Add parallel Print Page Options

32 Jifunze kwa mtini: Matawi yake yanapokuwa ya kijani na laini na kuanza kutoa majani mapya, ndipo mnatambua kuwa majira ya joto yamekaribia. 33 Katika namna hiyo hiyo, mtakapoona mambo haya yote yakitokea, mtajua kuwa wakati[a] umekaribia wa kile kitakachotokea. 34 Ninawahakikishia kuwa mambo haya yote yatatokea wakati ambao baadhi ya watu wa nyakati hizi wakiwa bado hai. 35 Ulimwengu wote, dunia na anga vitaangamizwa, lakini maneno yangu yatadumu milele.

Mungu Peke Yake Ndiye Ajuaye Siku ya Kurudi kwa Mwana wa Adamu

(Mk 13:32,35; Lk 17:26-30,34-36)

36 Hakuna anayeijua siku wala wakati. Malaika wa mbinguni hawaijui hata Mwana hajui itakuwa lini. Baba peke yake ndiye anayejua.

Read full chapter

Footnotes

  1. 24:33 wakati Wakati ambao Yesu aliuzungumzia ni ule ambapo kitu muhimu kitatokea. Tazama Lk 21:31, pale ambapo Yesu anasema huu ni wakati wa Ufalme wa Mungu kutufikia.