazi atakayoifanya kila mtu itaonekana siku ya hukumu itakapofika, na itaonekana ilivyo mbaya au nzuri. Siku hiyo kila kazi ya mtu itajaribiwa kwa moto. 14 Mungu atampa thawabu mtu anayejenga juu ya msingi huu ikiwa kazi yake haitateketea kwa moto. 15 Lakini ikiwa itateketea atapata hasara. Lakini yeye mwenyewe ataokolewa, lakini itakuwa kama mtu anayeokolewa kutoka kwenye moto.

16 Hakika mnajua kuwa ninyi ni hekalu la Mungu na Roho wa Mungu anaishi ndani yenu. 17 Ndiyo, ninyi nyote kwa pamoja ni Hekalu la Mungu. Na yeyote atakayeliharibu Hekalu la Mungu ataadhibiwa na Mungu, kwa sababu Hekalu la Mungu ni mali yake yeye mwenyewe.

18 Msijidanganye. Yeyote anayejiona kuwa ana hekima kwa viwango vya ulimwengu huu, basi na awe mpumbavu. Hiyo ndiyo njia pekee itakayomfanya kuwa na hekima. 19 Ninasema hivi kwa sababu hekima ya ulimwengu huu ni upumbavu kwa Mungu. Kama Maandiko yanavyosema, “Mungu huwanasa katika mitego yao wenyewe wale wanaojidhania kuwa na hekima.”(A) 20 Pia Maandiko yanasema, “Bwana anajua mawazo ya wenye hekima. Anajua kuwa mawazo yao hayana maana.”(B) 21 Hivyo hakuna mtu yeyote duniani ambaye ninyi mnapaswa kujivunia. Kila kitu ni chenu: 22 Paulo, Apolo, Petro, ulimwengu, uzima, mauti, wakati uliopo na ujao, vyote hivi ni vyenu. 23 Ninyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

Luka 18:31-43

Yesu Azungumza Tena Kuhusu Kifo Chake

(Mt 20:17-19; Mk 10:32-34)

31 Kisha Yesu alizungumza na mitume wake kumi na mbili wakiwa peke yao. Akawaaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu. Kila kitu ambacho Mungu aliwaambia manabii waandike kuhusu Mwana wa Adamu kitatokea. 32 Atakabidhiwa kwa wasio Wayahudi, ambao watamcheka, watamtukana na kumtemea mate. 33 Watamchapa kwa mijeledi kisha watamuua. Lakini katika siku ya tatu baada ya kifo chake, atafufuka kutoka kwa wafu.” 34 Mitume walijaribu kulielewa hili, lakini hawakuweza; maana yake ilifichwa wasiielewe.

Yesu Amponya Asiyeona

(Mt 20:29-34; Mk 10:46-52)

35 Yesu alipofika karibu na mji wa Yeriko, mwanaume mmoja asiyeona alikuwa amekaa kando ya barabara, akiomba pesa. 36 Aliposikia kundi la watu linapita barabarani, akauliza, “Nini kimetokea?”

37 Walimwambia, “Yesu kutoka Nazareti anapitia hapa.”

38 Kipofu akapasa sauti yake, akaita, “Yesu, Mwana wa Daudi, tafadhali nisaidie!”

39 Watu waliotangulia, wakiongoza kundi, wakamkanya asiyeona, wakamwambia anyamaze. Lakini alizidi sana kupaza sauti zaidi na zaidi, “Mwana wa Daudi, tafadhali unisaidie!”

40 Yesu alisimama pale na akasema, “Mleteni yule asiyeona kwangu!” Yule asiyeona alipofika kwa Yesu, Yesu akamwuliza, 41 “Unataka nikufanyie nini?”

Asiyeona akasema, “Bwana, nataka kuona.”

42 Yesu akamwambia, “Unaweza kuona sasa. Umeponywa kwa sababu uliamini.”

43 Yule mtu akaanza kuona saa ile ile. Akamfuata Yesu, akimshukuru Mungu. Kila mtu aliyeliona hili alimsifu Mungu.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International