22 Nanyi watumwa, watiini mabwana wenu wa hapa duniani katika mambo yote; fanyeni hivyo kwa moyo safi mkimwogopa Mungu, na wala si kwa kutafuta upendeleo wakati wanapowatazama. 23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana na siyo wanadamu. 24 Kwa maana mnafahamu kwamba mtapokea urithi wenu kwa Bwana kama tuzo yenu.

Read full chapter

22 Enyi watumwa, watiini mabwana zenu katika mambo yote. Mwe watii kila wakati, hata kama wao hawawezi kuwaona. Msijifanye kazi kwa bidii ili wawatendee mema. Mnapaswa kuwatumikia mabwana[a] zenu kwa moyo kwa sababu mna hofu ya Bwana. 23 Kila kazi mnayoifanya, ifanyeni kwa bidii. Fanyeni kama mnamfanyia Bwana wenu wa mbinguni, na si kama mnamfanyia bwana wa dunia hii. 24 Mnajua kwamba mtapokea kutoka kwa Bwana ujira aliowaahidi watu wake. Ndiyo, mnamtumikia Kristo aliye Bwana[b] wenu halisi. 25 Kumbukeni kuwa Mungu hana upendeleo; kila afanyaye uovu ataadhibiwa kwa sababu ya uovu wake.

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:22 mabwana Au “wakuu wenu”.
  2. 3:24 Bwana Au “Mkuu”.