Font Size
Yohana 19:30-32
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yohana 19:30-32
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
30 Alipoionja ile siki, akasema, “Imekwisha.” Baada ya hapo akainamisha kichwa chake na kufa.
31 Hii ilikuwa Ijumaa, Siku ya Matayarisho. Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ya Sabato maalumu. Viongozi wa Kiyahudi hawakuitaka ile miili ya waliosulubiwa ikae juu misalabani katika siku ya Sabato. Hivyo wakamwomba Pilato atoe amri kuwa miguu ya wale watu misalabani ivunjwe. Pia wakaomba ile miili ishushwe kutoka kwenye misalaba. 32 Kwa hiyo askari wakaja na kuivunja miguu[a] ya watu wale wawili kwenye misalaba kando ya Yesu.
Read full chapterFootnotes
- 19:32 kuivunja miguu Miguu ilivunjwa ili kuwafanya wale waliokuwa misalabani wafe haraka zaidi.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Copyright © 2017 by Bible League International