34 Yesu akawaambia, “Ukweli ni kwamba, mtu ye yote anayetenda dhambi ni mtumwa wa dhambi. 35 Mtumwa hana haki ya kuishi siku zote katika nyumba anapotumika, lakini mwana ana haki zote katika nyumba ya baba yake. 36 Kwa hiyo, kama Mwana akiwafanya muwe huru, mtakuwa huru kweli.

Read full chapter