Baada ya kusema haya, akatema mate kwenye udongo aka tengeneza tope kwa mate yake akampaka yule kipofu machoni. Kisha akamwambia, “Nenda kanawe uso katika kijito cha Siloamu.” Neno ‘Siloamu’ maana yake ni ‘aliyetumwa.’ Yule kipofu akaenda akanawa na akarudi akiwa anaona!

Majirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona akiomba omba wakauliza, “Huyu si yule kipofu aliyekuwa akiketi hapa akiomba msaada?”

Read full chapter