35 Pilato akamjibu, “Unadhani mimi ni Myahudi? Watu wa taifa lako na maku hani wao wakuu wamekushtaki kwangu. Umefanya kosa gani?” 36 Ndipo Yesu akamwambia, “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Ingekuwa hivyo, watumishi wangu wangenipigania na kuhakikisha kuwa siwekwi mikononi mwa Wayahudi; lakini Ufalme wangu hautoki ulimwenguni.” 37 Pilato akasema, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema mimi ni mfalme. Nimezaliwa na nime kuja ulimwenguni kwa makusudi ya kushuhudia kweli. Mtu ye yote anayepokea yaliyo ya kweli anakubaliana na mafundisho yangu.”

Read full chapter