Font Size
Yohana 12:35-37
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yohana 12:35-37
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
35 Kisha Yesu akasema, “Nuru[a] itabaki pamoja nanyi kwa muda mfupi tu. Kwa hiyo mtembee mkiwa bado na hiyo nuru. Hapo giza[b] halitaweza kuwakamata. Watu wanaotembea gizani hawajui kule wanakoenda. 36 Hivyo wekeni matumaini yenu katika nuru wakati bado mkiwa nayo. Jinsi hiyo mtakuwa watoto wa nuru.” Yesu alipomaliza kusema mambo hayo, aliondoka na kwenda mahali ambapo watu wasingeweza kumwona.
Baadhi ya Wayahudi Wakataa Kumwamini Yesu
37 Watu wakaona ishara[c] hizi zote alizozifanya Yesu, lakini bado hawakumwamini.
Read full chapterFootnotes
- 12:35 Nuru Ina maana ya Kristo, kama katika Yh 1:5-9. Pia ni ishara ya wema na kweli unahusiana na Kristo na ufalme wake.
- 12:35 giza Giza au usiku ni ishara ya aina zote za mambo yanayoueleza ufalme wa Shetani, kama vile dhambi na maovu.
- 12:37 ishara Ni tendo la kushangaza linalodhihirisha nguvu za Mungu.
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
© 2017 Bible League International