Yohana 6:60-71
Neno: Bibilia Takatifu
Wafuasi Wengi Wamwacha Yesu
60 Wengi wa wanafunzi wake waliosikia maneno haya walisema, “Mafundisho haya ni magumu! Ni nani awezaye kukubaliana nayo?”
61 Yesu alitambua kwamba wafuasi wake walikuwa wakilalamika kuhusu mafundisho yake. Kwa hiyo akawauliza, “Mafundisho haya yanawaudhi? 62 Ingekuwaje basi, kama mngeniona mimi Mwana wa Adamu nikirudi mbinguni nilikotoka? 63 Roho wa Mungu ndiye anayetoa uzima, uwezo wa mwanadamu haufai kitu. Maneno haya ni Roho na ni uzima. 64 Lakini baadhi yenu hamuamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini na yule ambaye angemsaliti. 65 Akaendelea kusema, “Ndio sababu nili waambia kwamba hakuna awezaye kuja kwangu kama Baba hakumwe zesha.”
66 Tangu wakati huo wanafunzi wake wengi waliondoka wakaacha kumfuata. 67 Yesu akawauliza wale wanafunzi kumi na wawili, “Ninyi pia mnataka kuondoka?” 68 Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. 69 Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiye Mtakatifu wa Mungu.”
Mungu.”
70 Yesu akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni shetani!” 71 Hapa alikuwa anamsema Yuda, mwana wa Simoni Iskariote ambaye, ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, baadaye angemsaliti Yesu.
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica