Yohana 10
Neno: Bibilia Takatifu
Mchungaji Mwema
10 “Ninawaambia hakika, mtu asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya ndani kwa kupitia njia nyin gine, ni mwizi na mnyang’anyi. 2 Anayepitia mlangoni ndiye mchun gaji wa kondoo. 3 Mlinzi humfungulia mlango na kondoo hutambua sauti yake. Yeye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwaongoza nje ya zizi. 4 Akiisha watoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaifahamu sauti yake. 5 Kondoo hawam fuati mtu wasiyemfahamu bali humkimbia, kwa sababu hawatambui sauti ya mgeni.” 6 Yesu alitumia mfano huu lakini wao hawakuel ewa maana yake.
7 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni mlango wa kupitia kondoo. 8 Wote walionitangulia ni wezi na wany ang’anyi. Hata hivyo kondoo hawakuwafuata. 9 Mimi ni mlango; mtu ye yote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu atakuwa salama, naye ataingia na kutoka na kupata malisho. 10 Mwizi huja kwa nia ya kuiba, kuua na kuharibu. Nimekuja ili watu wapate uzima; uzima ulio kamili. 11 Mimi ni Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema hutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtu wa kuajiriwa anapoona mbwa mwitu akija, hukimbia na kuwaacha kondoo hatarini kwa kuwa kondoo si wake, naye si mchungaji wao; na hivyo mbwa mwitu huwar ukia kondoo na kuwatawanya. 13 Yeye hukimbia kwa sababu ameaji riwa tu na hawajali kondoo.
14 Mimi ni Mchungaji Mwema: ninawafahamu kondoo wangu nao wananifahamu, 15 kama vile Baba yangu anavyonifahamu na mimi ninamfahamu. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili; nao pia itanibidi niwalete, nao wataisikia sauti yangu. Hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 17 Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 18 Hakuna mtu atakayeondoa uhai wangu, bali ninautoa mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuuchukua tena. Hii ni amri niliyopo kea kutoka kwa Baba yangu.”
19 Maneno haya yalisababisha mafarakano tena kati ya Way ahudi. 20 Wengi wao walisema, “Huyu amepagawa na shetani, kwa nini tuendelee kumsikiliza?” 21 Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na shetani. Je, shetani anaweza kumpo nya kipofu?”
Yesu Anajitambulisha
22 Ilikuwa sikukuu ya Utakaso wa Hekalu wakati wa majira ya baridi, 23 na Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Sulemani. 24 Wayahudi wakamzunguka wakamwuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo utuambie wazi wazi.” 25 Yesu akawajibu, “Nimewaambia lakini hamuamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yan anishuhudia. 26 Lakini hamuamini kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 27 Kondoo wangu husikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata; 28 nami ninawapa uzima wa milele. Hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu. 29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32 Yesu akawauliza, “Nimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?” 33 Wao wakamjibu, “Tunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”
Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”
34 Yesu akawauliza, “Je, haikuandikwa katika Maandiko yenu ya sheria, ‘Nimesema, ninyi ni miungu’? 35 Ikiwa Maandiko, ambayo ni kweli daima, yanawataja wale waliyoyapokea kuwa ni ‘miungu 36 itakuwaje mseme ninakufuru ninaposema ‘mimi ni Mwana wa Mungu,’ ambapo mimi Baba ameniteua niwe wake na akani tuma ulimwenguni? 37 Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msi niamini; 38 lakini ikiwa nafanya kazi za Mungu, mziamini hizo; hata kama hamniamini mimi. Mkifanya hivyo, mtaelewa na kutambua kuwa Baba yangu yuko ndani yangu na mimi ni ndani yake.”
39 Kwa mara nyingine Wayahudi wakajaribu kumkamata, lakini yeye aka waponyoka.
40 Kisha akaenda ng’ambo ya mto Yordani mpaka pale mahali ambapo Yohana alianzia kubatiza, akakaa huko. 41 Watu wengi wakamfuata, nao wakawa wakiambiana, “Yohana hakufanya muujiza wo wote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 42 Na wengi wakamwamini Yesu.
Yohana 11
Neno: Bibilia Takatifu
Kifo Cha Lazaro
11 Palikuwa na mtu mmoja jina lake Lazaro ambaye aliugua. Yeye aliishi katika kijiji cha Bethania pamoja na dada zake wawili, Mariamu na Martha. 2 Huyu Mariamu ndiye aliyempaka Bwana Yesu manukato miguuni na kumpangusa kwa nywele zake. 3 Hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Yesu kumwambia, “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa sana.” 4 Lakini Yesu alipopata habari hizi alisema, “Ugonjwa huu hautaleta kifo bali umetokea ili kudhihirisha utu kufu wa Mungu. Kutokana na ugonjwa huu, mimi Mwana wa Mungu, nitatukuzwa. ”
5 Kwa hiyo ijapokuwa Yesu aliwapenda Martha, Mariamu na Lazaro, 6 alipopata habari kuwa Lazaro ni mgonjwa, aliendelea kukaa huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi. 7 Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni tena Yudea.” 8 Wanafunzi wake wakam wambia, “Mwalimu, utakwendaje tena Yudea ambako siku chache tu zilizopita Wayahudi walitaka kukupiga mawe?” 9 Yesu akawajibu, “Si kuna masaa kumi na mawili ya mchana katika siku moja? Mtu akitembea mchana hawezi kujikwaa kwa maana kuna mwanga wa ulim wengu. 10 Lakini mtu akitembea usiku hujikwaa kwa sababu hana mwanga nafsini mwake.”
11 Baada ya kusema haya Yesu aliongezea kusema, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini nakwenda kumwamsha.”
2 Wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala bila shaka atapona.” 13 Yesu alikuwa amemaanisha kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa. Walidhani amesema Lazaro amelala usingizi. 14 Kwa hiyo Yesu akawaambia wazi wazi, “Lazaro amekufa. 15 Hata hivyo nafurahi sikuwepo kabla Lazaro kufa. Hii itakuwa kwa faida yenu, ili muweze kuamini. Lakini sasa twendeni.” 16 Tomaso aliyeitwa Pacha akawaambia wanafunzi wenzake, “Na sisi pia twendeni tukafe pamoja naye.”
Yesu Ni Ufufuo Na Uzima
17 Yesu alipowasili alikuta Lazaro alikwisha zikwa siku nne zilizopita. 18 Kwa kuwa kijiji cha Bethania kilikuwa umbali wa kama kilometa tatu tu kutoka Yerusalemu, 19 Wayahudi wengi wal ikuwa wametoka mjini kuja kuwafariji Martha na Mariamu kwa kifo cha ndugu yao. 20 Martha aliposikia Yesu amefika, alitoka kwenda kumpokea, ila Mariamu akabaki amekaa ndani. 21 Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu hangali kufa. 22 Na hata sasa ninafahamu kuwa cho chote utakachomwomba Mungu, atakutimizia.” 23 Yesu akamwambia, “Kaka yako atakuwa hai tena.” 24 Martha akamjibu, “Ndio, ninajua ya kuwa atakuwa hai tena wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” 25 Yesu akamwambia, “Mimi ndiye ufufuo na uzima; mtu akiniamini mimi, hata akifa ataishi; 26 na ye yote anayeishi akiwa ananiamini hatakufa kamwe. Je, unaamini haya?” 27 Martha akajibu, “Ndio Bwana; ninaamini ya kuwa wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye ange kuja ulimwenguni.”
Yesu Analia
28 Baada ya kusema haya Martha alikwenda akamwita Mariamu kando akamwambia, “Mwalimu amefika na anakuita.” 29 Mariamu akaondoka upesi akaenda alipokuwa Yesu. 30 Yesu alikuwa bado hajaingia kijijini. Alikuwa bado yuko pale Martha alipokutana naye. 31 Wale Wayahudi waliokuwa wakimfariji Mariamu walipoona ameondoka haraka, walidhani anakwenda kaburini kuomboleza, kwa hiyo wakamfuata. 32 Mariamu alipomwona Yesu aliinama chini kwa heshima akasema, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, ndugu yangu han galikufa.” 33 Yesu alipomwona Mariamu akilia na wale Wayahudi waliokuja naye pia wanalia, alifadhaika sana moyoni; 34 akau liza, “Mmemzika wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo uone.” 35 Yesu akalia. 36 Wale Wayahudi wakasema, “Tazameni jinsi alivyompenda Lazaro!” 37 Lakini wengine wakasema, “Alimponya kipofu, kwa nini hakuweza kuzuia Lazaro asife?”
Yesu Amfufua Lazaro
38 Yesu akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana. Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake ulikuwa umezibwa kwa jiwe. 39 Akasema, “Ondoeni hilo jiwe.” Dada yake mare hemu, Martha, akasema, “Bwana, patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita tangu azikwe.” 40 Yesu akamjibu, “Sikukuam bia kama ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?” 41 Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru kwa kunisikia. 42 Ninajua ya kuwa huwa unanisikia wakati wote, lakini nimesema hivi kwa faida ya hawa walio hapa, ili wapate kuamini ya kuwa umenituma.” 43 Baada ya kusema haya akapaaza sauti akaita, “Lazaro, toka nje!” 44 Yule aliyekuwa amekufa akatoka, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa. Yesu akawaambia, “Mfungueni awe huru!”
Mpango Wa Kumwua Yesu
45 Wayahudi wengi waliokuja kumfariji Mariamu, walipoona yaliyotokea wakamwamini Yesu. 46 Lakini wengine walikwenda kwa Mafarisayo wakawaambia mambo Yesu aliyofanya. 47 Kwa hiyo maku hani wakuu na Mafarisayo wakafanya baraza wakaulizana, “Tufa nyeje? Huyu mtu anafanya ishara nyingi. 48 Kama tukimruhusu aendelee hivi, kila mtu atamwamini; na Warumi watakuja kuharibu Hekalu letu na taifa letu.” 49 Lakini mmoja wao, aliyeitwa Kayafa, ambaye alikuwa kuhani mkuu kwa mwaka ule akawaambia wen zake, “Ninyi hamjui kitu! 50 Hamwoni kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, badala ya taifa lote kuangamia?” 51 Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama kuhani mkuu mwaka ule, alikuwa anatabiri kuwa Yesu angekufa kwa ajili ya Wayahudi; 52 na pia kwa ajili ya watoto wa Mungu wal iotawanyika ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe wamoja. 53 Tangu siku hiyo viongozi wa Wayahudi wakawa wanafanya mipango ili wamwue Yesu. 54 Kwa hiyo Yesu akawa hatembei hadharani, bali alitoka Bethania akaenda mikoani karibu na jangwa, kwenye kijiji kimoja kiitwacho Efraimu. Alikaa huko na wanafunzi wake.
55 Wakati Pasaka ya Wayahudi ilipokaribia, watu wengi wali toka vijijini wakaenda Yerusalemu kabla ya Pasaka ili wakajita kase kabla ya sikukuu. 56 Watu walikuwa wakimtafuta Yesu, wakawa wanaulizana wakati wamesimama Hekaluni, “Mnaonaje? Mnadhani ata kuja kwenye sikukuu?” 57 Makuhani wakuu na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kuwa kama yupo mtu anayefahamu alipo awafahamisha, ili wapate kumkamata.
Copyright © 1989 by Biblica