55 Wakati Pasaka ya Wayahudi ilipokaribia, watu wengi wali toka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajita kase kabla ya sikukuu. 56 Watu walikuwa wakimtafuta Yesu, wakawa wanaulizana wakati wamesimama Hekaluni, “Mnaonaje? Mnadhani ata kuja kwenye sikukuu?” 57 Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa kama yupo mtu anayefahamu alipo awafahamisha, ili wapate kumkamata.

Mariamu Ampaka Yesu Mafuta

12 Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alikwenda mpaka Bethania ambako Lazaro aliyemfufua alikuwa anaishi. Wakamwan dalia karamu; na Martha akawahudumia. Lazaro alikuwa miongoni mwa wageni waliokaa mezani pamoja na Yesu. Kisha Mariamu akachukua chupa yenye manukato ya thamani kubwa akayamimina miguuni mwa Yesu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu ya manukato. Ndipo Yuda Iskariote, mmoja wa wanafunzi, ambaye baadaye alimsaliti Yesu, akasema, “Kwa nini manukato haya hay akuuzwa zikapatikana fedha nyingi wapewe maskini?” Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali sana maskini bali kwa kuwa alikuwa mwizi. Kama mtunza fedha, alikuwa mara kwa mara anaiba kutoka katika fedha alizokabidhiwa. Yesu akajibu, “Msimsumbue! Mwacheni ayaweke manukato hayo kwa ajili ya siku ya kifo changu. Maskini wapo pamoja nanyi siku zote ila hamtakuwa nami siku zote. ” Umati mkubwa wa Wayahudi waliposikia kwamba Yesu ali kuwa Bethania, walikuja ili pia wamwone Lazaro ambaye alimfufua. 10 Kwa hiyo makuhani wakuu wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, 11 kwa kuwa baada ya kufufuliwa kwake Wayahudi wengi wal iamua kuwakataa viongozi wao na kumwamini Yesu.

Yesu Aingia Yerusalemu Akishangiliwa

12 Kesho yake watu wengi waliokuja mjini kwa sikukuu waka pata habari kuwa Yesu angekuja Yerusalemu. 13 Basi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumpokea, huku wakiimba, “Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana! Mungu ambar iki Mfalme wa Israeli!” 14 Yesu akampata mwanapunda akampanda, kama ilivyoandikwa katika Maandiko, 15 “Usiogope, wewe mwenyeji wa Sioni. Tazama, mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda!”

16 Wanafunzi wa Yesu hawakuelewa mambo haya wakati huo, lakini Yesu alipofufuka kwa utukufu walikumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yametajwa katika Maandiko; na kwamba waliyatekeleza kwa ajili yake. 17 Wale waliokuwepo wakati Yesu alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua, baadaye waliwasimulia wengine yaliy otokea. 18 Ndio sababu watu wengi walitoka kwenda kumpokea, kwa kuwa walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu. 19 Mafarisayo walipoona haya wakaambiana, “Mnaona? Hakuna tun aloweza kufanya; ulimwengu wote unamfuata!”