38 Pilato akamwuliza Yesu, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu, “Sioni kosa lo lote ali lotenda mtu huyu.

39 Lakini kuna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachilie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mngependa nimwachilie huru huyu ‘Mfalme wa Wayahudi?” ’ 40 Wao wakapiga kelele wakisema, “Hapana, usimwachilie huyo. Tufungulie Bar aba!” Baraba alikuwa mnyang’anyi.

Read full chapter