Book of Common Prayer
4 Nakuamuru mbele za Mungu na mbele za Kristo Yesu, ambaye punde atawahukumu wale walio hai na wale waliokwisha kufa na juu ya kuja kwa mara ya pili kwa Kristo kwa sababu kwa hakika atatokea kuja kutawala kama Mfalme: 2 Hubiri Ujumbe, uwe tayari kutimiza wajibu wako wakati ulio sahihi hata ule usio sahihi. Wathibitishie watu kwa wanafanya makosa na uwaonye juu ya yale yatakayowatokea. Ufanye hivi kwa subira kubwa na tahadhari katika yale unayofundisha.
3 Nasema hivi kwa sababu utakuja wakati ambapo watu hawatakuwa tayari kuyasikiliza mafundisho yenye uzima. Badala yake watawatafuta walimu wanaowapendeza. Watawatafuta walimu wanaosema yale wanayotaka kusikia. 4 Na watayageuzia mbali masikio yao kutoka kwenye kweli na kugeukia simulizi za uongo. 5 Lakini wewe ujizuie mwenyewe katika mambo yote; vumilia mateso; fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema; ifanye huduma uliyopewa na Mungu.
6 Kwangu mimi, nimemiminwa kama kinywaji cha sadaka, na wakati wa kuondoka kwangu kutoka katika maisha haya umekwisha kufika. 7 Nimejihusisha katika mashindano ya thamani; nimemaliza mbio; nimeilinda imani. 8 Sasa tuzo ya mshindi inaningoja, hii ni taji inatolewa kwa wenye haki. Bwana, aliye hakimu wa haki atanipa taji hiyo katika Siku ile. Ndio atanipa mimi na yeyote mwingine anayengojea kwa dhati kuja kwake.
Yesu Amtaja Atakayemgeuka
(Mt 26:20-25; Mk 14:17-21; Lk 22:21-23)
21 Baada ya Yesu kuyasema mambo haya, alisumbuka sana moyoni. Akasema kwa uwazi, “Mniamini ninaposema kwamba mmoja wenu atanisaliti kwa maadui zangu.”
22 Wafuasi wake wote wakatazamana wao kwa wao. Hawakuelewa kuwa Yesu alikuwa anamzungumzia nani. 23 Mmoja wa wafuasi wake alikaa karibu na Yesu na alikuwa amemwegemea. Huyu alikuwa yule aliyependwa sana na Yesu. 24 Simoni Petro akaonyesha ishara kwa mfuasi huyo amwulize Yesu alikuwa anamzungumzia nani.
25 Yule mfuasi alisogea karibu sana na Yesu na kumwuliza, “Bwana, ni nani huyo?”
26 Yesu akamjibu, “Nitachovya mkate huu kwenye bakuli. Mtu yule nitakayempa mkate huo ndiye mwenyewe.” Kwa hiyo Yesu akachukua kipande cha mkate, akakichovya, na akampa Yuda Iskariote, Mwana wa Simoni. 27 Yuda alipoupokea mkate ule, Shetani akamwingia. Yesu akamwambia Yuda, “Yale unayotaka kuyafanya, yafanye haraka!” 28 Hakuna hata mmoja pale mezani aliyeelewa kwa nini Yesu alimwambia Yuda hayo. 29 Kwa vile Yuda ndiye aliyekuwa msimamizi wa fedha[a] zao,[b] baadhi yao walidhani kuwa Yesu alikuwa na maana kuwa Yuda aende kununua vitu ambavyo wangehitaji kwa ajili ya sherehe. Au walidhani kuwa Yesu alitaka Yuda aende na kuwapa maskini cho chote.
30 Yuda akaula mkate aliopewa na Yesu. Kisha akatoka nje mara hiyo hiyo. Wakati huo ulikuwa ni usiku.
© 2017 Bible League International