Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ezra for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ufunuo 4

Yohana Aiona Mbingu

Kisha nikatazama, na mbele yangu ulikuwepo mlango uliokuwa wazi mbinguni. Na nikasikia sauti iliyosema nami mwanzoni. Ilikuwa sauti iliyosikika kama tarumbeta. Ilisema, “Njoo huku juu, nitakuonesha yale ambayo ni lazima yatokee baada ya hili.” Ghafla Roho akanichukua, na huko mbinguni kilikuwepo kiti cha enzi na mmoja amekaa juu yake. Aliyekikalia alikuwa mzuri kama mawe ya thamani, kama yaspi na karneli. Pande zote kuzunguka kiti cha enzi kulikuwa upinde wa mvua wenye rangi kama zumaridi.

Vilikuwepo viti vingine vya enzi ishirini na nne kuzunguka kiti cha enzi vilivyokaliwa na wazee ishirini na nne. Wazee walikuwa wamevaa nguo nyeupe na taji za dhahabu vichwani mwao. Mianga na ngurumo za radi vilitoka katika kiti cha enzi. Mbele ya kiti cha enzi zilikuwepo taa saba zikiwaka, ambazo ndizo Roho saba za Mungu. Pia mbele ya kiti cha enzi kilikuwepo kitu kilichoonekana kama bahari ya kioo, iiliyo angavu sana.

Mbele ya kiti cha enzi na kukizunguka pande zake zote walikuwepo viumbe wenye uhai wanne. Walikuwa na macho kila mahali. Kiumbe wa kwanza alikuwa kama simba. Wa pili alikuwa kama fahali. Wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu. Wa nne alikuwa kama tai anayeruka. Kila mmoja wa hawa wenye uhai wanne alikuwa na mabawa sita. Walikuwa na macho kila mahali, ndani na nje. Usiku na mchana hawaachi kusema:

“Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu Mwenye nguvu zote.
    Daima amekuwepo, yupo na anakuja.”

Wenye uhai hawa wanne walikuwa wanampa utukufu, heshima na shukrani yule anayekaa kwenye kiti cha enzi, anayeishi milele na milele. Na kila wakati walifanya hivyo, 10 wazee ishirini na nne waliinama mbele ya[a] yule anayekaa kwenye kiti cha enzi. Wanamwabudu anayeishi milele na milele. Wanaweka taji zao mbele ya kiti cha enzi na kusema:

11 “Bwana wetu na Mungu!
    Unastahili kupokea utukufu, heshima na nguvu.
Uliumba vitu vyote.
    Kila kinachoishi kiliumbwa kwa sababu ulitaka.”

Mathayo 13:1-9

Simulizi Kuhusu Mkulima Aliyepanda Mbegu

(Mk 4:1-9; Lk 8:4-8)

13 Siku hiyo hiyo Yesu alitoka nje ya nyumba na kukaa kando ya ziwa. Kundi kubwa wakakusanyika kumzunguka. Hivyo akapanda mtumbwini na kuketi. Watu wote wakabaki ufukweni. Kisha Yesu akatumia simulizi kuwafundisha mambo mengi. Akawaambia simulizi hii:

“Mkulima alitoka kwenda kupanda mbegu. Alipokuwa anatawanya mbegu, baadhi ziliangukia njiani. Ndege wakaja na kuzila zote. Mbegu zingine ziliangukia kwenye ardhi yenye mawe, ambako hakukuwa na udongo wa kutosha. Zikakua haraka pale, kwa sababu udongo haukuwa na kina. Lakini jua lilipowaka, likaichoma mimea. Mimea ikafa kwa sababu haikuwa na mizizi mirefu. Baadhi ya mbegu ziliangukia katikati ya miiba. Miiba ikakua na kusababisha mimea mizuri kuacha kukua. Lakini baadhi ya mbegu ziliangukia kwenye udongo wenye rutuba. Hapo zikakua na kuzaa nafaka. Baadhi ya mimea ikazaa nafaka mara mia zaidi, baadhi mara sitini na baadhi mara thelathini zaidi. Ninyi watu mnaoweza kunisikia, nisikilizeni!”

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International