Add parallel Print Page Options

Yesu Azungumza na Mwanamke Msamaria

Yesu akatambua ya kwamba Mafarisayo wamesikia habari kuwa alikuwa anapata wafuasi wengi kuliko Yohana na kuwabatiza. (Lakini kwa hakika, Yesu mwenyewe hakumbatiza mtu yeyote huko; bali wafuasi wake ndiyo waliowabatiza watu kwa niaba yake.) Hivyo akaondoka Uyahudi na kurudi Galilaya.

Barabara ya kuelekea Galilaya ilimpitisha Yesu katikati ya nchi ya Samaria. Akiwa Samaria Yesu akafika katika mji wa Sikari, ulio karibu na shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yusufu. Mahali hapo ndipo kilikuwapo kisima cha Yakobo. Kutokana na safari yake kuwa ndefu Yesu alichoka, hivyo akakaa chini kando ya kisima. Nayo ilikuwa saa sita adhuhuri. Baadaye mwanamke Msamaria akaja kisimani hapo kuchota maji, na Yesu akamwambia, “Tafadhali nipe maji ninywe.” Hili lilitokea wakati wafuasi wake walipokuwa mjini kununua chakula.

Mwanamke yule akajibu, “Nimeshangazwa wewe kuniomba maji unywe! Wewe ni Myahudi nami ni mwanamke Msamaria!” (Wayahudi hawana uhusiano na Wasamaria.[a])

10 Yesu akajibu, “Hujui kile Mungu anachoweza kukukirimu. Na hunijui mimi ni nani, niliyekuomba maji ninywe. Kama ungejua, nawe ungekuwa umeniomba tayari, nami ningekupa maji yaletayo uzima.”

11 Mwanamke akasema, “Bwana, utayapata wapi maji yaliyo hai? Kisima hiki kina chake ni kirefu sana, nawe huna kitu cha kuchotea. 12 Je, wewe ni mkuu kumzidi baba yetu Yakobo? Yeye ndiye aliyetupa kisima hiki. Yeye alikunywa kutoka kisima hiki, na wanawe, na wanyama wake wote.”

13 Yesu akajibu, “Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena. 14 Bali yeyote anayekunywa maji ninayompa mimi hatapata kiu tena. Maji ninayowapa watu yatakuwa kama chemichemi inayobubujika ndani yao. Hayo yatawaletea uzima wa milele.”

15 Mwanamke akamwambia Yesu, “Bwana, nipe maji hayo. Kisha sitapata kiu na sitapaswa kuja tena hapa kuchota maji.”

16 Yesu akamwambia, “Nenda kamwite mumeo kisha urudi naye hapa.”

17 Mwanamke akajibu, “Lakini mimi sina mume.”

Yesu akamwambia, “Uko sahihi kusema kuwa huna mume. 18 Hiyo ni kwa sababu, hata kama umekuwa na waume watano, mwanaume unayeishi naye sasa sio mume wako. Huo ndiyo ukweli wenyewe.”

19 Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona ya kuwa wewe ni nabii. 20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu. Lakini ninyi Wayahudi mnasema kuwa Yerusalemu ndipo mahali ambapo watu wanapaswa kuabudia.”

21 Yesu akasema, “Mwanamke! Niamini mimi, wakati unakuja ambapo hamtakwenda Yerusalemu wala kuja kwenye mlima huu kumwabudu Baba. 22 Ninyi Wasamaria hamwelewi mambo mengi kuhusu yule mnayemwabudu. Sisi Wayahudi tunamfahamu vizuri tunayemwabudu, kwa maana njia yake ya kuuokoa ulimwengu imepatikana kupitia Wayahudi. 23 Lakini wakati unakuja wenye nia halisi ya kuabudu watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa hakika, wakati huo sasa umekwishafika. Na hao ndiyo watu ambao Baba anataka wamwabudu. 24 Mungu ni roho. Hivyo wote wanaomwabudu wanapaswa kumwabudu katika roho na kweli.”

25 Mwanamke akasema, “Naelewa kwamba Masihi anakuja.” (Ndiye anayeitwa Kristo.)

“Atakapokuja, atatufafanulia kila kitu.”

26 Kisha Yesu akasema, “Mimi ninayezungumza nawe sasa, ndiye Masihi.”

27 Wakati huo huo wafuasi wa Yesu wakarudi toka mjini. Nao walishangaa kwa sababu walimwona Yesu akiongea na mwanamke. Lakini hakuna aliyemwuliza yule mwanamke, “Unataka nini?” Wala Yesu, “Kwa nini unaongea naye?”

28 Yule mwanamke akauacha mtungi wake wa maji na kurudi mjini. Akawaambia watu kule, 29 “Mwanaume mmoja amenieleza mambo yote niliyowahi kuyafanya. Njooni mkamwone. Inawezekana yeye ndiye Masihi.” 30 Hivyo wale watu wakatoka mjini wakaenda kumwona Yesu!

31 Wakati huyo mwanamke akiwa mjini, wafuasi wa Yesu wakamsihi Bwana wao wakamwambia, “Mwalimu, ule chakula chochote.”

32 Lakini Yesu akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkijui.”

33 Hapo wafuasi wake wakaulizana, “Kwani kuna mtu yeyote hapa aliyemletea chakula mapema?”

34 Yesu akasema, “Chakula changu ni kuimaliza kazi ile ambayo aliyenituma amenipa niifanye. 35 Mnapopanda mimea, huwa mnasema, ‘Bado miezi minne ya kusubiri kabla ya kuvuna mazao.’ Lakini mimi ninawaambia, yafumbueni macho yenu na kuyaangalia mashamba. Sasa yako tayari kuvunwa. 36 Hata sasa, watu wanaovuna mazao wanalipwa. Wanawaleta ndani wale watakaoupata uzima wa milele. Ili kwamba watu wanaopanda waweze kufurahi wakati huu pamoja na wale wanaovuna. 37 Ni kweli tunaposema, ‘Mtu mmoja hupanda, lakini mwingine huvuna mazao.’ 38 Mimi niliwatuma kukusanya mazao ambayo ninyi hamkuyahangaikia. Wengine waliyahangaikia, nanyi mnapata faida kutokana na juhudi na kazi yao.”

39 Wasamaria wengi katika mji huo wakamwamini Yesu. Wakaamini kutokana na yale ambayo walisikia yule mwanamke akiwaambia juu ya Yesu. Aliwaambia, “Yeye amenieleza mambo yote niliyowahi kuyafanya.” 40 Wasamaria wakaenda kwa Yesu. Wakamsihi akae pamoja nao. Naye akakaa nao kwa siku mbili. 41 Watu wengi zaidi wakamwamini Yesu kutokana na mambo aliyoyasema.

42 Watu hao wakamwambia mwanamke, “Mwanzoni tulimwamini Yesu kutokana na jinsi ulivyotueleza. Lakini sasa tunaamini kwa sababu tumemsikia sisi wenyewe. Sasa tunajua kwamba hakika Yeye ndiye atakayeuokoa ulimwengu.”

Yesu Amponya Mwana wa Afisa

(Mt 8:5-13; Lk 7:1-10)

43 Siku mbili baadaye Yesu akaondoka na kwenda Galilaya. 44 (Yesu alikwishasema mwanzoni kwamba nabii huwa haheshimiwi katika nchi yake.) 45 Alipofika Galilaya, watu wa pale walimkaribisha. Hao walikuwepo kwenye sikukuu ya Pasaka kule Yerusalemu na waliona kila kitu alichofanya huko.

46 Naye Yesu akaenda tena kutembelea Kana huko Galilaya. Kana ni mahali alikoyabadili maji kuwa divai. Mmoja wa maafisa muhimu wa mfalme alikuwa anaishi katika mji wa Kapernaumu. Mwanawe afisa huyu alikuwa mgonjwa. 47 Afisa huyo akasikia kwamba Yesu alikuwa amekuja kutoka Uyahudi na sasa yuko Galilaya. Hivyo akamwendea Yesu na kumsihi aende Kapernaumu kumponya mwanawe, aliyekuwa mahututi sana. 48 Yesu akamwambia, “Ninyi watu ni lazima muone ishara zenye miujiza na maajabu kabla ya kuniamini.”

49 Afisa wa mfalme akasema, “Bwana, uje kabla mwanangu mdogo hajafa.”

50 Yesu akajibu, “Nenda, mwanao ataishi.”

Mtu huyo akayaamini maneno Yesu aliyomwambia na akaenda nyumbani. 51 Akiwa njiani kwenda nyumbani watumishi wake wakaja na kukutana naye. Wakasema, “Mwanao ni mzima.”

52 Mtu huyo akauliza, “Ni wakati gani mwanangu alipoanza kupata nafuu?”

Wakajibu, “Ilikuwa jana saa saba mchana homa ilipomwacha.”

53 Baba yake akatambua kuwa saa saba kamili ulikuwa ndiyo ule wakati aliposema, “Mwanao ataishi.” Hivyo afisa huyo na kila mmoja katika nyumba yake wakamwamini Yesu.

54 Huo ulikuwa muujiza wa pili ambao Yesu aliufanya baada ya kufika kutoka Uyahudi na Galilaya.

Footnotes

  1. 4:9 Wayahudi … Wasamaria Au “Wayahudi hawatumii vitu ambavyo Wasamaria wametumia.”

Yesu Na Mwanamke Msamaria

Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kuba tiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana. Lakini kwa hakika Yesu hakubatiza, wanafunzi wake ndio waliokuwa wakibatiza watu. Bwana alipopata habari hizi aliondoka Yudea akarudi Galilaya. Katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria.

Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu. Kisima cha Yakobo kilikuwa hapo na kwa kuwa Yesu alikuwa amechoka kutokana na safari, aliketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

Mama mmoja Msamaria akaja kuteka maji na Yesu akamwambia, “Naomba maji ya kunywa.” Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula. Yule mama akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” -Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria. 10 Yesu akamjibu, “Kama ungelifahamu Mungu anataka kukupa nini, na mimi ninayekuomba maji ya kunywa ni nani, ungeliniomba nikupe maji ya uzima.”

11 Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kuchotea maji na kisima hiki ni kirefu . Hayo maji ya uzima utay apata wapi? 12 Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”

13 Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. 14 Lakini ye yote atakayekunywa maji nitakay ompa mimi, hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa kama chemchemi itakayobubujika maji yenye uhai na kumpa uzima wa milele.”

15 Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuchota maji!”

16 Yesu akamjibu, “Nenda kamwite mumeo, kisha uje naye hapa.” 17 Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Yesu akamwam bia, “Umesema kweli kuwa huna mume. 18 Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanamume unayeishi naye sasa si mume wako!”

19 Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. 20 Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu lakini ninyi Way ahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”

21 Yesu akamjibu, “Mama, niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. 22 Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwab udu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. 23 Lakini wakati unakuja, tena umekwisha timia, ambapo wale wanaoabudu inavyostahili watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu kwa njia hii ndio anaowataka Baba. 24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” 25 Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masihi, aitwaye Kristo, anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”

26 Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye Masihi.”

Masihi.”

27 Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kum wona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemwuliza, “Unataka nini kwake?” au “Kwa nini unazungumza naye?”

28 Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaam bia watu, 29 “Njooni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote nili yowahi kufanya! Je, yawezekana huyu ndiye Masihi?”

30 Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.

31 Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau cho chote.”

32 Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”

33 Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?” 34 Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma, na kuikamilisha kazi yake. 35 Si mnao msemo kwamba, ‘Bado miezi minne tutavuna’? Hebu yaangalieni mashamba, jinsi mazao yalivyoiva tayari kuvunwa! 36 Mvunaji hupokea ujira wake, naye hukusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele. Kwa hiyo aliyepanda mbegu na anayevuna, wata furahi pamoja. 37 Ule msemo wa zamani kwamba , ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa. 38 Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi hiyo; ninyi mmefaidika kutokana na jasho lao!”

39 Wasamaria wengi walimwamini kutokana na ushuhuda wa yule mama alipowaambia kwamba, “Ameniambia mambo yote niliyowahi kutenda.” 40 Kwa hiyo wale Wasamaria walipokuja, walimsihi akae kwao, naye akakaa kwa siku mbili. 41 Watu wengi zaidi wakamwa mini kutokana na ujumbe wake. 42 Wakamwambia yule mama, sasa hatuamini tu kwa sababu ya yale uliyotuambia bali kwa kuwa tumem sikia sisi wenyewe, na tunajua hakika kwamba yeye ni Mwokozi wa ulimwengu.”

Yesu Amponya Mtoto Wa Afisa

43 Zile siku mbili zilipokwisha, Yesu aliondoka kwenda Gali laya. 44 Yesu mwenyewe alikwisha sema kwamba nabii haheshimiki nchini kwake. 45 Lakini alipofika, Wagalilaya walimpokea vizuri baada ya kuona mambo aliyofanya huko Yerusalemu wakati wa siku kuu, maana na wao walihudhuria.

46 Alikwenda tena mjini Kana katika Galilaya, kule alipo geuza maji kuwa divai. Na huko Kapernaumu alikuwapo afisa mmoja ambaye mtoto wake alikuwa mgonjwa. 47 Huyo afisa alipopata habari kuwa Yesu alikuwa amefika Galilaya kutoka Yudea, alikwenda akamwomba aje kumponya mwanae ambaye alikuwa mgonjwa karibu ya kufa.

48 Yesu akamwambia, “Ninyi watu hamwezi kuamini pasipo kuona ishara na miujiza?”

49 Yule afisa akajibu, “Bwana, tafadhali njoo kabla mwa nangu hajafa.” 50 Yesu akamwambia, “Nenda nyumbani, mwanao ataishi.” Yule afisa akaamini maneno ya Yesu, akaondoka kurudi nyumbani. 51 Alipokuwa bado yuko njiani, alikutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanae alikuwa mzima. 52 Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.” 53 Yule baba akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao ataishi.” Kwa hiyo yeye, pamoja na jamaa yake yote wakamwamini Yesu.

54 Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Yudea.