Yesu Amponya Mtoto Wa Afisa

43 Zile siku mbili zilipokwisha, Yesu aliondoka kwenda Gali laya. 44 Yesu mwenyewe alikwisha sema kwamba nabii haheshimiki nchini kwake. 45 Lakini alipofika, Wagalilaya walimpokea vizuri baada ya kuona mambo aliyofanya huko Yerusalemu wakati wa siku kuu, maana na wao walihudhuria.

46 Alikwenda tena mjini Kana katika Galilaya, kule alipo geuza maji kuwa divai. Na huko Kapernaumu alikuwapo afisa mmoja ambaye mtoto wake alikuwa mgonjwa. 47 Huyo afisa alipopata habari kuwa Yesu alikuwa amefika Galilaya kutoka Yudea, alikwenda akamwomba aje kumponya mwanae ambaye alikuwa mgonjwa karibu ya kufa.

48 Yesu akamwambia, “Ninyi watu hamwezi kuamini pasipo kuona ishara na miujiza?”

49 Yule afisa akajibu, “Bwana, tafadhali njoo kabla mwa nangu hajafa.” 50 Yesu akamwambia, “Nenda nyumbani, mwanao ataishi.” Yule afisa akaamini maneno ya Yesu, akaondoka kurudi nyumbani. 51 Alipokuwa bado yuko njiani, alikutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanae alikuwa mzima. 52 Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.” 53 Yule baba akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao ataishi.” Kwa hiyo yeye, pamoja na jamaa yake yote wakamwamini Yesu.

54 Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Yudea.

Read full chapter