31 Kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi ya Pasaka Wayahudi hawakutaka miili yao ibaki msalabani siku ya sabato. Hii ingekuwa sabato ya pekee kwa kuwa iliangukia wakati wa Pasaka. Wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe ili wafe upesi waondolewe msalabani.

Read full chapter

31 Hii ilikuwa Ijumaa, Siku ya Matayarisho. Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya Sabato maalumu. Viongozi wa Kiyahudi hawakuitaka ile miili ya waliosulubiwa ikae juu misalabani katika siku ya Sabato. Hivyo wakamwomba Pilato atoe amri kuwa miguu ya wale watu misalabani ivunjwe. Pia wakaomba ile miili ishushwe kutoka kwenye misalaba.

Read full chapter