45 Lakini alipofika, Wagalilaya walimpokea vizuri baada ya kuona mambo aliyofanya huko Yerusalemu wakati wa siku kuu, maana na wao walihudhuria.

46 Alikwenda tena mjini Kana katika Galilaya, kule alipo geuza maji kuwa divai. Na huko Kapernaumu alikuwapo afisa mmoja ambaye mtoto wake alikuwa mgonjwa. 47 Huyo afisa alipopata habari kuwa Yesu alikuwa amefika Galilaya kutoka Yudea, alikwenda akamwomba aje kumponya mwanae ambaye alikuwa mgonjwa karibu ya kufa.

Read full chapter