Book of Common Prayer
Haki Za Mtume
9 Je, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana? 2 Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni uthibitisho wa utume wangu katika Bwana. 3 Huu ndio utetezi wangu kwa hao wanaokaa kunihukumu. 4 Je? hatuna haki ya kupewa chakula na cha kunywa? 5 Je, hatuna haki ya kusafiri na mke anayeamini kama wanavyofanya mitume wengine na ndugu zake Bwana na Kefa? 6 Au ni Barnaba na mimi tu ambao tunal azimika kufanya kazi ili tuweze kupata mahitaji yetu?
7 Ni askari yupi anayelipa gharama zake mwenyewe akiwa kam bini? Ni mkulima gani anayepanda mizabibu na hali matunda yake? Ni mfugaji yupi asiyekunywa maziwa ya kundi la wanyama wake? 8 Mnadhani nasema haya kwa kutumia mifano ya kila siku tu? Je, sheria haisemi vivyo hivyo? 9 Kwa maana sheria ya Musa inasema, “Usimfunge ng’ombe kinywa wakati anapopura nafaka.” Je? Mnad hani ni ng’ombe ambaye Mungu anamfikiria? 10 Je, Mungu hasemi haya hasa kwa ajili yetu? Kwa kweli haya yalisemwa kwa ajili yetu kwa sababu mtu anapolima na mwingine akapura nafaka, wote wana paswa kufanya hivyo wakiwa na matumaini ya kupata sehemu ya mavuno. 11 Je, ikiwa sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, itakuwa ni kitu kikubwa sana iwapo tutavuna mahitaji ya mwili kutoka kwenu? 12 Kama wengine wana haki ya kupata msaada kutoka kwenu, sisi je, isingepasa tuwe na haki hiyo hata zaidi? Lakini sisi hatukupenda kutumia haki hii, bali tunavumilia kila kitu ili tusije tukaweka kizuizi kwenye Injili ya Kristo.
13 Hamjui kwamba, watu walioajiriwa kazi Hekaluni wanapata chak ula chao hekaluni, na wale wanaohudumu madhabahuni wanapata sehemu ya sadaka zinazotolewa? 14 Vivyo hivyo, Bwana aliagiza kwamba wale wanaohubiri Injili watapata chakula chao kutokana na Injili. 15 Lakini mimi sikutumia haki hizi, na wala siandiki haya ili kudai haki zangu. Ni afadhali nife, kuliko mtu aniondolee haki hii ya kujisifu.
22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’
Nyumba Iliyojengwa Kwenye Mwamba
24 “Basi, kila anayesikiliza haya maneno yangu na kuyate keleza, atafanana na mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo uka vuma ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuanguka kwa sababu ili jengwa kwenye msingi imara juu ya mwamba. 26 Na kila anayesikia haya maneno yangu asiyafuate, atafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua ikanyesha, yakatokea mafu riko, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.” 28 Na Yesu alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu waliomsikiliza walishangaa sana, 29 kwa sababu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama walimu wao wa sheria.
Copyright © 1989 by Biblica