23 Mkimsamehe mtu ye yote dhambi zake, atakuwa amesamehewa. Msipomsamehe, atakuwa hajasame hewa.”

Yesu Anamtokea Tomaso

24 Tomaso, aliyeitwa Pacha, hakuwepo wakati Yesu aliwatokea wanafunzi wenzake. 25 Kwa hiyo wakamwambia, “Tumemwona Bwana.” Lakini yeye akawaambia, “Sitaamini mpaka nione alama za misumari katika mikono yake na niguse kwa vidole vyangu makovu ya misumari na kuweka mkono wangu ubavuni mwake.”

Read full chapter